Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 10/22 uku. 23
  • Je! Mazoezi Huwanufaisha Wazee-Wazee?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Mazoezi Huwanufaisha Wazee-Wazee?
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Unafanya Mazoezi ya Kutosha?
    Amkeni!—2005
  • Njia ya 3—Fanya Mazoezi
    Amkeni!—2011
  • Tunaweza Kuishi Muda Mrefu Kadiri Gani?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
  • Ni Nini Kitakachonichochea Kufanya Mazoezi?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 10/22 uku. 23

Je! Mazoezi Huwanufaisha Wazee-Wazee?

“Je! Mazoezi Yaweza Kubadili Mwendo wa Kuzeeka?” Hicho kilikuwa kichwa kikuu katika The New York Times karibu miaka mitano iliyopita. Makala hiyo iliripoti hivi: “Wanasayansi wa kitiba kutoka Chuo Kikuu cha Tufts [katika Boston] wamepata kwamba watu wenye kufikia hata umri wa miaka ya 90 waweza kuwa wenye nguvu zaidi na hata waongeze ukubwa wa misuli yao wakiwekwa katika utaratibu wa mazoezi makali ya uzani.”

Uthibitisho wa kwamba wazee-wazee wanaweza kunufaika kikweli na mazoezi umeendelea kuongezeka. Toleo la Harvard Health Letter la Februari 1991 liliripoti juu ya uchunguzi mmoja wa 1990, likisema hivi: “[Wakaaji tisa wa makao ya kutunzia wazee-wazee] wenye umri wa miaka kati ya 87 na 96 walimaliza mazoezi makali ya viungo vya mwili kwa kutumia mizani.” Kuhusu uchunguzi huo, Mayo Clinic Nutrition Letter laeleza hivi: “Walioshiriki waliongeza nguvu ya msuli wa mguu kwa karibu maradufu, na kuongeza ukubwa wa msuli wa paja kwa asilimia 9 na waliongeza uwezo wa wepesi wa mwili wao.”

Watafiti hao waliripoti hivi: “Itikio hilo zuri kwa mazoezi hayo ya kutoa nguvu kwa watu hao ni la kustaajabisha sana ukifikiria umri wao mkubwa, tabia zao za kupendelea upweke kabisa, maradhi mengi yenye kudumu, kutoweza kufanya mambo kikawaida na upungufu wa lishe.” Ubora wa mazoezi umethibitishwa tena na tena.

Kwa kielelezo, ebu fikiria Jack Siebert mwenye umri wa miaka 90, aliyeugua maradhi ya ghafula katika 1979 iliyopooza upande wake wa kulia na kumwacha bila uwezo wa kutembea pasipo msaada wa mkongojo. Kila asubuhi kwa miaka zaidi ya kumi amekuwa akilala kihalisi kitandani mwake na kubeba juu mguu wake wa kushoto usiopooza, akiusogeza kwa karibu dakika 20 katika mwendo kama ule wa kukanyaga baiskeli. Nyakati nyingine alikuwa akiegemeza mguu wake wa kulia uliopooza kwenye ule wa kushoto (kama ilivyo katika picha) na kuizungusha miguu hiyo miwili pamoja. Mazoezi hayo ya ukawaida hayajaimarisha tu misuli ya mguu wake ili kwamba bado aweze kutembea kwa mkongojo bali pia yamemsaidia adumishe mfumo wake wa moyo na mishipa ya damu na kufanya hivyo kumemfanya awe chonjo kiakili.

Kwa hiyo, kumbuka kwamba si kuchelewa mno kuanza mazoezi. Ni kweli kwamba huenda usiweze kukimbia ile mbio ndefu za Boston Marathon—mbio ya kilometa 42—katika muda wa saa tano na dakika tano, kama alivyofanya John Kelley mwenye umri wa miaka 82 katika 1990. Wala haielekei kwamba utaweza kumaliza mwendo huo katika muda wa saa saba na dakika tisa, kama alivyofanya nyanya mkongwe Mavis Lindgren mwenye umri wa miaka 84 katika 1991. Hata hivyo, Circulation, jarida moja la Shirika la Moyo la Amerika, lilihimiza hivi mwaka uliopita: “Ni muhimu kuwa na tabia ya kutafuta njia za kuwa mwenye utendaji.”

Jarida hilo lilieleza hivi: “Hata utendaji mdogo unaofanywa kila siku waweza kuwa na manufaa ya afya ya muda mrefu na kupunguza hatari ya kupatwa na maradhi ya moyo na mishipa. Utendaji mbalimbali kama huo watia ndani kutembea kwa ajili ya kujifurahisha, utunzaji wa bustani, kazi ya ua, kazi ya nyumbani, kucheza dansi na mazoezi ya nyumbani yaliyopendekezwa.”

[Picha katika ukurasa wa 23]

Mzee-mzee asiyejiweza aweza kunufaika na mazoezi, kama ilivyo na huyu aliye na umri wa miaka 90 aliyepatwa na maradhi ya ghafula

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki