Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 7/8 kur. 4-7
  • Nyota na Mwanadamu—Je! Kuna Uhusiano?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nyota na Mwanadamu—Je! Kuna Uhusiano?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Chaguo Kubwa Sana la Nyota
  • Nyota Katika Maandiko
  • “Ile Nyota” ya Bethlehemu
  • Je, Maisha Yako Yanaongozwa na Nyota?
    Amkeni!—2012
  • Nyota kwa Kweli Zina Ujumbe Fulani Kwako!
    Amkeni!—1994
  • Je! Kweli Nyota Hudhibiti Maisha Yako?
    Amkeni!—1990
  • Hobi Yangu Ni Astronomia
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 7/8 kur. 4-7

Nyota na Mwanadamu—Je! Kuna Uhusiano?

ZOEA la kuzitazama nyota si jipya. Kulingana na The World Book Encyclopedia, maelfu ya miaka iliyopita wakulima “walizitazama nyota kujua wakati wa kupanda mimea yao. Wasafiri walijifunza kutumia nyota ili kuelewa pande za kuelekea.” Hata leo katika usafiri wa angani, nyota bado hutumiwa kuwa miongozo. Wakale walivumbua pia ngano juu ya watu na wanyama ambao walihisi walionekana katika vikundi vya nyota, au konstelesheni. Baada ya muda watu walikuja kuhisi kwamba nyota zingeweza kuathiri maisha zao.

Chaguo Kubwa Sana la Nyota

Hesabu yenyewe tu na ukubwa wa nyota hustaajabisha sana. Yakadiriwa kwamba kuna galaksi, au makundi makubwa sana ya nyota, zipatazo bilioni 100 katika ulimwengu wote mzima! The International Encyclopedia of Astronomy husema hivi: “Hiyo ndiyo hesabu ya punje za mchele ambazo zingeweza kuingizwa katika kathedro [kanisa] ya wastani.” Galaksi ya Njia ya Maziwa, ambayo mfumo wetu wa jua ni sehemu yayo, yakadiriwa kuwa na angalau nyota nyingi hivyo. Nyota iliyo karibu zaidi na Dunia yetu (bila kuhesabu Jua), iliyo ya kikundi cha Alpha Centauri, iko umbali wa karibu miaka-nuru 4.3. Mwaka-nuru ni umbali ambao nuru husafiri kwa mwaka mmoja. Hiyo yamaanisha kwamba tutazamapo nyota hiyo, nuru inayoingia katika jicho letu ilitoka kwenye nyota hiyo miaka 4.3 iliyopita na muda wote huo ikawa ikisafiri kupita angani kwa mwendo wa kilometa 299,792 kwa sekunde moja. Kuwazia umbali ambao wahusika kwapita uwezo wetu wa akili. Hata hivyo, hiyo ni nyota ile iliyo karibu zaidi tu. Nyota fulani ziko mabilioni ya miaka-nuru kutoka kwenye galaksi yetu. Si ajabu nabii wa Mungu alitangaza hivi: “Tazama, mataifa ni kama tone la maji katika ndoo, huhesabiwa kuwa kama mavumbi membamba katika mizani; tazama, yeye huvinyanyua visima kama ni kitu kidogo sana.” (Isaya 40:15) Nani huhangaishwa na kavumbi katiti?

Gimba la kimbingu lililo karibu zaidi na dunia ni mwezi, ambao huwa na athari ya wazi juu ya dunia yetu, hata uvutano wao ukisababisha tofauti ya zaidi ya meta 15 kati ya miinuko na mishuko ya bahari mahali fulani-fulani. Kulingana na wanasayansi watatu Wafaransa, uvutano wa mwezi sasa waaminiwa kuwa ndio huweka mwinamo wa dunia katika mlalo wa digrii 23, na hivyo kuhakikisha kuna badiliko la kawaida la majira. (Nature, Februari 18, 1993) Kwa kuwa mwezi una athari nyingi hivyo ya kihalisi juu ya sayari yetu, kuna sababu nzuri ya kuuliza hivi, Namna gani yale mabilioni ya nyota? Lakini kwanza, vyanzo vya kale, kama Biblia, vyatuambia nini juu ya nyota?

Nyota Katika Maandiko

Biblia hurejezea nyota mara nyingi, katika maana halisi na ya kitamathali pia. Kwa kielelezo, kulingana na mtunga-zaburi mmoja, Muumba alifanya “mwezi na nyota ziutawale usiku” ili nyota zisaidie kuiandalia dunia nuru. (Zaburi 136:9, Tanakh) Baadaye, Mungu alipokuwa akifanya agano pamoja na Abrahamu mwaminifu, alisema: “Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.” (Mwanzo 15:5) Mtume Paulo aonyesha kwamba nyota ni tofauti-tofauti, akisema: “Kuna fahari moja ya jua, na fahari nyingine ya mwezi, na fahari nyingine ya nyota; maana iko tofauti ya fahari hata kati ya nyota na nyota.”a (1 Wakorintho 15:41) Wakati uleule, hesabu hii kubwa sana ya nyota na utukufu wazo hairuki mipaka ya milki au udhibiti wa Muumba wazo: “Huihesabu idadi ya nyota, huzipa zote majina.”—Zaburi 147:4.

Kwa upande mwingine, katika Maandiko twapata kwamba mara nyingi nyota hutumiwa kurejezea watu, watawala, na malaika. Yusufu mwana wa Yakobo apata ndoto ambamo wazazi wake wafananishwa na “jua na mwezi” na ndugu zake na “nyota.” Malaika warejezewa kuwa “nyota za asubuhi.” Mfalme wa Babiloni asemwa ana lengo la kuwa juu ya “nyota za Mungu,” wale watawala wa Kidaudi wa taifa la Israeli. Wanaume wasio imara katika kutaniko la Kikristo wafananishwa na “nyota zisizo na kipito kamili,” hali mabaraza ya wazee waaminifu wa kutaniko yatajwa kuwa “nyota” zilizo katika mkono wa kulia wa Kristo.—Mwanzo 37:9, 10; Ayubu 38:7; Isaya 14:13; Yuda 13; Ufunuo 1:16; linganisha New World Translation.

Usimulizi mmoja katika Biblia wasema kwamba “nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera,” mkuu wa jeshi la Mfalme Yabini wa Kanaani, aliyekuwa amelemea taifa la Israeli kwa miaka 20. Yehova alimpa Mwamuzi Baraka wa Israeli mgawo wa kuokoa Israeli utumwani na kumpa ushindi mkubwa ajabu juu ya Sisera, hata ingawa Sisera alikuwa na magari mia tisa yenye miundu ya chuma katika magurudumu yayo. Katika wimbo wa ushindi, Waisraeli waliimba hivi: “Walipigana kutoka mbinguni, nyota katika miendo yao zilipigana na Sisera.” Hakuna elezo litolewalo juu ya jinsi hasa nyota zilivyopigana. Badala ya kuchukulia kwamba nyota zilikuwa na uvutano wa moja-kwa-moja katika pigano, yafaa zaidi kuamini kwamba usemi huo waonyesha namna fulani ya mwingilio wa kimungu kwa ajili ya Israeli.—Waamuzi 5:20.

“Ile Nyota” ya Bethlehemu

Labda mojapo nyota zijulikanazo zaidi katika Biblia ni “ile nyota” ya Bethlehemu iliyowaongoza wanajimu kutoka “sehemu za mashariki” hadi ile nyumba ambamo Yesu alikuwa amepelekwa na wazazi wake baada ya yeye kuzaliwa katika banda la mifugo. Nyota hiyo ilikuwa nini? Hakika haikuwa ya kawaida, kwa kuwa ilikuwa chini kadiri ya kutosha wanajimu kuifuata kwa karibu kilometa 1,600. “Ile nyota” iliwaongoza hadi Yerusalemu kwanza. Kusikia hilo, Mfalme Herode aliwahoji kisha akaamua kuua kitoto kichanga Yesu. Halafu “ile nyota” ikawaongoza wanajimu katika nyumba hususa ambamo Yesu alikuwa akiishi. Hakika hakuna nyota yoyote ya kawaida ingeweza kufanya hivyo. Je! kitu hiki kilicho kama nyota kilitokana na Mungu? Kwa kuwa ziara ya wanajimu ilitokeza kwa njia isiyo ya moja kwa moja machinjo ya “watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua,” je, hakuna sababu nzuri kukata shauri kwamba “ile nyota” ilikuwa kitu fulani kilichotumiwa na Mpinzani wa Mungu, Shetani, katika jaribio la kuangamiza Mwana wa Mungu?—Mathayo 2:1-11, 16.

Yapasa pia kukumbukwa kwamba wanajimu hao walitoka Mashariki, labda kutoka Babiloni, ambayo ilikuwa kitovu cha kale cha miungu, ulozi, na unajimu. Magimba kadhaa ya kimbingu yamepewa majina ya miungu ya Babiloni. Katika siku za Mfalme Nebukadreza, uaguzi ulitumiwa kumsaidia kuamua apite njia ipi katika kampeni yake ya pigano.—Ezekieli 21:20-22.

Nabii Isaya aliwatolea wito wa ushindani washauri wa Babiloni, akisema: “Wewe [Babiloni] huna nguvu ujapokuwa ushauri uupatao. Acha wanajimu wako waje mbele na kukuokoa—watu wale wajifunzao nyota, wapangiliao ramani ya kanda za mbingu na kukuambia mwezi hadi mwezi ni nini litakalokupata wewe. Wao watakuwa kama vipande vya manyasi makavu, na moto utawateketeza! Hawataweza hata kujiokoa wenyewe . . . na hakuna wowote watakaobaki kukuokoa.” Kulingana na unabii wa Isaya, Babiloni yenye uweza ilianguka kwa Sairasi Mkuu katika 539 K.W.K. Ule mwongozo ambao wanajimu hao Wababiloni walidai kuleta kutokana na nyota uligeuka kuwa msiba kwa wahusika wote.—Isaya 47:13-15, Today’s English Version.

Je! hii yamaanisha kwamba hatuwezi kujifunza lolote kutokana na nyota?

[Maelezo ya Chini]

a Astronomia ya ki-siku-hizi yathibitisha maneno ya Paulo, kwa kuwa nyota hutofautiana kwa rangi, ukubwa, kiasi cha nuru itokezwayo, halijoto, na utungamano wazo kuhusiana na nyinginezo.

[Sanduku katika ukurasa wa 5]

Yale Ambayo Watu Fulani Wamesema

UNAJIMU: “kiongezeo na kishiriki cha astronomia.”—Johannes Kepler (1571-1630) mwastronomia Mjerumani.

“Unajimu ni ugonjwa, si sayansi. . . . Ni mti ambao chini ya kivuli chao namna zote za ushirikina husitawi.”—Moses Maimonides (1135-1204), mwanachuo Myahudi wa Enzi za Kati.

“Sayansi ya kizamani ambayo hudai kuweza kukadiria utu na mwenendo wa mtu na kutabiri mielekeo na matukio ya wakati ujao kutokana na mikao ya magimba ya kimbingu. . . . Labda karibu na karne ya 6 KK—Wakaldayo katika kusini mwa Iraki hufikiriwa kuwa ndio walioanzisha falaki ya kibinafsi. Hiyo ilihusiana na athari zilizotokezwa wakati wa kuzaliwa na nyota zilizokazika mahali pamoja, na pia Jua, Mwezi na sayari tano. . . . Taratibu za unajimu na ufasiri wa falaki hutegemea mawazo ambayo waastronomia na walio wengi wa wanasayansi wengine huyaona kuwa ya watu binafsi na yasiyokubalika.”—C. A. Ronan, aliye mratibu wa mradi, Historia ya Amana ya Sayansi ya Asia Mashariki, Cambridge, Uingereza, na mchangiaji wa habari za kichapo The International Encyclopedia of Astronomy ambapo nukuu hili limetolewa.[2]

Kwa kutoa kielezi cha hali hii ya kushikilia maoni ya kibinafsi, Ronan aeleza kwamba ingawa akili za watu wa Magharibi huchukua kwamba ile sayari nyekundu, Mihiri, yahusiana na vita na hali ya kutaka ugomvi, kwa Wachina, wekundu ni rangi ya kuvutia, na Mihiri huonwa kuwa na uvutano mwema. Tofauti na hivyo, ngano za Magharibi hushirikisha Zuhura na weupe na uzuri. Kwa Wachina “weupe . . . huonwa kuwa rangi ya kifo, uozi na uangamivu; kwa hiyo Zuhura ilirejezewa kuwa ile ‘sayari ya ugizagiza wa vita.’”

Ronan aendelea kusema: “Ijapokuwa unajimu una asili ya sayansi ya kizamani, katika nyakati za mapema ulishiriki sehemu yenye mafaa katika kuendeleza astronomia na kuandaa fedha za kuutekeleza.”

Washindi 19 wa tuzo ya Nobel, pamoja na wanasayansi wengine, walitoa tangazo rasmi katika 1975 lenye kichwa “Vikanusha Unajimu—Taarifa ya Wanasayansi Mashuhuri 192.” Lilitangaza hivi:

“Katika nyakati za kale watu . . . hawakuwa na wazo lolote juu ya umbali mkubwa sana uliopo kutoka duniani hadi kwenye zile sayari na nyota. Kwa kuwa sasa umbali huo waweza kuhesabiwa na umehesabiwa, twaweza kuona jinsi zilivyo ndogo sana nguvu za uvutano na matokeo mengine yatokezwayo na hizo sayari za mbali na nyota zilizo mbali hata zaidi. Ni kosa kabisa kuwazia kwamba athari za nyota na sayari wakati wa kuzaliwa zaweza kwa njia yoyote kuamua kimbele jinsi nyakati zetu zijazo zitakavyokuwa.”[5]b

[Maelezo ya Chini]

b Kwa habari zaidi juu ya unajimu, ona Amkeni! Aprili 8, 1987, kurasa 3-9.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki