Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g91 10/8 kur. 15-16
  • “Waheshimu Baba Yako na Mama Yako”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Waheshimu Baba Yako na Mama Yako”
  • Amkeni!—1991
  • Habari Zinazolingana
  • Heshimu Wanadamu Wa Namna Zote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Onyesha Wengine Heshima
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Heshimu Yehova, Kwa Nini Na Kwa Jinsi Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1991
  • Mpe Heshima Yule Anayestahili
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2017
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1991
g91 10/8 kur. 15-16

“Waheshimu Baba Yako na Mama Yako”

MANENO hayo yanatujia kutoka zamani za kale, karne nyingi kabla ya wakati wa Kristo. Yaliletwa kutoka juu ya mlima, yakiwa yameandikwa juu ya jiwe kwa kidole cha Mungu. Musa alikuwa ametumiwa kuwaongoza Waisraeli mateka kutoka kwa utumwa wa Kimisri, kupitia Bahari ya Nyekundu (Shamu), hadi kwenye kambi chini ya Mlima Sinai wenye mawemawe. Baada ya kutumia siku na usiku 40 pamoja na Yehova kwenye Mlima Sinai, Musa alikuja chini pamoja na vibamba viwili vya mawe ambavyo viliandikwa zile Amri Kumi.—Kutoka 34:1, 27, 28.

Juu ya kibamba kimoja iliandikwa amri ya tano, ambayo sasa huonekana kwenye Biblia katika Kutoka sura ya 20, mstari wa 12. Inasomeka hivi: “Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA [Yehova, NW], Mungu wako.” Kulingana na mtume Paulo, ndiyo “amri ya kwanza yenye ahadi,” ahadi ikiwa ni: “Ukae siku nyingi katika dunia.”—Waefeso 6:1-3.

Wonyesho wenye kutisha wa moto na moshi na tetemeko lenye kuogofya la Mlima Sinai wakati wa kutolewa kwa zile Amri Kumi kwa njia ya drama ilitangaza umaana wazo, kutia na ile ya tano, kutoa heshima kwa baba na mama. Ni nini kinachotiwa ndani katika kuonyesha heshima hii? Si heshima tu na utii bali pia utunzaji na utegemezo katika njia ya kimwili inapohitajiwa.

Hii ilifanywa wazi karne nyingi baadaye wakati Yesu alipokinzana na waandishi na mafarisayo kuhusiana na mapokeo yao. Yesu alionyesha kwamba wakati walipozuia utegemezo wa kimwili kutoka kwa wazazi walio na uhitaji, walikuwa wanakosa kuheshimu baba yao au mama yao. Aliwaambia, kama ilivyorekodiwa katika Mathayo 15:3-6: “Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na, Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Chochote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, basi asimheshimu baba yake na mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.”

Katika kisa cha Yesu mwenyewe, alionyesha utii kwa wazazi wake, akijiweka chini yao. (Luka 2:51) Miaka baadaye, alipokuwa anakufa juu ya mti wa mateso, alionyesha heshima kwa mama yake kwa kufanya andalizi la upendo kwa ajili ya utunzaji na utegemezo wake.—Yohana 19:25-27.

Mtume Paulo alijua vizuri sana kwamba lilikuwa takwa la Mungu kwa watoto, na hata wajukuu, kutunza wazazi wenye uhitaji. Na, kwa kupendeza, alihusisha usaidizi huo wa kimwili na wonyesho wa heshima: “Uwaheshimu wajane walio wajane kweli kweli. Lakini mjane akiwa ana watoto au wajukuu, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.” (1 Timotheo 5:3, 4) Wazazi wako walikutunza ulipokuwa kitoto kichanga kisichojiweza na ukiwa mtoto; na katika umri wao wa uzee, ni zamu yako kuwasaidia katika mahitaji yao.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki