Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 9/8 kur. 22-23
  • Uwasiliano Kati ya Daktari na Mgonjwa Ufunguo wa Mafanikio

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uwasiliano Kati ya Daktari na Mgonjwa Ufunguo wa Mafanikio
  • Amkeni!—1991
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Chanzo Tayari cha Msaada
  • Ithibati Kwamba Una Matokeo Mazuri
  • Mashahidi wa Yehova na Wastadi wa Tiba Washirikiana
    Amkeni!—1993
  • Je! Wewe Uko Tayari Kukabili Hali Ngumu ya Kitiba Yenye Kujaribu Imani?
    Huduma Yetu ya Ufalme—1990
  • Kulinda Salama Watoto Wenu na Matumizi Mabaya ya Damu
    Huduma Yetu ya Ufalme—1992
  • Msaada Katika Kudumisha Utakatifu wa Damu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 9/8 kur. 22-23

Uwasiliano Kati ya Daktari na Mgonjwa Ufunguo wa Mafanikio

KATIKA miaka ya mapema ya 1980, ilikuwa wazi kwamba hatua jasiri ya kujianzishia ilipasa kuchukuliwa ili kuweka mawasiliano mema zaidi kati ya Mashahidi wa Yehova na jamii ya kitiba. Kwa hiyo Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova lilidhiinisha programu fulani ili kuendeleza uhusiano wenye matokeo mazuri pamoja na madaktari na mahospitali.

Wawakilishi kutoka makao makuu ya ulimwengu ya Mashahidi katika Jiji la New York walizuru hospitali kubwa nyingi katika jiji hilo. Hilo lilithaminiwa sana na wafanya kazi wa hospitali, na liliweka msingi wa ushirikiano, badala ya mashindano. Wawakilishi hao baadaye waliendesha warsha (mikutano) katika majiji makubwa kuzunguka nchi hiyo. Jambo moja la warsha hizo lilikuwa ni kwenda pamoja na wahudumu Mashahidi wa Yehova walio wenyeji kwenye mikutano katika vitovu vya kitiba vilivyo katika eneo hilo, hivyo wakizoeza wahudumu hao kuendeleza programu. Walipokuwa Chicago, Illinois, U.S.A., walikutana na mwandishi wa Journal of the American Medical Association. Hii iliongoza kwenye mwaliko wa kuandikwa kwa makala moja juu ya jinsi madaktari wawezavyo kufanya kazi pamoja na Mashahidi wa Yehova.a

Baada ya muda, mazoezi na mielekezo iliyoandikwa iliandaliwa kwa msingi uliopanuka ili kwamba Mashahidi katika mabara mengine waweze kuanzisha programu kama hizo.b Kwa mfano, baada ya warsha moja kuongozwa katika Kanada, Halmashauri za Kupatanisha na Hospitali (ambazo baadaye zilikuja kuitwa Halmashauri za Kupatanisha Kitiba) zilifanyizwa na kuzoezwa. Kila halmashauri ilikuwa na wazee wa Kikristo wenye nia na uwezo wa kuzungumza na madaktari, wafanya kazi wa kijamii, na wafanya kazi wa hospitali.

Miadi ilifanywa pamoja na baadhi ya wahudumu wa afya mikoani, wakurugenzi wa mashirika ya kitiba na wa hospitali, na wengine wenye uwezo katika nyanja za kitiba. Mikutano hiyo ilisaidia kufanya jumuiya ya kitiba iweze kuwa macho zaidi kwa yale yanayohusu Mashahidi wa Yehova. Hivyo msingi imara uliwekwa kwa ajili ya mazungumzo ya wakati ujao.

Chanzo Tayari cha Msaada

Ilikuwa imethaminiwa kwa muda mrefu kwamba habari iliyo sahihi ni msaada mkubwa katika kumaliza mahitilafiano yoyote ambayo yangeelekea kutokea kati ya Wakristo wenye moyo mweupe na matabibu ambao hutegemea matibabu ya kutumia damu. Katika miaka ya mapema ya 1960 kwenye makao makuu ya Mashahidi wa Yehova, orodha ya madaktari wa kitiba wenye kushirikiana ilianza kukusanywa. Hawa walikuwa matabibu ambao walifahamiana na njia tofauti za kitiba kuhusiana na kutia damu mishipani. Baadaye, ikiwa daktari mwenyeji au hospitali haikustareheka juu ya kisa fulani, halmashauri fulani ingeweza kupata majina ya matabibu wengine. Mgonjwa huyo halafu angeweza kuhamishiwa kwenye kikundi kingine cha kitiba.

Njia nyingine ilikuwa kwamba Halmashauri za Kupatanisha na Hospitali huenda zingepanga kushauriana kwa simu kati ya daktari wa upasuaji aliye mwenyeji na wenzake wenye ujuzi. Nyakati nyingine namna hiyo ya uwasiliano wa mara moja iliwezesha madaktari kurekebisha matibabu yao, bila kuhatarisha mgonjwa. Hivyo, zikitumika kama kipatanisho kati ya mgonjwa na daktari, halmashauri hizo zimekuwa na ustadi katika kuondoa wasiwasi wa wote wawili mgonjwa na daktari wakati damu inapoonekana ni kama inahitajiwa.

Ithibati Kwamba Una Matokeo Mazuri

Sonya alikuwa kijana mchangamfu wa miaka 13 wakati ambapo, mapema katika 1989, alijua kwamba alikuwa na uvimbe wa kansa chini ya jicho moja. Daktari wa upasuaji alidhihirishia Sonya na wazazi wa msichana huyo umaana mkubwa wa upasuaji uliohitajiwa. Kwa sababu uvimbe huo ulikuwa ukikua kwa haraka, upasuaji haukupasa kuahirishwa. Ndipo utibabu wa kutumia kemikali ungehitajiwa, na daktari akasema kwamba wazazi wangelazimika kutoa ruhusa ya mitio ya damu mishipani. Lakini familia haingeweza kuidhinisha hilo kwa sababu ya masadikisho yao ya kidini. Daktari huyo mwanamke aliye mpasuaji hodari mwenye kumtunza Sonya alikubali kuondoa uvimbe huo wa kansa, akiwa na uhakika kwamba angefanya hivyo bila kutumia damu. Hata hivyo, kwa sababu ya mwongozo rasmi wa hospitali, mpasuaji hakupata daktari mwenye ujuzi wa dawa ya kugandisha ili kusaidia.

Jonathan ndiye kijana wa kwanza wa Michael na Valerie. Mwishoni mwishoni mwa 1989, alipokuwa na umri wa miaka 16, madaktari waliwajulisha wazazi kwamba Jonathan alikuwa na ukuzi mkubwa sana kwenye wengu lake. Madaktari kwanza walihofishwa juu ya upasuaji usiotumia damu, lakini kwa moyo mkuu wakafanya hivyo, wakistahi msimamo wa kidini wa familia. Wakati wa kipindi cha kupona, matataniko mabaya yalianza kujitokeza. Msukumo wa damu wa Jonathan ulipungua sana, na hesabu yake ya damu ikashuka. Katika upasuaji wa pili, alipoteza damu nyingi sana, hemoglobini yake ikishuka hadi 5.5, ambayo ni kama theluthi moja ya kipimo cha kawaida. Daktari wa sehemu za ndani mwilini akasema: “Hali ya kijana wenu inazorota sana. Hatuna la kufanya. Ikiwa yeye hatiwi damu, huenda akafa!” Tufanye nini sasa?

Halmashauri za Kupatanisha ziliandaa msaada muhimu katika visa vyote viwili hivyo katika Kanada. Moja ilihakikishia familia ya Sonya kwamba iwapo ingehitajika kabisa, wao wangeweza kusaidia kufanya mipango ili msichana huyo ahamishwe kwenye kitovu cha kitiba katika nchi nyingine. Lakini je! jambo fulani lingeweza kufanywa ili yule mpasuaji wa kike ambaye tayari alifahamiana na kisa chake aweze kuendelea? Kwa hakika, mpasuaji huyo alikuwa amefungamana sana na Sonya hivi kwamba alijitoa awe katika timu ya upasuaji mahali popote ambapo ungefanyiwa. Ingawa hivyo, uhamisho haukuhitajiwa. Washiriki wa halmashauri waliweza kuhimiza wafanya kazi wa kitiba wenyeji washirikiane na mpasuaji. Kulingana na daktari huyo, baada ya upasuaji huo wa muda wa saa nane u nusu, maneno ya kwanza ya Sonya yalikuwa swali la kuhangaikia kama alikuwa ametiwa damu kwa nguvu. Ilikuwa shangwe iliyoje kwa Sonya kujua kwamba jibu lilikuwa la!

Katika kisa cha Jonathan, kiwango chake cha damu kiliposhuka kufikia 5.5 baada ya kupasuliwa mara mbili, madaktari walisadiki kwamba ilihitajika kabisa kutia damu mishipani ili kuokoa uhai wake, na walikuwa tayari kupata idhini ya mahakama ili kulazimisha atiwe damu. Lakini imani imara ya Jonathan na ukinzano wake mwenyewe kwa utumizi wa damu ulifanya mambo yaende polepole. Jonathan anaripoti: “Nilimshika Dkt.—kwa ukosi wa shingo nikamtazama machoni na kumwambia, ‘Usitumie damu wala bidhaa za damu, TAFADHALI!’” Ile halmashauri ya ndugu waliozoezwa ilisaidia kupanga ili Jonathan apelekwe kwa ndege kwenye kituo cha kitiba kikubwa zaidi. Alipowasili, mshiriki wa halmashauri alikuwa kwenye hospitali na tayari alikuwa amezungumza na matabibu wenye kuhudumia. Siku iliyofuata hemoglobini yake iliimarika. Hesabu yake ya damu iliendelea kupata nafuu kwa uthabiti, na akaachiliwa siku 15 baada ya upasuaji ule wa kwanza.

Kwa wazi, kukiwa na idadi inayoongezeka ya wafanya kazi wa kitiba na wa kijamii walio na nia ya kufanya kazi pamoja na Halmashauri ya Kupatanisha na Hospitali ya Mashahidi wa Yehova, mafanikio mema ya uendelevu yaweza kutarajiwa.

[Maelezo ya Chini]

a Iliyochapishwa tena katika kurasa 27-9 za How Can Blood Save Your Life?, kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.

b Sasa kuna Halmashauri za Kupatanisha na Hospitali 100 katika United States, 31 katika Kanada, 67 katika Ufaransa, na nyingine zaidi katika mabara mengine kuzunguka tufe letu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki