Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/8 uku. 10
  • Wewe Hukoroma?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wewe Hukoroma?
  • Amkeni!—1994
  • Habari Zinazolingana
  • Kutambua Matatizo ya Kukosa Usingizi
    Amkeni!—2004
  • Vijana Wanaosinzia—Je, Hilo Ni Jambo la Kuhangaisha?
    Amkeni!—2002
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1995
  • Jinsi ya Kuboresha Usingizi Wako
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 9/8 uku. 10

Wewe Hukoroma?

WEWE ni mkoromaji sana? Watu hukoroma sana na hata hawajui hivyo. Hivyo, hawajui kwa nini wao huamka wakijihisi wanyonge na kulewalewa miguu. Kasoro yao yajulikana kuwa kikatiza-pumzi usingizini. Ingawa mtu mwenye kasoro hii hulala, misuli ya koo iwekayo wazi vipito vya pumzi hulegea kiasi cha kufunga kipitio cha hewa. Muda wa kufikia dakika moja huenda ukapita kabla mtu huyo hajashtuka kutafuta hewa na kuamka kwa muda mfupi. Walio wengi wa wakatiza-pumzi usingizini hawajui usingizi wao umevurugwa. Mwenye kuwadokezea hivyo peke yake huenda akawa ni mwanachumba aamshwaye mara nyingi na kule kukoroma. Wastadi huamini kwamba kikatiza-pumzi usingizini huchangia aksidenti za magari na za kikazi na kwamba huenda kikawa ni kisababishi cha kiharusi na magonjwa-ghafula ya moyo.[1]

Je, kuna utatuzi? Complete Home Medical Guide (Koleji ya Chuo Kikuu cha Columbia cha Matabibu na Wapasuaji) chashauri: “Wanaume huathiriwa mara 20 zaidi ya wanawake. Zaidi ya nusu ya waathiriwa wana mafuta kupita kiasi, jambo ambalo hupunguza mtiririko wa kawaida wa hewa. Basi, kupunguza uzito ni sehemu ya maana ya matibabu.” Chanzo hichohicho chadokeza kwamba katika visa vikali, huenda ikafaa kupasuliwa ili kupunguza uzuizi ulio katika kipitio cha hewa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki