Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 2/8 uku. 3
  • Kutunza Wazazi Wazee-Wazee

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutunza Wazazi Wazee-Wazee
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoa Utunzi—Kukabili Mikazo ya Siku kwa Siku
    Amkeni!—1994
  • Kuwaheshimu Wazazi Wetu Wazee-Wazee
    Siri ya Furaha ya Familia
  • Kuwatunza Waliozeeka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Waheshimuni Ndugu na Dada Waliozeeka
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 2/8 uku. 3

Kutunza Wazazi Wazee-Wazee

“SIKULALA mchana na usiku, lakini bado nilihisi kwamba lilikuwa pendeleo.” Hivyo ndivyo mwanamke mmoja alivyoeleza juu ya kutunza mamaye mzee-mzee.[1] Kwa mwanamke huyo, na wengine wengi, kutunza wazazi wanaozeeka ni ono lifaalo.

Pia hilo ni ono ambalo linakuwa la kawaida zaidi. Rika linalokua upesi zaidi katika United States lasemekana kuwa lile lenye miaka 75 na zaidi. Katika 1900, Waamerika wanaopungua milioni moja walikuwa wenye miaka 75 au wazee zaidi. Kufikia 1980 karibu milioni kumi walikuwa wenye miaka zaidi ya 75. Watu wazee-wazee wanaishi muda mrefu zaidi, na karibu theluthi moja ya wale wenye miaka 85 au zaidi wahitaji msaada wa kawaida.

Ingawa kutoa utunzi kwaweza kuwa ono lenye kunufaisha, hilo halikosi mkazo. Ikiwa mmoja wa wazazi wako au wote wawili ni wazee na wahitaji utunzi wako, huenda ukapata mambo fulani kuwa magumu. Kutazama tu afya yao ikizorota kwa kweli huleta uchungu. Na ikiwa hupokei msaada kutoka kwa washiriki wengineo wa familia, basi unaachiwa kazi yote ya kutoa utunzi.

Huenda pia ukagundua kwamba hata uwe una umri gani, huhisi kamwe kuwa mtu mzima mbele ya wazazi wako. Mwelekeo wao ni kukutendea kama mtoto mdogo, na mwelekeo wako waweza kuwa kuitikia kama mtoto.[4] Kukosa kutegemezwa kihisiamoyo na rafiki zako kwaweza kuongeza kiasi fulani cha mkazo kwenye kazi yako ya kutoa utunzi.

Hata hivyo, magumu ya kutunza wazee-wazee hayahitaji kuingilia kudumisha kwako uhusiano wa karibu na wazazi wako. Maandiko yaelekeza waziwazi watu wazima ‘wajifunze kwanza ujitoaji kimungu kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili lakubalika mbele za Mungu.’ Kwa upande mwingine, ‘amfukuzaye mamaye, ni mwana aaibishaye, na kuleta lawama.’—1 Timotheo 5:4; Mithali 19:26.

Ujitoaji kimungu unaoonyeshwa kupitia kutoa utunzi waweza kuwa ono lenye kunufaisha. Lakini kwanza, ni lazima ujue yale ambayo wazazi wako wahitaji hasa kutoka kwako yakiwa msaada. Makala zifuatazo zaweza kukusaidia katika kutambua na kutosheleza mahitaji hayo. Na ingawa makala hizo zakazia juu ya yale yanayoweza kufanywa nyumbani, inaeleweka kwamba katika visa fulani, kwa sababu ya afya mbaya sana au umri mkubwa sana, huenda mzazi akahitaji msaada wa wataalamu, kama ule upatikanao katika makao ya utunzi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki