Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 9/8 uku. 31
  • Uhuru wa Kidini Katika Bulgaria

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uhuru wa Kidini Katika Bulgaria
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Kampeni ya Pekee Nchini Bulgaria Yafanikiwa
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
  • Walijitoa kwa Hiari—Nchini Bulgaria
    Masimulizi ya Mashahidi wa Yehova
  • Ndoto Yangu Yaishia Kwenye Kiti cha Magurudumu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Mikusanyiko Uthibitisho wa Udugu Wetu
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 9/8 uku. 31

Uhuru wa Kidini Katika Bulgaria

Mabasi sita kutoka Bulgaria, yakiwa yamebeba wajumbe zaidi ya 300 kuelekea Mkusanyiko wa Wilaya wa “Wapendao Uhuru,” yalifika kwenye mahali pa mkusanyiko nje ya Thesalonike, Ugiriki, Alhamisi usiku, Julai 11, 1991. Wajumbe hao hawakuwa wameweza kupata viza zao hadi dakika ya mwisho kabisa kwa sababu ya vita vya wenyewe kwa wenyewe katika Yugoslavia iliyo jirani na hali ya msukosuko iliyotokea katika sehemu hiyo.

Jumatano alasiri wafanyakazi wa ubalozi katika Sofia, Bulgaria, walifanya kazi zaidi ya saa zao za kawaida ili kushughulikia viza hizo. Hivyo, mabasi hayo yaliweza kuwachukua wajumbe kwa wakati barabara kutoka sehemu mbalimbali za Bulgaria na kuweza kuwafikisha kwenye sehemu ya mkusanyiko usiku wa kabla ya mkusanyiko kuanza Ijumaa, Julai 12.

Wakati huo, Mashahidi wa Yehova walikuwa wamepigwa marufuku katika Bulgaria, kwa hiyo ilisisimua kama nini kufurahia ushirika wa Kikristo kwa uhuru katika nchi jirani ya Ugiriki! Kwenye sehemu ya mkusanyiko, jumba moja lenye jukwaa la kuvutia lenye madoido (linaloonekana kwenye picha), lilikuwa limetayarishiwa wageni Wabulgaria. Wageni hao walijawa na furaha na shukrani jinsi gani kupata kihalisi programu nzima ikitolewa katika lugha yao wenyewe! Tofauti ilikuwa drama tu. Hotuba ya dakika 15 ya muhtasari wayo ilitolewa katika Kibulgaria, na kisha wajumbe wakakutana na ndugu zao Wagiriki ili kutazama drama hiyo ikichezwa.

Jambo kuu katika mkusanyiko wa Wabulgaria lilikuwa hotuba ya ubatizo Jumamosi asubuhi. Kilele cha watu 342 walihudhuria, na 39 wakabatizwa (wengine wao wanaonekana wakisimama hapo juu). Wajumbe hao pia walisisimuliwa na kitolewaji cha broshua Roho za Wafu—Je! Zaweza Kukusaidia au Kukuumiza? Je! Ziko Kweli?, na kichapo Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia katika lugha yao wenyewe.

Lakini jambo lenye kusisimua zaidi ya yote liliwangoja wajumbe muda mfupi baada yao kurudi nyumbani Bulgaria. Katika Julai 17, muda usiozidi juma moja baada ya mkusanyiko, utendaji wa Mashahidi wa Yehova ulihalalishwa katika Bulgaria! Kwa kutokeza, mwezi uliofuata wahubiri wa kundi katika Bulgaria walifanya wastani wa saa 21.2 katika huduma. Jinsi tunavyoweza kuwa wenye furaha kwamba uhuru wa kidini unafurahiwa katika nchi nyingine bado ya Ulaya ya Mashariki!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki