Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • w76 6/1 kur. 244-246
  • Kula Viapo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kula Viapo
  • Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
  • Habari Zinazolingana
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2022
  • Maswali Kutoka kwa Wasomaji
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Mtii Mungu Ili Ufaidike Kutokana Na Ahadi Zake Zenye Kiapo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2012
  • Kiapo cha Kale Ambacho Ni Muhimu Leo
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1976
w76 6/1 kur. 244-246

Kula Viapo

KIAPO kimeelezwa kuwa “ombi zito kwa Mungu, au kwa mtu au kitu fulani chenye kuheshimiwa sana, linalofanywa kutoa ushahidi wa uamuzi wa mtu kusema kweli au kutimiza ahadi.” Wewe waonaje juu ya kula viapo? Vikundi fulani vya kidini, kama Mennonites na Quakers hukataa kula viapo. Na kwa kuwa watu wengine hukataa kula kiapo kwa sababu ya dhamiri, mara nyingi hukubaliwa kufanya tangazo zito la kisheria badala ya kula kiapo.

Watu wengine wamesema kwa uthabiti kwamba maneno aliyosema Yesu Kristo katika Mahubiri juu ya Mlima hukataza wafuasi wake wasile viapo. Yesu alisema hivi: “Tena mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usizuri [usiape kwa uongo], ila mtimizie Bwana nyapo zako; lakini mimi nawaambia, Usiape kabisa; hata kwa mbingu, kwa maana ndicho kiti cha enzi cha Mungu; wala kwa nchi, kwa maana ndiyo pa kuwekea miguu yake; wala kwa Yerusalemu, kwa maana ndio mji wa Mfalme mkuu. Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. Bali maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo; kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.”​—⁠Mt. 5:33-37; linganisha Yakobo 5:12.

Je! Yesu alimaanisha ni vibaya kwa wafuasi wake kula viapo vya aina yo yote? Sivyo, hatuwezi kukata maneno hivyo, kwa sababu mbalimbali. Fikiri: Zaidi ya mara 50 Yehova Mungu mwenyewe atajwa katika Maandiko akila viapo. Kwa mfano, mwandikaji wa Kikristo wa barua kwa Waebrania alionyesha kwamba wakati “Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza.” (Ebr. 6:13-18) Biblia yaonyesha wanadamu pia wamekula viapo vyenye kukubaliwa na Yehova. Ibrahimu aliapa kwa Mungu, na chini ya hali fulani sheria ya Musa ilitaka watu mmoja mmoja wale viapo. (Mwa. 21:23, 24; Kut. 22:10, 11; Hes. 5:21, 22) Hata Yesu Kristo hakupinga, bali alijibu hivi wakati kuhani mkuu wa Kiyahudi aliponena: “Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.” (Mt. 26:63, 64) Kwa hiyo, tutayaelewaje maneno ya Yesu juu ya kuapa?

Tafadhali angalia kwamba Kristo alitaja kuapa kwa mbingu, nchi, Yerusalemu na hata kichwa cha mtu. Kwa wazi, watu wengi walioishi wakati wa huduma ya kidunia ya Yesu walitilia mkazo kila usemi kwa kuapa. Ilikuwa kana kwamba ni lazima usemi ufanyiwe kiapo ndiyo uaminiwe. Viapo hivyo havikuwa vya lazima ndiyo watu wawe wasema kweli na kumaanisha mambo waliyosema. Hivyo, kwa kusema, “Maneno yenu yawe Ndiyo, ndiyo; Siyo, siyo,” Kristo alimaanisha kwamba watu wamepaswa kuwa wanyofu katika usemi wao. Haionekani kwamba alikuwa akipinga kula viapo vizito kortini (barazani).

Wakristo wenye kufikiri hulichunguza jambo hili kwa msaada wa kanuni za Biblia kabla hawajala kiapo cho chote. Wafanyapo hivyo, wao huona kwamba viapo vingine havikubaliwi na Maandiko. Kwa mfano, siku za Utawala wa Hitler, kila askari Mjeremani alitakiwa ale kiapo hiki: “Naapa kwa Mungu kiapo hiki kitakatifu kwamba nitatii bila masharti Kiongozi wa Utawala wa Ujeremani na watu wake, Adolf Hitler, Amiri Mkuu wa Majeshi, na kwamba kama askari shujaa nitakuwa tayari nyakati zote kuhatirisha maisha yangu kwa ajili ya kiapo hiki.” Mtu aliye wakf kwa Mungu Mwenye Nguvu Zote hawezi kujifunga bila masharti kwa mwanadamu mwenye dhambi, kwa maana Yehova hutaka “ibada ya pekee.” (Kum. 5:9) Zaidi ya hilo, je! ingefaa Mkristo wa kweli, ambaye Yesu alisema angekuwa “si wa ulimwengu,” ajiingize katika magomvi ya ulimwengu? (Yohana 15:19; Yak. 1:27; Isa. 2:4) Hivyo, ijapokuwa waliteswa, mashahidi waaminifu wa Kikristo wa Yehova katika Ujeremani walikataa kula viapo vyenye kuwafunga kwa Adolf Hitler.

Kwa hiyo, Mkristo wa kweli hawezi kula kiapo kitakachomtia katika magomvi ya ulimwengu au kitakachomtiisha kwa mapenzi ya mwanadamu mwingine. Lakini namna gani taifa likitaka kiapo kiliwe na wanaotaka kuwa raia? Je! mtu aliye wakf kwa Mungu aweza kula kiapo cha aina hiyo akiwa na masharti akilini, akiwaza kwamba sex yake (kuwa kwake mwanamke au mwanamume), umri wake au mambo mengine yatafanya iwe vigumu kwake kuombwa atimize aliyoapa? Lazima mtu mwenyewe aamue, lakini lisingekuwa jambo la Kikristo kula kiapo cha uongo cha aina yo yote, hata ikiwa mtu atakatazwa kuwa raia kwa sababu ya kukataa kufanya hivyo.​—⁠Efe. 4:25; linganisha Hosea 10:1, 4.

Raia wa United States ya Amerika anayetaka kusafiri ng’ambo ataona kiapo kifuatacho kimeandikwa katika ombi la passport: “Naapa kwa uzito (au nathibitisha bila kiapo) kwamba nitaunga mkono na kutetea Katiba ya United States isishambuliwe na maadui wote, wa kigeni na wa ndani; kwamba nitakuwa na imani na utii wa uaminifu kwayo; na kwamba nakubali wajibu huu kwa hiari, bila masharti akilini, wala kusudi la kuepa: Kwa hiyo nisaidie Mungu.” Mwombaji akiona hawezi kukubali kiapo hicho, anaruhusiwa kukifuta katika ombi la passport, naye hatakatazwa kupata hati hiyo.

Kwa kufaa mtu mwenye kumcha Mungu hufikiria mambo pia kulingana na maneno ya Yesu Kristo: “Vya Kaisari mpeni Kaisari, na vya Mungu mpeni Mungu.” (Luka 20:25) Ikiwa kitu cho chote kinapingana na sheria ya Mungu, Mkristo hawezi kukiapia kulingana na dhamiri. Hata hivyo anaweza kula kiapo cha ‘kuunga mkono na kutetea’ mipango ya sheria ya nchi isiyopingana na sheria ya Mungu. Mataifa yenye ujuzi yanayowapa raia uhuru wa ibada hayawekei Wakristo takwa la kufanya mambo tofauti na imani zao za Biblia na wajibu wao kwa Mungu Mwenye Nguvu Zote.

Lakini ni kwa njia gani Mkristo aweza ‘kuunga mkono na kutetea’ sheria au Katiba ya nchi yenye kutoa uhuru wa kidini? Ni kwa kuwa tu na mwenendo unaofaa na wenye kupatana na sheria ya nchi, hata ile ya Mungu. Anaweza kufanya hivyo kwa kinywa pia, hata kutoa ushuhuda wa kweli kortini (barazani). Hakuna mtu anayeweza kupinga kwa akili nzuri Mkristo asiape kufanya jambo ambalo Mungu amtazamia alifanye, tena wafuasi wa Kristo wanatakiwa wawe na utii wa kadiri kwa wakuu wa serikali.​—⁠Rum. 13:1.

Bila shaka kuna viapo vingi sana. Kwa mfano, vyama (unions) vingine hutaka wanachama waape hivi: “Mimi nitakuwa na utii wa kweli kwacho wala sitaharibu mapendezi yacho kwa njia yo yote.” Hii inamaanisha kwamba mwanachama hatajaribu kukomesha mgomo wa wafanya kazi wala mambo mengine kama hilo yanayochukuliwa kuwa yenye kuharibu chama. Mtu mwenye kumcha Mungu akiamua asingekuwa akipingana na utendaji wake wa Kikristo kwa kukubali kiapo hicho, aweza kukila.

Kwa hiyo, wakati kiapo cho chote kinapofikiriwa dhamiri ya mtu inahusika. Bila shaka, mtu aliyejitoa kwa Yehova atakumbuka kanuni za Biblia. Hata iweje, hilo ni jambo la lazima ili mtu aendelee kuwa na uhusiano wa karibu na Mungu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki