Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 8/8 kur. 11-13
  • Ukame Wenye Uharibifu Mkubwa Kusini mwa Afrika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukame Wenye Uharibifu Mkubwa Kusini mwa Afrika
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Vitatanishi Vingine
  • Suluhisho Ni Nini?
  • Ni Nini Linalofanywa?
  • Mvua Ikosapo Kunyesha
    Amkeni!—1999
  • Matatizo ya Wakulima Yanasababishwa na Nini?
    Amkeni!—2003
  • Kutoa Msaada kwa Walioathiriwa na Misiba
    Jinsi Michango Yako Inavyotumiwa
  • Matatizo ya Wakulima
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 8/8 kur. 11-13

Ukame Wenye Uharibifu Mkubwa Kusini mwa Afrika

NA MLETA-HABARI ZA AMKENI! KATIKA AFRIKA

WENGI walisema ndio ukame mbaya zaidi uliopata kutukia karne hii.[1] Baadhi hata walisema ndio mbaya zaidi uliopata kutukia katika historia ya kusini mwa Afrika.[2] Ukame huu wa miaka miwili uliokumba kusini mwa Afrika uliacha mkururo wa misiba.[2a] “Ni mbaya, tena sana, kuliko tulivyotazamia,” akataarifu mkuu wa Shughuli ya Kupambana na Njaa, ambacho ni kishirika cha kibinafsi cha Afrika Kusini cha kutoa misaada. “Safari za uchunguzi ni za kuvumbua kadiri zisizopata kujulikana za mateso, taabu na ukosefu wa kibinadamu.”[3]

“Huwezi kukuza chochote. Ardhi imekufa,” alitamauka mkulima mmoja wa kijiji.[4] Mahali fulani-fulani wanakijiji wenye njaa walikula matope au mizizi ya mimea-mwitu.[5] Mashirika yenye kugawa msaada wa chakula yalilemewa na uhitaji uliokuwapo.[6] Kulingana na The Guardian Weekly, “kusini mwa Afrika imepoteza kiasi kikubwa cha mazao yayo kuliko zilivyopoteza Ethiopia na Sudan katika ule ukame wa 1985.”[7]

Ukame huo ulifanya watu kama milioni 18 wakaribie kufa njaa.[8] Katika Angola hatari hiyo ndiyo mbaya zaidi iliyopata kutukia katika historia ya nchi hiyo.[9] Imekadiriwa kwamba mifugo milioni moja walikufa,[10] na katika mwaka mmoja karibu asilimia 60 ya mazao yaliharibika.[11] Haingewezekana kuwafikia watu walioathiriwa zaidi ili kuwasaidia.[12] Kufikia Agosti 1992, theluthi mbili za mazao ya Zambia yaliharibika, ikawa lazima kuingiza nchini tani milioni moja za mahindi kutoka nje.[13] Karibu watu milioni 1.7 walikuwa wakifa njaa.[14]

Katika Zimbabwe, iliyokuwa ikiitwa bohari la chakula kusini mwa Afrika, milioni nne walihitaji msaada wa chakula—karibu nusu ya idadi ya watu.[15] Katika eneo moja mwalimu wa shule alisema: “Maji ni haba na vyakula ni nadra. Hata ujani mmoja haukubakia ardhini.”[16]

Katika vijiji fulani watu walipanda juu ya miti kuchuma majani wayapike na kuyala.[17] Serikali ililazimika kupunguza msaada wayo wa chakula kutoka kilo 15 ukawa kilo 5 kwa kila mtu kwa mwezi.[18][19] Ziwa kubwa la Kariba lililofanyizwa na binadamu lilipungua zaidi ya wakati mwingineo wote,[20] na utumizi wa maji uliwekewa vizuizi Bulawayo.[20a]

Maelfu ya wanyama katika mashamba ya mbuga za Zimbabwe walilazimika kupigwa risasi, maana maji hayakuwatosha.[21] Gazeti moja liliripoti: “Ndege wafu wameanguka kutoka miti iliyonyauka, kobe, nyoka, wanyama-wagugunaji na wadudu wametoweka.”[22]

Msumbiji ilikuwa miongoni mwa nchi zilizoathiriwa zaidi na ukame.[23][24] Nchi hiyo ilipata asilimia 80 ya chakula chayo kwenye msaada wa kimataifa,[25] na kadirio moja lilikuwa kwamba watu milioni 3.2 walikuwa wakifa njaa.[26] Wakimbizi walimiminika Malawi, Afrika Kusini, Swaziland, na Zimbabwe. Lakini ukame ulipolegea zaidi majuzi, wakimbizi wengi wamerejea.[28]

Mara nyingi wanamajiji hawajui uzito wa ukame juu ya maisha za wanashamba. Ofisa ahusikaye na misaada ya chakula alisema: “Hasara zilizosababishwa na ukame huonekana kama matukio ya mbali kwa watu walio wengi maeneo ya mijini ambao wameponyoka upungufu mkali wa chakula na maji.”[29]

Ingawa mvua zilisaidia kidogo maeneo mengi, sehemu za Msumbiji, Swaziland, na Afrika Kusini bado zahitaji mvua zaidi. Bila shaka matokeo ya ukame huu yatahisiwa kwa miaka mingi ijayo.[29a]

Basi, ni wazi kisababishi kimoja cha ukame ni kukosa mvua. Lakini matokeo yao huzidishwa na matatizo mengine yastahiliyo ufikirio.

Vitatanishi Vingine

Katika Afrika nguvu za ukame huongezewa sana na kukosa uthabiti kisiasa.[30] Nchi ambazo zimekabili upungufu wa chakula ulio mkali zaidi ni zile ambazo zimekumbwa na ukosefu huo wa uthabiti. Vielelezo ni Angola, Ethiopia, Msumbiji, na Somalia.[31] Vita vimevuruga ukulima na kulazimisha wakulima wengi wakimbie, wakiacha mashamba yao bila kutunzwa.[32]

Kichangiaji kimoja cha ukame kibishaniwacho ni uchafuzi wa binadamu wa hali ya hewa na kuzidi kwa joto la dunia ambalo wengine husema ni matokeo ya uchafuzi huo.[33] Kichangiaji kingine ni ongezeko la idadi ya watu. Kadiri ya ukuzi wa wastani kila mwaka katika Afrika ni asilimia 3, ikiwa ni mojapo zilizo juu zaidi ulimwenguni.[34] Ili kuweza kulisha watu wengi zaidi, wakulima hulima ardhi isiyofaa ukulima na hawaachi ardhi ilale bila kulimwa ijirutubishe. [35]

Tena, misitu inaharibiwa, hasa kufyeka ili ardhi kubwa zaidi iwe ya ukulima.[36] Kulingana na gazeti African Insight, miaka 20 iliyopita asilimia 20 ya Ethiopia ilikuwa msitu; sasa ni asilimia 2 tu.[37] Wakuu fulani wasema kwamba kati ya matatizo yote ya mazingira yatishayo dunia, kufyeka misitu ndilo tatizo kubwa zaidi.[38] Hilo huathiri kawaida za hali ya hewa na kuchangia mmomonyoko wa udongo, na pia kuenea kwa maeneo ya jangwa.[39]

Serikali fulani za Kiafrika zimeweka bei za chakula na mifugo chini ili kuvutia wanunuzi wa mijini.[40] Hii huvunja moyo wakulima, wasioweza kulima wapate faida.[41] Serikali ya Zimbabwe iliitikia kwa kuongeza bei ya mahindi kwa asilimia 64 kuchochea wakulima waongeze mazao.[42]

Suluhisho Ni Nini?

Wastadi wana madokezo mengi. Lakini nyakati fulani wameshauri nchi za Kiafrika zifuate makulima ya Magharibi, yakawa yasiyofaa mazingira ya Afrika.[43]

Masuluhisho yenye kutumika yahitajiwa karibuni. Ofisa mkuu Mwafrika wa Tume ya UM ya Uchumi kwa Afrika alitaarifu: “Kwa msingi wa miradi yote ya kiuchumi ambayo tumeona hadi hapo, mwaka 2000 Afrika haitakuwa katika shimo ilimo sasa. Itakuwa katika lindi la kudidimia.”[44]

Ni wazi kinachotakwa ni uthabiti wa kisiasa na mwisho wa jeuri na vita.[45] Ushirikiano na nchi jirani ni muhimu pia.[46]

Kulingana na Shirika la UM la Chakula na Kilimo, Afrika yaweza kulisha idadi ya watu wayo wa sasa mara tatu.[49] Lakini mazao yayo yamekuwa yakipungua kwa miongo mingi, na kwa kadiri ya ukuzi wa sasa, idadi ya watu wayo ingeweza kurudufika muda wa miaka 30.[47][48][50]

Msaada wa chakula kutoka nchi za kigeni bila shaka umeokoa wengi wasife njaa. Hata hivyo, kusaidiwa hivyo kwa ukawaida silo suluhisho na kuna tokeo hasi kwa kuwa huvunja wakulima moyo wasiwe na mazao.[51] Huenda wasiweze kuuza mazao yao kwa bei nafuu, na mara nyingi watu huanza kupendelea vyakula vya kutoka nje wasitamani tena nafaka za kwao.[52]

Ni Nini Linalofanywa?

Jitihada zisizokoma za wengi watakao kusaidia watu wa Afrika kwa moyo mweupe zasifika. Katika maeneo fulani jitihada hizo zimekuwa na matokeo. Katika Zimbabwe kikoa cha watafiti wa kimataifa kimeanzisha mpango wa kupanda miti ikuayo vema na upesi kidogo katika maeneo makavu. Lengo ni kupanda miti hii kwa wingi ili kushinda shida ya viwasha-moto, kwa kuwa asilimia 80 ya watu hutumia kuni kupikia.[53][54][55]

Katika kijiji cha Charinge katika eneo lililokumbwa na ukame la Masvingo, Zimbabwe, wakulima wametiwa moyo watumie miamba kama kihifadhi-mboji katika mboga na mitunda yao.[56] Basi, wahitaji maji kidogo zaidi, na mazao yamekua vema sana. Wakulima hata waliweza kuwauzia chakula wahitaji wengine.[57]

Katika Afrika Kusini kampuni kubwa ilirekebisha kiwanda chayo cha kugeuza makaa-mawe kuwa mafuta ili kiweze kutakasa sana karibu maji yote yaliyokuwa yametumiwa kusafisha makaa-mawe.[60] Ingawa kutakaswa kwa maji ya viwandani kuna gharama, Afrika Kusini yakusudia kutakasa hatimaye karibu asilimia 70 ya maji yayo ya viwandani.[61]

Katika Luanshya, Zambia, maharagwe-soya yalianzishwa kutumiwa kuwa chakula-badala cha kulisha mwili.[62] Mfanyakazi wa misaada alisema: “Vifo vilivyo vingi kutokana na utapiamlo hutukia Machi na Juni vipunguapo vyakula vikuu vya kawaida. Hata hivyo, soya huvunwa Aprili na huhifadhika vizuri kuliko vyakula vikuu kama mahindi na mtama.”[63]

Hata jitihada hizo za kushinda matatizo ya ukame na upungufu wa chakula ziwe nzuri namna gani, mwanadamu, ajapokuwa na ufundi na maendeleo yake yote, ameshindwa kuzima ukame katika Afrika. Ni Mmoja tu aelewaye vihusika vyote, na alitabiri kale suluhisho. Chini ya utawala wa Ufalme wa Yehova Mungu kupitia Mfalme wake mwekwa, Yesu Kristo, karibuni maneno ya nabii Isaya yatatimia kihalisi duniani pote: “Katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Na mchanga ung’aao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji; katika makao ya mbweha, walipokuwa wamelala, patakuwa na majani, pamoja na mianzi na manyasi.”—Isaya 35:6, 7.

[Picha katika ukurasa wa 12]

Wanakijiji walishindania na mifugo maji machache yaliyosalia katika mashimo ya matope

[Hisani]

The Star, Johannesburg, S.A.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki