Utafutaji Wenye Kusisimua wa Dawa Zilizo Mpya
Na mleta-habari za Amkeni! katika Uingereza
Kuna ufanano gani kati ya mpira, kakao, pamba na vigandisha-maumivu? Vyote vyaweza kupatikana kutokana na mimea. Zaidi ya sukari na oksijeni ifanyizwayo kwa njia ya usanidimwanga, [1] mimea ya kijani hutokeza pia vitu vingi ajabu vya namna mbalimbali katika kemikali za kwanza zilizo za msingi. Kemikali hizo za upili ndizo huupa kila mmea hali zenye kuupambanua kutokana na mimea mingineyo.[2]
MCHOMO wa kiwawi (mmea-mchomaji), ladha kali ya tufaha, na unukato wa waridi hutokana na miungano tofautitofauti ya vitu vya kikemikali vifanyizwavyo na mimea hiyo yenyewe. Hivyo, kile ambacho huenda kikaonekana kuwa zao moja tu kwa kweli huwa mara nyingi ni mchanganyiko tata sana.
Kemikali za Kiasili Zifuatazo Utaratibu Viwandani
Fikiria ile harufu ya kawaida ya kakao ya kunywa. Je! ulijua kwamba wanasayansi kufikia sasa wamegundua kemikali 84 tofautitofauti zenye kuyeyuka ambazo huungana kufanyiza harufu hiyo isiyo na kifani?[3] Vitu vilivyo katika maharagwe ya kakao ni tata kabisa, na jitihada nyingi zimefanywa miaka ya majuzi kuvitambua. Na hilo ni zao moja tu la kiasili.[4]
Kolesteroli ni kitu cha mafutamafuta, ambacho labda chajulikana zaidi kwa uwezekano wa kwamba chahusiana na ugonjwa wa moyo wa kibinadamu.[5] Hata hivyo, katika mimea fulani kitu hicho ndicho hatua ya kwanza ya kufanyiza kikundi muhimu cha kemikali ziitwazo steroidi.[6] Steroidi ni kutia na vitamini D, homoni (kama vile kotisoni), na dawa kama betamethasoni isiyoweza kuwashwa moto. [7] Dayosjenini, ambayo ni steroidi itumiwayo kutengeneza vizuia-mimba vya kupitishwa mdomoni, hutokezwa na namna fulani za kiazi-kikuu-mwitu.[8] Kotisoni, kwa upande mwingine, hutengenezwa kutokana na hekojenini, steroidi ya kiasili itolewayo katika nyamanyama ya jani la mkonge baada ya kupiga nyuzi.[9] Nyingi za dawa mpya za leo zilipatikana mara ya kwanza kutokana na tungamano la chembechembe za mmea.[16]
Mimea na Mwanadamu
Ingawa utumizi wa mwanadamu wa dawa za kufanyizwa kwa mashine ni hatua ya tiba ya ki-siku-hizi, vitu vilivyotolewa katika mimea vimetumiwa kama maponyo ya magonjwa ya kawaida kwa maelfu ya miaka. Kumbukumbu za mapema za Kiashuri zaeleza kwamba anemoni ya kawaida ilitumiwa kupunguza maumivu.[10] Na mafunjo ya tiba ya Misri kuanzia wakati wa Mafarao yafunua kwamba mimea ilitumiwa mahali pengi kama dawa.[12]
Shirika la Afya Ulimwenguni lina kumbukumbu za kwamba limetumia karibu mimea 20,000 kama dawa ulimwenguni pote. Katika Uingereza pekee kadiri ya tani 6,000 hadi 7,000 za mimea hutumiwa kila mwaka kuwa vichanganyio vya kutengeneza vitu tofauti vyapata 5,500 vilivyofanyizwa kwa mimea,[13] na katika United States, imekadiriwa kwamba zaidi ya nusu ya matibabu yote yatolewayo na madaktari huwa ya dawa zilizotolewa katika mimea.[15]
Kutafuta Dawa Zilizo Mpya
Wanasayansi hutafuta daima vidokezi vya kupata dawa zenye mafaa kwa kuwa ulimwenguni kuna namna 250,000 zijulikanazo za mimea, kila mmoja ukiweza kuwa na mchanganyiko wa kemikali zinazotofautiana kabisa na za ule mwingine. Moja ya njia za wazi ni kuchunguza jinsi watu watibuvyo maradhi kwa kutumia mimea inayokua katika eneo la kwao.
Kugunduliwa kwa kokeni kulianza na uchunguzi wa kwamba kutafuna majani ya koka kuligandisha maumivu makali ya njaa na kupunguza uchovu mwingi.[18] Kwa kutenga na kurekebisha umbo la molekyuli ya kokeni, wanakemia walifanyiza kitokano cha bandia kikatumiwa kama dawa ya kugandisha mahali palipoumia.[19] Ikiwa daktari wako wa meno amekudunga sindano ya kugandisha sehemu fulani ya utaya wako ili kukuepusha na maumivu, yawezekana kwamba hapo umenufaika na utafiti huo.[20]
Habari nyingi za thamani juu ya utumizi wa mimea zingali hazijafichuka wazi katika uchunguzi wa wataalamu wa mimea. Wanasayansi waliotumia zaidi ya miaka minne wakichunguza namna milioni 2.5 katika Gray Herbarium na Arnold Arboretum za Chuo Kikuu cha Harvard[21] waliweza kuonyesha hususa namna za mimea zaidi ya 5,000 ambazo hapo kwanza zilipitwa bila kuonwa kwamba zaweza kuwa vyanzo vya dawa.[22]
Upande mwingine wa utafiti hulinganisha kemikali zilizo katika mimea. Ikiwa namna moja ina vitu vyenye mafaa, basi namna zile ambazo zahusiana nayo huenda pia zikawa zenye thamani.[23] Wakati uchunguzi wa mti mmoja wa kaskazini mwa Australia, chestnati ya Ghuba ya Moreton, ilipotenga kastanospamaini kuwa mmea wenye sumu ya kukinza virusi,[24] wataalamu wa mimea wenye kutafuta miti inayohusiana na huo walidokeza kwamba utafiti ufanywe juu ya Alexa wa Amerika Kusini.[25]
Utafiti Dhidi ya Kansa
Nyakati fulani vidokezo vyaweza kupotosha kisha viwe na matokeo yasiyotarajiwa. Kwa kielelezo, ilidaiwa kwamba vitu vilivyotolewa katika mmea periwinko wa Madagaska vingeweza kutibu ugonjwa wa sukari. Watafiti wa Kanada walianza kuujaribu, lakini wakashangaa kuona kwamba dawa iliyotokana na periwinko iligandamiza mfumo wa kinga za mwili kwa kupunguza mfanyizo wa chembe nyeupe za damu.[28] Hiyo ikawapa madaktari wazo la kujaribu kama dawa hiyo ingekuwa na matokeo dhidi ya leukemia, kansa ya chembe nyeupe za damu.[29]
Hatimaye vitu karibu 90 vilitengwa,[30] na viwili kati yavyo, viitwavyo vinkristini na vinblastini, vikathibitika kuwa na mafaa ya kitiba.[31] Vitu hivyo huwa ndani ya mmea huo kwa kadiri ndogondogo hivi kwamba karibu tani moja ya vifanyizo vya mmea huo vyahitajiwa ili kufanyiza aunzi .07 ya vinkristini.[32] Leo vichanganyo hivyo na dawa zenye kutokana navyo huandaa matibabu ya kikemikali ambayo hutumiwa ulimwenguni pote kutibu leukemia ya watoto.[33]
Mwishoni-mwishoni mwa miaka ya 1950, Taasisi ya Kitaifa ya Kansa katika United States ilianzisha programu ya uchunguzi, na wakati huo dawa 114,000 zilizotolewa katika namna 40,000 za mimea zilijaribiwa kama zingeweza kukinza ukuzi wa chembe zenye kutokeza vivimbe vya kansa. Karibu 4,500 za dawa hizo zilizotolewa katika mimea zilikuwa na matokeo ya wazi, ya kustahili uchunguzi zaidi.[34] Lakini Dakt. W. C. Evans aliye stadi wa kuchunguza utendaji na athari za dawa aonyesha hivi: “Yaelekea sana kwamba dawa za matumizi mapana dhidi ya kansa haitapatikana” moja kwa moja kutokana na utafiti huo, ingawa ni wa maana sana.[35] Kansa hutofautiana sana, na ni namna chache tu za ukuzi wa chembe za kansa zilizotumiwa katika majaribio hayo.[36]
Dawa Zilizo Mpya Kutokana na Mimea Mizee
Mimea ijulikanayo sana inafanya watafiti wafikiri zaidi. Kwa kielelezo, tangawizi sasa inatumiwa kuzuia hali za kutaka kutapika, na ina matokeo hasa dhidi ya ugonjwa wa safarini.a[40] La maana zaidi, tangawizi ingeweza kuthibitika kuwa yenye thamani ya kuwatuliza wagonjwa wa kichocho. Majaribio yaliyofanywa juu ya watoto wa shule walioambukizwa katika Naijeria, kwa kutumia tembe za ungaunga wa tangawizi, yamekomesha kutokea kwa damu katika mkojo wao na kupunguza mayai ya kichocho ndani yao.[41]
Watafiti ni kama hata hawajaanza kile kibarua kigumu cha kutafuta dawa zaidi kutokana na milki ya mimea kwa jinsi ilivyo na mimea mingi ajabu. Hata mimea ile ambayo yajulikana sana ingali imeficha siri nyingi. Likorisi sasa ni mmea wenye kupendwa sana kwa kuwa kemikali zilizogunduliwa ndani zaweza kuwatuliza watu fulani wasumbuliwao na ugonjwa wa yabisi kavu.[42] Wanasayansi wanachunguza pia njugu ya kawaida kuona kama inaweza kukinza kuvu na vijiumbe viletavyo maradhi.[43]
Ule uharibifu ovyo wa namna za mimea unaofanyika katika maeneo fulani ya ulimwengu, kabla ya mimea hiyo kutiwa katika kumbukumbu, wamaanisha kwamba ni lazima dawa mpya ziendelee kutafutwa mbiombio. Bado kuna uhitaji mkubwa wa kuchunguza kwa uangalifu kemikali zilizo katika mimea na hifadhi ya chembe zayo za urithi, hata kuhusiana na mimea ijulikanayo sana.[44] Lakini kungali kuna utatanishi mmoja wa kutatuliwa: Nyingi za kemikali hizo za ajabu zina mafaa gani kwa mimea yenyewe?[45] Kwa kielelezo, kwa nini mmea pasleni hutokeza wingi mkubwa wa noradrinalini, homoni iliyoonwa kuwa ya maana kwa masilahi ya wanadamu?[47]
Kwa kweli, ujuzi wetu ni haba mno juu ya mambo yaliyo ya kutatanisha kuhusu mimea.[48] Lakini yale tujuayo yaonyesha kuna mbuni wa ujumla, na sifa yaenda kwa Mbuni fulani aliye Mkuu.
[Maelezo ya Chini]
a Ona ukurasa wa 31 wa toleo la Julai 22, 1982, la Amkeni! (Kiingereza).
[Picha katika ukurasa wa 24]
Tangawizi inatumiwa kama dawa ya kuzuia ugonjwa wa safarini