Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 7/8 kur. 5-8
  • Je! Kweli Nyota Hudhibiti Maisha Yako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Kweli Nyota Hudhibiti Maisha Yako?
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Chanzo
  • Nguvu Yenye Kuendesha Unajimu
  • Je, Unajimu Unaweza Kukufunulia Wakati Ujao?
    Amkeni!—2005
  • Je, Maisha Yako Yanaongozwa na Nyota?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Nyota Zina Habari Gani Kwako?
    Amkeni!—1994
  • Nyota na Mwanadamu—Je! Kuna Uhusiano?
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 7/8 kur. 5-8

Je! Kweli Nyota Hudhibiti Maisha Yako?

“WATU wengi wataka kujua ule upuuzi wa kawaida—nitapata lini dola milioni moja au nitakutana lini na huyu Bwana Mashuhuri?” asema mnajimu wa nusu-wakati. Kwa kweli, watu walio wengi huchukua unajimu kuwa njia ya kujifunza jambo fulani juu ya wakati ujao. Na wanajimu wengi wana hamu nyingi ya kufadhili watu hao kwa kuhudumia matakwa yao—bila shaka kwa malipo.

Hata hivyo, wanajimu ambao hujifikiria kuwa wa kimamboleo hupuuza oni hilo. “Mimi si mtu wa jinsi hiyo,” aendelea kusema yule mfanya kazi wa nusu-wakati. “Kazi yangu ni kujaribu kusaidia watu wajielewe.” Basi, unajimu ni wa kusaidia watu wajielewe wenyewe kwa njia gani?

Kila mtu ajua kwamba utendaji mbalimbali wa kibinadamu huathiriwa na jua, mwezi, na nyota. Jua huamua majira na utaratibu wa ukuzi. Mwezi ndiyo kani kuu yenye kuongoza mawimbi-bahari. Kwa muda mrefu nyota zimetumiwa kuwa miongozo katika ubaharia. Je! kuna sababu nzuri ya kuwaza kwamba magimba haya ya kimbingu huathiri sana utendaji mwingine pia katika maisha zetu?

Unajimu wajibu ndiyo. Imani ya msingi ya unajimu ni kwamba mahali ambapo jua, mwezi, na sayari huwa miongoni mwa konstelesheni (makundi-makundi ya nyota) za kifumbo wakati za kuzaliwa kwetu huathiri sana tabia yetu na maisha yetu. Hivyo, akijua wakati na mahali pa kuzaliwa kwa mtu, mnajimu aweza kujenga chati, au falaki, akionyesha mahali zilipo nyota na sayari na kufasiri mambo ambayo huenda yakaathiri vitendo vya mtu huyo wakati fulani hususa. Msingi wa dai hilo ni nini? Lina uthabiti wa kadiri gani?

Kwa kujaribia, mwanasaikolojia Mfaransa Michel Gauquelin alimpelekea mnajimu tarehe na mahali pa kuzaliwa pa mwuaji aliyenyongwa ili afanye uchanganuzi. Halafu akapeleka matokeo kwa watu 150 waliokuwa wameitikia tangazo lake lenye toleo la kufanyia watu uchanganuzi wa bure wa falaki. Tokeo likawa nini? Alipata kwamba asilimia 90 ya watu hao walisema kwamba uchanganuzi waliopokea ulikuwa elezo sahihi juu ya utu wao na asilimia 80 wakasema kwamba hata rafiki na jamaa zao waliafikiana na jambo hilo.

Hebu sasa na tuache hilo tuzungumzie kusababu mambo kiakili! Ukweli ni kwamba kwa kawaida mabashiri ya kinajimu huelezwa kwa usemi usioeleweka vizuri—tena asili ya kibinadamu imetatanika sana—hivi kwamba ikiwa mtu anatafuta sana jambo lenye kufaa, sikuzote ataweza kulipata, bila kujali ubashiri ule umetegemezwa juu ya nini.

Chanzo

Yote haya yatuleta kwenye suala lililo la msingi hasa: Kwa kuchukua kwamba nyota hushiriki sehemu fulani katika kuathiri maisha yetu, athari hiyo huletwaje juu yetu? Kati ya kani zote zijulikanazo na sayansi, ni ipi au ni zipi zenye kuhusika? Kwa sababu nyota na sayari ziko mbali sana, mwanasayansi mmoja alionelea kwamba “kwa habari ya tokeo lenye kupata mtoto ambaye ndipo tu amezaliwa, ile nguvu ya uvutano wenye kutoka kwa tabibu anayehudumia, ule mnurisho wa sumaku-umeme wa taa zilizo chumbani ni wa kadiri kubwa kuliko wa sayari yoyote.” Ikiwa nyota hazituathiri kwa kani za uvutano, za sumaku-umeme, au nyingine zozote zinazojulikana na sayansi, basi ni nini chanzo cha athari hiyo?

Swali hilo lenye kuamsha upendezi laulizwa na profesa mmoja wa elimu ya nyota, George Abell, katika kitabu Science and the Paranormal. Baada ya kuchunguza madai yote yenye kufanywa na wanajimu kuhusu nguvu ya nyota na sayari, Abell aandika hivi:

“Kama sayari zingetokeza athari fulani juu yetu, ingepasa kuwa hivyo kupitia kani fulani isiyojulikana na yenye hali za kiajabu sana: ingepasa kutokana na magimba fulani ya kimbingu wala si yote, ingepasa kuathiri vitu fulani duniani wala si vyote, na imara yayo haingeweza kutegemea umbali, utungamo, au hali nyingine za sayari hizo zenye kuitokeza. Yaani, ingekuwa bila matokeo yenye kuhusu ulimwengu wote mzima, bila utaratibu, na upatano upatikanao kwa kila kani nyingine na sheria ya asili iliyopata kugunduliwa ambayo hutumika katika ulimwengu wote mzima ulio halisi.”

Sayansi haijui habari zozote kuhusu kani hiyo. Ikiwa kweli unajimu hufanya kazi kwa matokeo, lazima uwe unafanya kazi kwa kani moja, au nyingi, zilizo nje ya “ulimwengu wote mzima ulio halisi.” Lakini kwa kukumbuka kwamba mizizi ya unajimu imo katika Babuloni ya kale, ambako nyota na sayari ziliabudiwa kuwa miungu, haipasi kushangaza kwamba chanzo cha athari yayo hakitokani na “ulimwengu wote mzima ulio halisi” bali kutokana na nguvu za kadiri kubwa kuliko zile za kibinadamu.

Nguvu Yenye Kuendesha Unajimu

Biblia huonyesha kwamba “ulimwengu wote mzima unalala katika uwezo wa yule mwovu,” Shetani Ibilisi, aliye kiumbe-roho asiyeonekana lakini mwenye nguvu nyingi awezaye kudhibiti na kuelekeza watu na matukio duniani kama atakavyo. (1 Yohana 5:19, NW) Kwa kuongoza mambo kwa werevu ili kufanya matabiri fulani yaonekane kuwa yanatimia, Shetani na roho waovu wamefanikiwa kuteka upendezo wa watu na wakageuza unajimu kuwa kiibada.

Ingawa hivyo, jambo lenye umaana ni kwamba hayo yenye kudhaniwa kuwa yametimia ni matabiri ya namna gani? Je! sana-sana hayahusiani na kifo, visa vya kuua kimakusudi, kuua watawala, misiba—mambo ya misiba na maogofyo ya kifo, yenye sifa za kishetani na ya roho waovu hasa? Ukweli ni kwamba unajimu ni moja ya “mbinu mbaya za Ibilisi” ambazo yeye hutumia kudhibiti na kuathiri watu watumikie kusudi lake.—Waefeso 6:11, HNWW.

Ni nini kusudi hilo? “Mungu wa ulimwengu huu amepofusha akili za wasioamini, kuwaweka bila kuona nuru ya gospeli ya utukufu wa Kristo,” yajibu Biblia. (2 Wakorintho 4:4, Revised Standard Version) Kwa lengo hilo, unajimu umemtumikia vizuri bwana-mkubwa wao. Mwanafizikia wa elimu ya nyota Vince Ford aliye Mwaustralia alionelea hivi: “Unajimu umekuwa namna ya dini lakini haiwezi kuthibitishwa kabisa . . . Niwezalo tu kusema ni kwamba nasikitika kwamba wale wenye kuiamini hawakubali lawama kwa vitendo vyao badala ya kusingizia zile nyota za zamani zisizo na hatia.”

Katika karne ya nne K.W.K., nabii Isaya alivuviwa kutoa wito wa ushindani wenye kuwadhihaki wanajimu: “Na wasimame hao wajuao falaki, wazitazamao nyota, watabirio kila mwezi mambo ya mwezi huo, wakakuokoe na mambo yatakayokupata.”—Isaya 47:13.

Mwenye kuamini unajimu hujiacha aongozwe na maoni ya kutegemea ajali kwamba ‘lolote liwalo litakuwa’ kwa sababu ‘limeandikwa katika nyota.’ Hiyo ni sawa na kukana mapenzi ya Mungu au daraka la wanadamu kutenda kulingana na mapenzi hayo.

Kwa hiyo badala ya kutegemea nyota kwa ishara na dalili za kuongoza maisha zetu, twaweza kujifunza nini kutokana na nyota? Ndiyo, nyota zaweza kutuambia nini? Makala ifuatayo yatoa jibu.

[Sanduku katika ukurasa wa 6]

Je! Unajimu Hupatana na Sayansi?

Magunduo ya kisayansi katika nyakati za hivi majuzi yametokeza madai yenye kutatiza sana unajimu. Fikiria mambo haya ya uhakika:

◼ Yajulikana sasa kwamba nyota ambazo huonekana kuwa katika konstelesheni (kundi) moja kwa kweli huwa hazimo katika kikundi kimoja. Baadhi yazo zimo ndani sana ya anga, nyingine zipo karibu kwa kulinganishwa. Hivyo, habari za zodiaki (ukanda wa nyota za ubashiri) kuhusu konstelesheni mbalimbali za nyota huwa za kuwazia tu.

◼ Sayari Uranus, Neptune, na Pluto hazikujulikana na wanajimu wa mapema, kwa maana hazikugunduliwa mpaka darubini ya kuona mbali ilipovumbuliwa. Basi, “athari” zayo ziliwezaje kuelezwa katika chati za kinajimu zilizochorwa karne kadhaa mapema?

◼ Sayansi ya urithi hutuambia kwamba vitabia vyetu vya utu hufanyika, si wakati wa kuzaliwa, bali wakati wa kuchukuliwa mimba, wakati ambapo moja ya mamilioni ya chembe za shahawa ya uzazi kutoka kwa baba huungana na chembe ya yai la kutoka kwa mama. Hata hivyo, unajimu hukaza kikiki falaki ya mtu kulingana na wakati wa kuzaliwa, miezi tisa baadaye.

◼ Sehemu ya anga ambayo jua, mwezi, na sayari huonekana zikiipitia, ambayo huitwa zodiaki, imegawanywa na wanajimu ikawa visehemu 12 vinavyolingana sawasawa, ishara ya kila kimoja ikiwa ni konstelesheni (kundi la nyota) moja. Kwa uhalisi, kuna konstelesheni 14 katika sehemu hiyo ya anga. Ukubwa wazo si sawasawa nazo hupishana kwa kadiri fulani. Kwa hiyo michoro ambayo huchorwa na wanajimu haina ufanano wowote na jinsi mambo yalivyo angani.

◼ Wakati ambao jua huchukua kusafiri miongoni mwa konstelesheni, kama uonwavyo na mtazamaji aliye duniani, leo ni mwezi mmoja hivi nyuma ya vile ulivyokuwa miaka 2,000 iliyopita wakati chati na jedwali za wanajimu zilipochorwa. Hivyo, unajimu ungembashiri mtu aliyezaliwa mwishoni-mwishoni mwa Juni au mapema Julai ya mwaka juzi kuwa yu katika Kansa—mwenye kugusika hisia upesi sana, mtu wa furaha mara hii na hasira mara hii, mwenye kujitenga na watu—kwa sababu kulingana na chati hizo Jua limo katika konstelesheni ya Kansa. Hata hivyo, kwa kweli Jua limo katika konstelesheni ya Gemini, na hiyo yadhaniwa kuwa ingefanya mtu huyo awe “mwenye kuwasiliana na watu, mwenye akili nyepesi kuelewa mambo, mwenye kuongea sana.”

[Sanduku katika ukurasa wa 7]

Unajimu wa Mashariki na wa Magharibi

Unajimu kama uzoewavyo katika Magharibi huihesabia vitabia maalumu kila moja ya konstelesheni 12 ambazo jua huonekana kama likisafiri kuzipitia mwakani. Vikundi hivi vya nyota vilipewa majina na Wagiriki, ambao waliviwazia kuwa viumbe, kama vile Aries Kondoo Dume, Taurus Fahali, na Gemini Mapacha.

Kwa kupendeza, unajimu katika China na Japani ya kale pia hugawanya zodiaki katika majimbo 12 yenye kulingana na wanyama 12 wa yale yaitwayo matawi ya kidunia—mbwa, kuku, tumbili (nyani), mbuzi, farasi, na kadhalika. Na kila mmoja wa wanyama hawa husemwa kuwa hutokeza athari yake kulingana na tabia aliyo nayo kwa kipindi fulani. Hivyo, visehemu vyenye kulingana vya mbingu hupangwa na unajimu wa Mashariki na wa Magharibi kwa njia ifuatayo:

Zodiaki ya Magharibi Zodiaki ya Mashariki

Aries Kondoo Dume Mbwa

Taurus Fahali Kuku

Gemini Mapacha Tumbili(Nyani)

Kansa Kaa Mbuzi

Leo Simba Farasi

Virgo Bikira Nyoka

Libra Mizani Drakoni(Joka)

Scorpio Nge Sungura

Sagittarius Mpinda-upinde Simba-milia

Capricorn Mbuzi Fahali

Aquarius Mchukua-Maji Panya

Pisces Samaki Nguruwe

Twaona nini tulinganishapo mifumo miwili hii? Ajabu ni kwamba konstelesheni hizo zaonekana kufanya kazi kwa njia zenye kutofautiana sana Mashariki na Magharibi. Hivyo, kwa kielelezo, unajimu wa Magharibi hutabiri kwamba mtu aliyezaliwa jua likiwa katika Aries ni mwenye kushikilia sana kauli yake, katika Taurus ni mwenye kichwa kigumu, na kadhalika. Lakini hizi ni sifa ambazo ni vigumu mtu kuzishirikisha na mbwa na kuku. Hata hivyo, ndivyo unajimu wa Mashariki ungetabiri. Yaweza kusemwa ivyo hivyo juu ya mambo yale mengine mawili-mawili. Hivyo, kwa kutegemea mfumo ambao wewe wachagua, nyota zile zile husemwa kuwa zina tabia tofauti kabisa na hudhaniwa kutokeza athari zilizo tofauti. Je! ni nyota au ni uwazio wa wanajimu ambao hudhibiti watu?

[Picha katika ukurasa wa 8]

Falaki iliyo ya zamani zaidi ulimwenguni, labda ya Aprili 29, 410 K.W.K. Ilifanyizwa katika Babuloni

[Hisani]

Kwa hisani ya Wageni Wenye Kuzuru Ashmolean Museum, Oxford

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki