Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 11/8 kur. 16-17
  • Kupitia Macho ya Mtoto

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kupitia Macho ya Mtoto
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Wao Si Watu Wazima Wadogo
  • Tia Moyo na Kuongoza Badala ya Kudai
  • Kulea Watoto tangu Uchanga
    Kufanya Maisha ya Jamaa Yako Yawe Yenye Furaha
  • Wazazi, Fikieni Moyo wa Mtoto Wenu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1982
  • Zoeza Mtoto Wako Tangu Utoto Mchanga Sana
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Jinsi ya Kuwalinda Watoto Wako
    Amkeni!—2007
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 11/8 kur. 16-17

Kupitia Macho ya Mtoto

WAZAZI walio wengi wataafikiana juu ya angalau jambo moja: kulea mtoto kwa mafanikio ni moja la matatizo yaliyo makubwa kabisa ambayo wamepata kukabili. Maneno yasiyohesabika yameandikwa juu ya jinsi ya kufanya hivyo na kufanikiwa. Hata hivyo, kuna njia moja ambayo watu wazima wote waweza kuitumia, wawe ni wazazi, akina babu na nyanya, mashangazi, wajomba, au marafiki tu. Liwapo ni jambo la kuwaelewa na kuwazoeza watoto, je! wewe umejaribu kutazama mambo kupitia macho ya mtoto? Ni nini hasa huendelea katika hizo akili ndogo?

Kumbuka, watoto ni watu wadogo. Kuwa na maoni haya kwa habari yao kutatusaidia kuelewa jinsi sisi huonwa na wao. Wao huzaliwa wakiwa wadogo mno katika ulimwengu wa watu walio mibabe katika ukubwa, mamlaka, na uwezo. Kwa mdema, watu wazima waweza ama kuwakilisha ulinzi, faraja, na msaada au tisho la kutumia mabavu.

Wao Si Watu Wazima Wadogo

Jambo jingine la muono-ndani ni kuwa waangalifu kutofanya kosa la kuwatendea kama watu wazima wadogo. Utoto wapasa kuwa mmoja wa nyakati zenye furaha kabisa maishani. Hakuna uhitaji wa kuwafanya waupitie haraka-haraka wala kusababisha waukose kabisa. Acha waufurahie. Wewe uliye mzazi, waweza kuchukua fursa ya kujenga ndani yao kanuni za kiadili zihitajiwazo ili, baada ya muda, wawe watu wazima waliorekebika vizuri.

Wakati wa kushughulika na vitoto vichanga, kuona mambo kupitia macho ya mtoto hakupotezi thamani. Kwa kielelezo, kulia hakupasi kamwe kuwa mwaliko wa kuchapwa-chapwa na wazazi waliotafurika (waliotamauka). Kulia kisauti au kikwikwi ndiyo njia ya kiasili ya mtoto aliyezaliwa karibuni kueleza mahitaji yake. Baada ya mtoto kutoka kwenye utunzi salama wa tumbo la uzazi la mama yake, mtoto aweza kujulisha maoni yake kwa sauti kubwa sana kwa kilio kitokacho moyoni!

Tia Moyo na Kuongoza Badala ya Kudai

Ni vema kutia moyo jitihada za watoto kueleza maoni yao. Huenda maoni yao yakafunua matatizo, na tatizo lililoeleweka wazi ni rahisi zaidi kutatua. Lakini jinsi tuitikiavyo matamko yao ni jambo la maana kwa kadiri moja na kuwafanya waeleze maoni yao. Wendy Schuman, mhariri mshirika wa gazeti Parents, atoa ushauri juu ya jinsi twapaswa kujaribu kuongea na watoto: “Kutia hisia-mwenzi katika maneno . . . ndilo wazo kuu linalokaziwa katika sehemu kubwa ya kazi ya hivi majuzi ya kufanya mawasiliano kati ya mzazi na mtoto. Lakini hisia-mwenzi tu haitoshi isipoonyeshwa kwa maneno ya kusikitikia. Na hilo ni jambo lisilokuja kiasili kwenye midomo ya wazazi walio wengi.”

Ndiyo kusema, ikiwa mtoto hana staha au amefanya jambo fulani la kushtusha, linalohitaji sahihisho, twapaswa kujaribu sana tusiache mtazamo wetu na hali ya sauti ilingane na udhia wetu au tafurani (tamauko). Bila shaka, ni rahisi kusema jambo hilo kuliko kulitenda. Lakini kumbuka kwamba, majibu makali-makali au yenye kupunguzia mtu hadhi, kama vile, “Jinga wewe” au, “Kwani hakuna jambo uwezalo kufanya vizuri?” hayaleti kamwe nafuu ya hali iliyokwisha kuwa ngumu tayari.

Wazazi wengi wamepata kwamba kusikitikia kwa kutoa pongezi, hasa kabla ya kushauri, kwaweza kuzaa matokeo chanya. Hapa tena ipo fursa ya kutazama mambo kupitia macho ya mtoto. Watoto walio wengi huwa wana habari sana wakati pongezi hiyo itolewapo kukiwa na kusudio jingine lililofichwa au wakati lisipotoka moyoni. Kwa hiyo, tunapowapa watoto wetu pongezi, twapaswa kuhakikisha kwamba sifa hiyo ni ya kweli na yastahiliwa.

Mwanasaikolojia maarufu, Dakt. Haim G. Ginott, katika kitabu chake Between Parent and Child, akazia kwamba wazazi wapaswa kusifu matimizo wala si utu. Kwa kielelezo, baada ya mwana wako kujenga kasha la vitabu na kukuonyesha wewe kwa fahari, elezo lako la kwamba, ‘Kasha hilo si la kuvutia tu bali pia lafaa matumizi,’ litajenga uhakika wake. Kwa nini? Kwa sababu unasifu timizo lake. Kwa sababu hiyo, sifa yako ina mafaa halisi kwa mtoto wako. Hata hivyo, usemi wa kwamba, ‘Wewe ni seremala mzuri,’ huenda usiwe na mafaa halisi, kwa kuwa unakaza fikira juu yake binafsi.

Dakt. Ginott aonelea hivi: “Watu walio wengi huamini kwamba sifa hujenga uhakika wa mtoto na kumfanya ahisi akiwa salama. Kwa kweli, huenda sifa ikatokeza mvuto wa ndani na mwenendo mbaya . . . Wakati mzazi aambiapo mtoto, ‘Wewe ni mvulana mwema sana,’ huenda asiweze kukubali hivyo kwa sababu maoni aliyo nayo juu yake mwenyewe ni tofauti kabisa . . . Sifa yapasa kushughulika, si na sifa za utu wa mtoto, bali na jitihada na matimizo yake . . . Sifa ina sehemu mbili: maneno yetu na kauli ambazo mtoto anakata. Maneno yetu yapasa yataarifu kwa wazi kwamba sisi twathamini jitihada, kazi, matimizo, msaada na ufikirio wa mtoto.”

Dokezo hili timamu la kutoa pongezi lapatana na ushauri uliovuviwa wa kuonyesha ukarimu, kama upatikanavyo kwenye Mithali 3:27: “Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, yakiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda.”—New International Version.

Kwa ukweli yaweza kusemwa kwamba hata kama twasoma ushauri gani mwema au shauri gani la hekima, hakuna njia ya mkato ya kutimiza ile ambayo wengine wameiita programu ya miaka 20 ya kulea mwana au binti. Yataka subira, upendo, uelewevu, na ufikirio. Lakini msaada mkubwa kuelekea kufanikiwa ni kujifunza kuona na kuelewa mwenendo wa mtoto wako mchanga “kupitia macho ya mtoto.”

“Mwana mwenye hekima humfurahisha babaye [hufanya baba ashangilie, NW],” akaandika Mfalme Solomoni mwenye hekima. (Mithali 10:1) Uelewevu mzuri zaidi wa njia ya kufikiri ya mtoto wako na maoni yake na ukusaidie wewe kushangilia ivyo hivyo.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki