Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 9/8 kur. 15-16
  • Ongezeko Kuu la Talaka

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ongezeko Kuu la Talaka
  • Amkeni!—1992
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Mkasa wa Tufeni Pote
  • Talaka Huwa na Majeruhi
    Amkeni!—1991
  • Talaka Matokeo Yayo Mabaya
    Amkeni!—1992
  • Je! Talaka Inapasa Kuruhusiwa?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • Jinsi Talaka Inavyowaathiri Watoto
    Msaada kwa Ajili ya Familia
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 9/8 kur. 15-16

Ongezeko Kuu la Talaka

“VITO VYA TALAKA.” Kichwa hicho cha habari kisicho cha kawaida kilitokea hivi karibuni katika gazeti la wanawake linalopendwa na wengi. Makala hiyo ilihimiza: “Kwa hiyo ndoa yako imelipuka na unahisi umechomeka. Kwa nini usiondolee mbali kumbukumbu hilo linalojaza sanduku lako la vito.” Watu waliotalikana hupewa tochi ya kuyeyusha chuma na mwuza vito aliye karibu na kuyeyusha vipuli vyao vya uchumba na vya ndoa kwa mchango fulani. Halafu yeye huvifinyanga katika umbo ambalo halitawakumbusha kuhusu ndoa zao zilizoshindwa.

Siku hizi, ndoa inapendwa zaidi na wengi ikiwa kwa namna inayoweza kutupwa kama vile kalamu, sahani, na wembe. ‘Unapochoka nayo, unaitupa tu’—ndio mwelekeo unaoenea sana.

“Hakuna kitu kama ndoa siku hizi,” akasema Lorenz Wachinger, mtungaji-vitabu, msaikolojia, na tabibu mashuhuri katika Munich, Ujerumani. Aliongezea chumvi zaidi? Labda; lakini si vigumu kuona kwa nini yeye angeweza kuhisi hivyo. Kulingana na gazeti Stuttgarter Zeitung, ndoa zipatazo 130,000 huvunjika kila mwaka katika Ujerumani. Lakini talaka si jambo linalotukia katika Ujerumani pekee.

Mkasa wa Tufeni Pote

Mwendo huo huo unaibuka katika nchi mbalimbali ulimwenguni pote. Kwa mfano, United States yaweza kuitwa kwa kufaa kitovu cha talaka ulimwenguni. Hesabu ya talaka ya kila mwaka ni zaidi ya 1,160,000 au karibu nusu ya hesabu za ndoa. Hiyo ni zaidi ya talaka mbili kwa kila dakika ya kila siku!

Inapochunguzwa kwa kulinganisha na muda mrefu uliopita wa historia, hesabu hizo zinaonyesha ongezeko kuu la talaka. Karne moja tu iliyopita, kulikuwako na talaka 1 tu kwa kila ndoa 18 katika United States. Isipokuwa ongezeko la ghafula baada ya Vita ya Ulimwengu ya 2, hesabu ya talaka iliongezeka polepole tu hadi miaka ya 1960. Halafu, katika muda wa miaka 25 tu, hesabu hiyo ikaongezeka mara tatu!

Katikati ya miaka ya 1980 (miaka ya karibuni zaidi ambayo tarakimu zenye kutegemeka zapatikana), nchi nyingi kuzunguka ulimwengu zilipata vilele vya talaka kama hivi: Urusi, 940,000 kila mwaka; Japani, 178,000; Uingereza, 159,000; Ufaransa, 107,000; Kanada, 61,000; Australia, 43,000. Hata katika mahali ambapo dini na sheria zimeweka hesabu ya talaka ikiwa chini, kuna mabadiliko yanayoendelea. Kwa mfano, katika Hong Kong bado kuna talaka 1 kwa kila ndoa 17; lakini hesabu ya talaka imekuwa maradufu katikati ya 1981 na 1987. Gazeti India Today liliripoti kwamba aibu inayoambatanishwa na talaka inakwisha miongoni mwa watu wa jamii ya kati katika India. Mahakama mpya zimeundwa katika majimbo kadha ya India ili kukabiliana na ongezeko la visa vya talaka kuanzia asilimia 100 hadi 328 katika mwongo mmoja tu.

Bila shaka, tarakimu hizo kubwa haziwezi kueleza mvunjiko wa moyo unaohisiwa. Kwa kusikitisha, talaka huhusu karibu kila mmoja wetu kwa sababu kimsingi, ndoa hufanywa ulimwenguni pote. Inaelekea kwamba, ama tumeoa au kuolewa ama sisi ni wazao wa wazazi waliooana, ama sisi ni wa karibu na watu waliofunga ndoa. Kwa hiyo hata ikiwa bado talaka haijatuumiza, tisho layo laweza bado kututia wasiwasi.

Ni nini kinachosababisha talaka hizo zote? Mabadiliko ya kisiasa yaweza kuwa sehemu ya jibu. Katika nchi nyingi, kuta za mikatazo ya Kitaifa dhidi ya talaka—iliyotegemezwa kwa muda mrefu na vikundi vya kidini vyenye nguvu—zimeporomoka katika miaka ya majuzi. Kwa mfano, katika miaka ya 1980, Argentina ilitangaza sheria iliyopinga talaka halali kuwa isiyo ya kikatiba. Uhispania na Italia vilevile zilianzisha talaka halali. Lakini mabadiliko ya sheria kama hayo hayaandamwi sikuzote na ongezeko katika hesabu za talaka.

Kwa hiyo lazima jambo fulani lenye uzito zaidi kuliko mfumo wa kisheria liwe ndilo linalosababisha mweneo wa talaka wa tufeni pote. Mwandikaji-vitabu Joseph Epstein aligusia hilo alipoandika kwamba katika wakati uliopita usio mrefu, “kutalikiwa kulimaanisha kuwa mtu ni kana kwamba anapata uhakikisho wa kisheria kwamba, yeye anakosa sifa zake.” Lakini leo, yeye aandika, “katika sehemu fulani fulani, jambo la mtu kuwa hajapata talaka laonekana kuwa lisilo la kawaida kuliko mtu kuwa amepata talaka; katika sehemu hizo mtu kuweza kuishi muda wake wa maisha akiwa bado katika ndoa yake ya kwanza kwaweza hata kufikiriwa kuwa kwaonyesha ukosefu wa kufikiri.”—Divorced in America.

Kwa maneno mengine, mitazamo ya msingi ambayo watu huwa nayo kuelekea ndoa imebadilika. Heshima na kicho kwa mpango ulioonwa kuwa mtakatifu kwa muda mrefu, sasa vinamomonyoka. Kwa hiyo kuzunguka ulimwengu, talaka inakubalika zaidi na zaidi. Kwa nini? Ni nini kingefanya watu walikubali jambo lililoonwa na wengi hapo mbeleni kuwa lisilofaa? Je! ingeweza kuwa kwamba talaka si mbaya sana kwa vyovyote?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki