Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 7/8 uku. 3
  • Nyota Zina Habari Gani Kwako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nyota Zina Habari Gani Kwako?
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Unajimu Unaweza Kukufunulia Wakati Ujao?
    Amkeni!—2005
  • Je! Kweli Nyota Hudhibiti Maisha Yako?
    Amkeni!—1990
  • Nyota na Mwanadamu—Je! Kuna Uhusiano?
    Amkeni!—1994
  • Je, Maisha Yako Yanaongozwa na Nyota?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 7/8 uku. 3

Nyota Zina Habari Gani Kwako?

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA BRAZILI

“JE! UMESIKIA kwamba nyota zaonyesha kuwa Julai unaokuja dunia yetu itagongana na Mihiri?” Maneno haya ya wimbo wenye mwendo mchangamfu wa Cole Porter yaeleza vema juu ya ile imani ya kawaida na ya kale kwamba wakati ujao wa mwanadamu wahusiana na nyota kwa njia fulani.a Lakini je, kuna uhusiano wowote wa kweli kati ya magimba ya kimbingu na maisha ya wanadamu katika dunia hii? Ikiwa ndivyo, wanadamu huathiriwaje? Ikiwa sivyo, nyota hutimiza kusudi gani hasa?

Haishangazi kwamba watu wengi sana hupendezwa na wakati ujao tufikiriapo matukio fulani ya kutazamisha ya hivi majuzi—anguko la Ukuta wa Berlin na kuvunjika upesi sana kwa Muungano wa Sovieti, kukosa kuwatumaini viongozi wa kisiasa, chuki ya kikabila inayotokea katika Afrika na Ulaya, uadui wa kidini katika India na Ireland, infleshoni inayoongezeka haraka sana ikisumbua nchi nyingi sana, na uasi wa vijana. Kulingana na ripoti moja kutoka Chuo Kikuu cha Hamburg, 1992 ulikuwa ndio mwaka wa ugomvi zaidi tangu mwisho wa Vita ya Ulimwengu 2, ukiwa na mapigano 52 ya kutumia silaha katika nchi tofauti-tofauti. Basi ni kawaida kwamba watu wapenda-amani wauliza hivi: ‘Ni wapi tuwezapo kupata uthabiti, amani, na usalama?’

Kukosa uhakika juu ya wakati ujao kumetokeza vuvumko la matabiri ya namna mbalimbali. Unajimu labda ndiyo namna ijulikanayo zaidi. Unajimu, ambao ni tofauti na astronomia ni “kufanya uaguzi juu ya athari ambazo nyota na sayari hudhaniwa kuwa nazo juu ya mambo ya kibinadamu na juu ya matukio ya nje ya eneo la ulimwengu kwa kutegemea mahali zilipo na mikao yazo kuhusiana na jua.” Leo, mamilioni ya watu hushindwa kujizuia kusoma falaki ili kupata madokezo juu ya wakati wao ujao.b

Maeneo mengine ambamo wanajimu hudai kutabiri wakati ujao ni kutia ndani matokeo ya magumu ya ndoa na matatizo ya afya, kuinuka na kuanguka kwa viongozi wa kisiasa, tarehe nzuri kabisa ya kufungua biashara mpya, na tarakimu za kutumia ili kushinda mchezo wa bahati-nasibu.

Ripoti moja ya shirika la habari za Reuters ilisema kwamba mnajimu Joan Quigley alifikiwa kwa ukawaida na Nancy Reagan ili kumpa ushauri juu ya wakati ambapo mume wake, ambaye wakati huo alikuwa rais wa Marekani, apaswa kutoa hotuba zake na wakati ambapo ndege yake yapaswa kuruka na kutua chini. New Catholic Encyclopedia ilifunua kwamba “unajimu ulitumiwa na Papa Julius 2 [1503-13] kupanga siku ya kutawazwa kwake na ukatumiwa na Paul 3 [1534-49] kuamua saa barabara ya kufanya Baraza la Kuzungumzia Masuala Mazito.” Alfred Hug, mkurugenzi wa shirika moja la Kiswisi ambalo hutumia unajimu kushauri waweka-akiba juu ya soko la hisa, huwatolea uthibitisho kamili wa kupata matokeo mazuri kabisa. “Hayo yameandikwa katika nyota,” yeye hushikilia.

Kwa wazi, watu wengi huhisi kwamba nyota huathiri maisha za wanadamu. Unajimu ulianzaje? Je! kile kitabu cha kale Biblia kina lolote la kusema juu ya unajimu na wanajimu?

[Maelezo ya Chini]

a “Katika China ya kale, . . . ishara za angani na vilevile misiba ya kiasili zilifikiriwa kuwa zilionyesha matendo hodari na matendo mabaya ya Maliki na serikali yake.”—The International Encyclopedia of Astronomy.

b Falaki ni “mchoro wa mikao ya uwiano wa sayari na ishara za zodiaki wakati fulani hususa (kama wakati wa kuzaliwa kwa mtu)” nayo hutumiwa na wanajimu kujaribu kutabiri matukio ya wakati ujao katika maisha ya mtu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki