Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 3/8 kur. 26-27
  • Mama Kumzalia Mwanamke Mwingine Mtoto—Je! Kwafaa Wakristo?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mama Kumzalia Mwanamke Mwingine Mtoto—Je! Kwafaa Wakristo?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maana ya Mama Kumzalia Mwanamke Mtoto Ni Nini?
  • Matatizo ya Kumzalia Mwingine Mtoto
  • Je! Mama Kumzalia Mwanamke Mtoto Huheshimu Ndoa?
  • Matibabu Mbalimbali na Masuala Yanayohusika
    Amkeni!—2004
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Ukurasa wa Pili
    Amkeni!—2002
  • Ongezeko la Watoto Wanaozaliwa kwa Njia Zisizo za Asili
    Amkeni!—2004
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 3/8 kur. 26-27

Maoni ya Biblia

Mama Kumzalia Mwanamke Mwingine Mtoto—Je! Kwafaa Wakristo?

MSHAIRI Mroma aitwaye Horace hakujua lolote kuhusu mama kumzalia mwanamke mtoto alipoandika: “Si kitu mtu awe amezaliwa na wazazi gani, maadamu awe ni mtu mstahifu.” Kanuni ya mwandikaji Mfaransa wa karne ya 17, “Kuzaliwa si kitu kusipokuwa wema,” iliandikwa pia muda mrefu kabla ya wazo la mama kumzalia mwanamke mtoto kuwa tatizo la kisheria. Lakini, kama vile Mary Thom alivyoripoti katika gazeti la Ms., kukiwa na tekinolojia mpya ya kuzalisha, “sehemu ya mwenye kutokeza yai, mhifadhi wa kiinitete kitakachokuwa mtoto, na mtunzi wa mtoto akishazaliwa” yaweza kugawanywa miongoni mwa “mama” wawili au watatu. Suala la “wema” na “si kitu” limekuwa lisiloeleweka na tata pia.

Zoea la kumzalia mwanamke mtoto lilianza ghafula ulimwenguni katika miaka ya katikati ya 1970, likizusha matatizo ya kijamii, kiadili, na kisheria yasiyopata kukabiliwa mbeleni. Wenzi wa ndoa wasiopata watoto walikuwa na hamu ya kutumia kwa faida yao aina hiyo ya kuzaa isiyo ya kawaida. Kwa upande mwingine, madaktari, mawakili, na wanasheria wameng’ang’ana kwenda sambamba na tekinolojia ya kuzaa inayopanuka katika jitihada za kuweka miongozo inayojibu masuala ya kiungwana na kiadili yaliyozushwa.

Maana ya Mama Kumzalia Mwanamke Mtoto Ni Nini?

Mama kumzalia mwanamke mtoto, au kukubaliana hivyo, hutukia wakati mwanamke aliyetiwa shahawa anapomzalia mwingine mtoto. Kule kuitwao kutungwa mimba kwa njia ya kawaida hutukia wakati mama mzaa anapotungwa mimba kwa shahawa ya mume kutoka kwa wenzi waliokubaliana naye. Hivyo, mama mzaa ndiye mama wa asili wa mtoto. Ujauzito wa mbegu na yai la mume na mke kutungwa katika mtu mwingine humaanisha kwamba yai la mke na shahawa ya mume huungana nje ya mimba katika utaratibu uitwao utungishaji (wa testi-tyubu), na kiinitete kinachofanyizwa hutiwa katika mji wa mimba wa mama mzaa kwa ajili ya ujauzito.

Kwa nini kumzalia mwanamke mtoto kumeongezeka? Kwanza, sayansi ya tekinolojia ya juu imevumbua njia kadha za kusaidia wanawake wapate watoto. Huenda wenzi wakatamani sana mtoto, na kwa sababu ya kutoweza kuzaa, tatizo, au watoto wachache walio na afya kuweza kuwachukua na kuwalea, wao hawana mtoto. Kwa hiyo wanakodisha mwili wa mtu mwingine ili wapate mtoto. Kwa kuwa inagharimu kiasi kikubwa cha pesa, kumzalia mwingine mtoto kumeitwa majina yasiyopendeza, kama vile “utwana na utumwa usio wa kujitakia” na “uchimbaji mgodi wa uzazi wa walio maskini.”

Katika United States, Mahakama Kuu ya New Jersey ilitambua uwezekano wa matajiri kuwatumia maskini kwa faida yao na katika kesi ya kumzalia mwingine mtoto ikasema: “Kwa kumalizia, kuna thamani ambazo jamii huona kuwa za maana zaidi ya kuupa utajiri chochote ambacho utajiri waweza kununua, iwe ni kazi, upendo, au uhai.” Mahakama Kuu ya Ufaransa ilisema kwamba kumzalia mwingine mtoto ni kumnajisi mwanamke na kwamba “mwili wa kibinadamu haupaswi kuazimwa, haupaswi kukodishwa, haupaswi kuuzwa.”

Matatizo ya Kumzalia Mwingine Mtoto

Mama anapomzalia mwanamke mtoto, hiyo huleta matatizo kadha. Mojawapo ni uwezekano wa vita vya kisheria visivyopendeza ikiwa mwanamke anayezaa anataka mtoto awe wake. Huyo ni mtoto wa nani, wa mwanamke anayezaa au wa mwanamke anayetoa mbegu? Kwa hiyo kuzaliwa kwa mtoto, ambako mara nyingi huwa wakati wa shangwe, nyakati nyingine huleta vita vya mahakamani. Tatizo jingine: Wanawake wengine wanaokubali kuzalia wengine mtoto hubadili hisia zao kadiri mtoto aliyefanyiwa makubaliano akuavyo na kuzaliwa. Makubaliano yaliyowekwa miezi michache mapema huwa magumu zaidi na zaidi kukubali. Uhusiano wenye nguvu wa kufungamanisha unafanyizwa kati ya mama mzaa na mtoto aliye ndani yake. Bila kutarajia ufungamano huo, mama mmoja mzaa alieleza hisi zake hivi kuhusu kumpeana mtoto: “Ilikuwa ni kana kwamba mtu fulani alikuwa amekufa. Mwili wangu ulikuwa ukimlilia binti yangu.”

Pia, ni matokeo gani ya muda mrefu ambayo mtoto huyo atakuwa nayo juu ya watoto wengineo wa mama mzaa, familia inayokubali mtoto huyo, na mtoto mwenyewe? Au ni nini kitatukia ikiwa mtoto anayezaliwa na mama mzaa ana kasoro ya mwili? Je! baba ana jukumu la kumchukua mtoto? Ikiwa sivyo, ni nani anayemtegemeza mtoto huyo kifedha? Na swali la maana hata zaidi, Maoni ya Mungu ni nini kuhusu mama kumzalia mwanamke mtoto?

Je! Mama Kumzalia Mwanamke Mtoto Huheshimu Ndoa?

Neno la Mungu hutuambia kwamba yeye huona ndoa kuwa jambo takatifu. Kwa mfano, Waebrania 13:4 husema: “Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.”a Mungu anatazamia Wakristo wote waone ndoa kuwa yenye kuheshimika na kuendelea kuwa hivyo. Ni nini huchafua ndoa? Uasherati, ambao waweza kuvunjia ndoa heshima kimbele, na uzinzi, ambao huvunjia ndoa heshima baada ya watu kufunga ndoa.

Je! mama anapomzalia mwanamke mtoto ni kuheshimu ndoa na kuweka kitanda cha ndoa kikiwa safi? Kwa wazi, la. Utungishaji mimba wa kawaida hutaka kutungwa mimba kwa mwanamke na shahawa ya mtoaji. Maoni ya Biblia yaweza kupatikana kwenye Mambo ya Walawi 18:20, ambayo husema: “Usilale na [usitoe kile kikutokacho kuwa shahawa kumpa, NW] mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.” Hakuna msingi wa Kibiblia wa kutofautisha kati ya utungaji mimba kwa kulala pamoja na utungaji mimba kwa njia isiyo ya asili kwa utungishaji uliochangwa. Kwa hiyo, katika kila kisa, uasherati au uzinzi hufanywa wakati utungaji mimba unapofanywa na mwanamume mwingine ila mume halali wa mwanamke mzaa.

Namna gani kuhusu ujauzito wa mbegu na yai la mume na mke kutungwa katika mzaa? Hiyo pia huchafua kitanda cha ndoa. Ni kweli, yai lililotungwa lingekuwa muungano wa mume na mke wake, lakini baadaye hutiwa katika mji wa mimba wa mwanamke mwingine na, kwa kweli, kumfanya atungwe mimba. Mimba hiyo haikusababishwa na uhusiano wa ngono kati ya mwanamke mzaa na mume wake mwenyewe. Hivyo, viungo vyake vya uzazi vinatumiwa sasa na mtu mwingine asiye mwenzi wake. Hiyo haipatani na kanuni za adili za Biblia kwamba mwanamke azae mtoto wa mume wake mwenyewe. (Linganisha Kumbukumbu la Torati 23:2.) Haingefaa mwanamume asiye mume wa mwanamke mzaa kutumia viungo vyake vya uzazi. Ni utumizi usiofaa wa kitanda cha ndoa. Hivyo, mama kumzalia mwanamke mtoto hakufai kwa Wakristo.

[Maelezo ya Chini]

a Kitabu cha marejezo New Testament Word Studies huonyesha kwamba “kitanda cha ndoa” cha Waebrania 13:4 humaanisha kwamba si hali tu ya ndoa bali pia utumizi wa ndoa haupaswi kuchafuliwa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 26]

Picha ya Mary Cassatt, Jumba la Uhifadhi wa Sanaa la Kitaifa, Zawadi ya Bi. Ralph J. Hines, 1960. (60.181)

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki