Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 9/8 kur. 14-15
  • Ni Nini Kiwezacho Kusaidia Mkazo Wako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nini Kiwezacho Kusaidia Mkazo Wako?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Epuka Matarajio Yasiyo ya Kiasi
  • Dhibiti Mkazo wa Kutimiza Mambo
  • Mambo Uwezayo Kufanya
  • Jinsi ya Kudhibiti Mfadhaiko
    Amkeni!—2010
  • Jinsi ya Kukabiliana na Mkazo
    Amkeni!—2020
  • Ninaweza Kukabiliana Jinsi Gani na Mikazo Shuleni?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Mkazo Mzuri, Mkazo Mbaya
    Amkeni!—1998
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 9/8 kur. 14-15

Maoni ya Biblia

Ni Nini Kiwezacho Kusaidia Mkazo Wako?

WEWE una mkazo? Ikiwa ndivyo, kuna wengi kama wewe. Hizi ni “nyakati za taabu,” na watu wa umri na tabaka zote za maisha wanapatwa na mkazo. (2 Timotheo 3:1, Habari Njema kwa Watu Wote) Wastadi fulani wadai kwamba zaidi ya nusu ya ziara zote kwa daktari husababishwa na matatizo yahusianayo na mkazo.[1]

Hata hivyo si lazima mkazo wenyewe uwe ni jambo baya. “Kwa kweli,” asema mkurugenzi wa kliniki ya wenye mikazo, “ndio hutupa msisimko wetu, idili ya kuishi, nishati ya kufanya mambo. Sisi huufurahia—tukiweza kuudhibiti.”[2]

Kwa upande mwingine, mkazo waweza kuharibu sana, kuangamiza. Basi, namna gani ikiwa mkazo unakusababishia matatizo? Haya ni madokezo machache yenye msingi wa hekima ya Biblia yawezayo kukusaidia upunguze athari zao zenye kuharibu.

Epuka Matarajio Yasiyo ya Kiasi

“Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua,” yasema Biblia. (Mithali 13:12) Matarajio yasipotimizwa kamwe, mkazo waweza kulemea. Huwa ni kama lazima itukie hivyo tujiwekeapo matarajio ya juu kupita kiasi.

Kwa kielelezo, vyombo vya kutangaza biashara vimehadaa wengi kuamini kwamba furaha yao hutegemea kuwa na vitu vya kimwili. Mtu atamanipo vitu asivyoviweza, matokeo yaweza kuwa mkazo na kuvurugika hisia. Hivyo Biblia hutoa ushauri huu: “Tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.” (1 Timotheo 6:8) Ndiyo, hata ingawa huenda usiwe na gari, nyumba, au fanicha ambayo ungependa iwe mali yako mwenyewe, thamini kile ulicho nacho. Uwe na matarajio ya kiasi ya vitu vya kimwili.

Matarajio yasiyo ya kiasi kuhusu watu yaweza pia kuleta mkazo. Kwa kielelezo, ingawa mwajiri au msimamizi ana haki ya kutarajia utendaji kazi wa kadiri nzuri kwa wale awasimamiao, ni upumbavu kutarajia ukamilifu kwao. Carlos, msimamizi Mbrazili wa kiwanda, asema: “Sharti uwakubali watu jinsi walivyo. Ukitarajia mengi kuliko wawezayo, mkazo utaongezeka, ikifanya kila mtu akose furaha.”[3]—Linganisha Yeremia 17:5-8.

Dhibiti Mkazo wa Kutimiza Mambo

Latin America Daily Post lafunua chanzo kingine cha mkazo, likitaarifu kwamba ‘tabia ya kuelekea kutimiza mambo na kushindana ni kisababishi kikubwa cha ugonjwa wa moyo.’[10] Mhasibu kijana akubali hivi: “Ofisini mimi huwa na wasiwasi sana na kuogopa kuonyesha nina udhaifu wowote. Mimi hufanya kazi sana na kuhisi ninavurugika hisia kwa kutotambuliwa na wengine.”[5]

Kuhusu jitihada hizo za kutafuta utambuzi na kutimiza mambo, Sulemani alisema: “Nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.”—Mhubiri 4:4.

Ukweli ni kwamba, ‘si wenye mbio washindao sikuzote’ katika kupanda cheo kazini au kupata utambuzi. (Mhubiri 9:11) Maria, mfanyakazi Mbrazili wa ofisini, alieleza hivi: “Huenda mtu akawa ana uwezo, lakini hali, na labda hata upendeleo, zaweza kumzuia asipande cheo.”[6]—Linganisha Mhubiri 2:21; 10:6.

Kaa bila kutarajia ya kupita kiasi na utambue mapungukiwa yako. Ifanyie kazi shangwe ambayo kazi yenyewe huileta badala ya kufanya kazi ili upande cheo tu. (Mhubiri 2:24) Kwa kweli, mtu mwenye uroho wa kutimiza mambo si kwamba hupoteza kiasi kikubwa tu cha shangwe ya kuishi bali pia aweza kupatwa na mkazo sana hata aharibu jitihada zake mwenyewe za kufanikiwa. Hivyo Dakt. Arnold Fox alishauri hivi: “Kutaka kuwa mtu aliye bora zaidi katika kazi yako ni mradi wenye kutamanika, lakini usiruhusu wazo hilo moja tu litawale maisha yako. Ukipuuza mawazo ya kuwa na upendo, kucheka, na shangwe ya kuishi, au uking’ang’ania sana mafanikio hata usahau kufurahia maisha, unajiletea mkazo.”[7]

Mambo Uwezayo Kufanya

Njia nyingine ya kujitahidi kuondosha mkazo wa mibano ya kila siku ni kusitawisha ucheshi. (Mhubiri 3:4) Si lazima uwe stadi wa kuchekesha ili kuwa na mtazamo mchangamfu. “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri; bali roho iliyopondeka huikausha mifupa.”—Mithali 17:22.

Wewe una elekeo la kuahirisha mambo? Hatimaye, kuahirisha huongeza mkazo badala ya kuupunguza. Biblia hushauri: “Msilegee katika bidii.” (Warumi 12:11, HNWW) Fanya orodha, ya maandishi au ya akilini, ya mambo uhitajiyo kufanya. (Mithali 21:5) Halafu amua mambo yahitajiyo kufanywa kwanza—na uanze kuyafanya.

Namna gani ikiwa, ujapojitahidi sana, bado wahisi umesongwa au umekazika? Huenda ukahitaji kujitahidi sana kubadili kufikiri kwako. Usikae ukiwazawaza makosa yaliyopita. Hii yaweza kuongezea sana mkazo wa sasa. Mwanafalsafa wa karne ya 19 aliandika: “Maisha huweza kueleweka tu kwa kutazama ya nyuma; lakini ili kuishi maisha ni lazima kutazama ya mbele.”[8] Ingawa twaweza kujifunza kwa yaliyotushinda, matendo yetu ya sasa ndiyo hufanyiza wakati wetu ujao.

Mfalme Daudi alionyesha dawa bora zaidi ya mkazo aliposali hivi kwa Yehova: “Taabu za moyo wangu zimeongezeka; unitoe katika huzuni yangu.” (Zaburi 25:17, ZSB) Ndiyo, Daudi alitegemea Mungu alegeze mahangaiko yake. Ukitumia wakati kusoma na kutafakari Neno la Mungu, wewe pia utajihisi karibu zaidi na Mungu. Upatapo kuthamini makusudi ya Mungu, utasukumwa kutanguliza masilahi yake maishani mwako, na hiyo itakulegezea mahangaiko mengi yasiyo ya lazima. (Mathayo 6:31, 33) Jifunze kuishi siku kwa siku. Mbona uongeze mahangaiko ya kesho kwa yale ya leo? Yesu alieleza hivi: “Msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.”—Mathayo 6:34.

[Blabu katika ukurasa wa 15]

“Huenda mtu akawa ana uwezo, lakini hali, na labda hata upendeleo, zaweza kumzuia asipande cheo”

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 14]

The Metropolitan Museum of Art, Fedha zilitolewa na Josephine Bay Paul na C. Michael Paul Foundation, Inc., na Charles Ulrick na Josephine Bay Foundation, Inc., na Fletcher Fund, 1967y.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki