Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Mama Kumzalia Mwanamke Mwingine Mtoto Katika makala yenu “Mama Kumzalia Mwanamke Mwingine Mtoto—Je! Kwafaa Wakristo?” (Machi 8, 1993), mnanukuu Mambo ya Walawi 18:20, kuwa kinasema hivi (NW): “Usitoe kile kikutokacho kuwa shahawa kumpa mke wa mwenzako.” Lakini, tafsiri ya Union Version yasema tu kisahili hivi: “Usilale na mke wa mwenzio.” Tafsiri za The New English Bible na New American Standard Bible husema vivyo hivyo. Mnabadili Maandiko. Neno la Mungu la awali lilisema nini?

S. S., United States

Tafsiri nyingi hufasiri mstari huo. Tafsiri ya “New World Translation” huutafsiri neno kwa neno, kama zifanyavyo tafsiri zote mbili “The NIV Interlinear Hebrew-English Old Testament” na “The Interlinear Hebrew/Greek English Bible.” Tafsiri hiyo ya pili hulitafsiri mstari huo hivi: “Na usimpe mke wa jirani yako mbegu za kujamii.”—MHARIRI

Machozi Ile makala “Kwa Nini Kuna Machozi Haya Yote?” (Septemba 22, 1992, Kiingereza) ilinigusa moyo sana. Kwa muda fulani nimekuwa nikitaka kujua ni kwa nini sisi hulia na kwamba machozi yana fungu gani. Asanteni sana kwa makala hiyo iliyoandikwa vizuri, sasa naelewa. Ilinifanya nihisi kuwa mwenye shukrani sana kwa Yehova kwa jinsi alivyotuumba kwa njia ya kiajabu.

F. G., Ureno

Kusomea Nyumbani Nataka kuwashukuru sana kwa ile makala “Kusomea Nyumbani—Je! Kunakufaa Wewe?” (Aprili 8, 1993) Kwa sasa ninasomesha wawili kati ya watoto wangu wanne nyumbani. Mara nyingi wengine wameniambia kwamba ninalinda watoto wangu kupita kiasi. Nathamini sana msimamo wenu wa kutokuwamo juu ya suala hili.

B. W., United States

Masimulizi ya Maisha Ono la Marlene Pavlow, “Kumkaribia Mungu Kulinisaidia Niwezane na Hali” (Machi 22, 1993), labda ilikuwa ndiyo makala yenye kutia moyo zaidi ambayo nimepata kusoma. Nilipenda jinsi alivyosimulia maisha yake kwa njia ya unyoofu na ya waziwazi. Kwa vile nilikuwa nimekuwa na matatizo kama hayo, nilihisi kuwa na ushikamano fulani na Marlene. Asanteni kwa kuwa na makala nzuri ajabu kama hizo kwa watu sahili tu kama sisi. Inanifanya nihisi kwamba kuna tumaini kama kuna wengine ambao wana shangwe na huzuni kama sisi.

R. H., United States

Sijapata kusoma makala iliyonigusa moyo sana jinsi hiyo. Ilisimulia maisha yangu neno kwa neno. Lilikuwa jambo tu nililohitaji!

K. B., New Zealand

Kutumbuiza Ninaandika kuwapongeza kwa ajili ya makala “Je! Ungependa Kuwatumbuiza Rafiki Zako?” (Aprili 22, 1993) Nikiwa mwanamuziki asiye stadi, nilinufaika sana nayo. Mara nyingi rafiki zangu hunialika niende kuchangamsha vikusanyiko vya kirafiki kwa kucheza na kuimba. Madokezo yenu juu ya kusitawisha unamna-namna wa muziki na kuhusisha wasikilizaji katika wonyesho huo yalikuwa bora sana!

P. S. S. M., Brazili

Wanyama-Rafiki Katika makala “Je! Mtoto Wako Ahitaji Mnyama-Rafiki?” (Januari 22, 1993), mlisema hivi: “Paka wa nyumbani huambukiza akina mama waja-wazito wapatao 3,300 [ugonjwa wa neva uitwao] toksoplasmosisi kila mwaka, hilo likitokeza vifo vya vijusu kwa kiwango cha asilimia 15.” Kulingana na chanzo kingine chenye kutegemeka, kiwango cha kupitishwa kwa maradhi hayo ni kidogo. Je! hamtii chumvi kuhusu hatari za kuwa na paka?

K. T., Japan

Taarifa unayonukuu ilinukuliwa kutoka kwa “U.S.News & World Report.” Ingawa ni idadi ndogo kwa kulinganisha ya wanawake waja-wazito huambukizwa na paka, ile “Barua ya Afya Bora” iliyochapwa na Chuo Kikuu cha Kalifornia katika Berkeley bado ilitahadharisha wanawake waja-wazito dhidi ya “kukaribiana mno na paka.” Kwa uzuri, ni mara chache sana kwa maradhi hayo kupitishwa kwa kugusa tu paka. Ile “Barua ya Afya Bora” yasema hivi: “Maradhi hayo hupitishwa sanasana unaposhughulika na mavi ya paka, kama wakati wa kuondoa takataka za paka.”—MHARIRI

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki