Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/22 kur. 16-17
  • Zanzibar—“Kisiwa cha Vikolezo”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Zanzibar—“Kisiwa cha Vikolezo”
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Karafuu na Utumizi Wazo
  • Watu
  • Mchango Wangu Katika Kuendeleza Elimu ya Biblia Ulimwenguni
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Tamaa Ambazo Zilibadili Ulimwengu
    Amkeni!—1993
  • Kisiwa Kilichotokea na Kutoweka
    Amkeni!—2004
  • Wamishonari Wangesafiri Hadi Wapi Upande wa Mashariki?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 2/22 kur. 16-17

Zanzibar—“Kisiwa cha Vikolezo”

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA KENYA

KILOMETA 35 kuelekea pwani ya Afrika mashariki-kati hukaa kisiwa Zanzibar. Kikiwa kimezungukwa na maji ya buluu yenye ujoto-joto ya Bahari ya Hindi, kikiwa na mkururo wa bichi nyeupe na kupambwa kwa milima yenye miinuko na mishuko na minazi inayoyumbayumba katika upepo wa msimu, Zanzibar ni kisiwa chenye kuvutia. Kikiwa kidogo kwa kulinganishwa—kilometa 85 kwenye urefu wacho mkubwa zaidi na upana wa kilometa 39—kimekuwa na sehemu muhimu sana katika historia ya Afrika.

Kwa karne nyingi Waajemi, Waarabu, Wahindi, Wareno, Waingereza, Waasia, Waamerika wa Kaskazini, na bila shaka, Waafrika wa bara wamezuru Zanzibar. Uvutio mkuu wakati huo ulikuwa ile biashara ya watumwa yenye faida sana. Palikuwa pia mahali ambapo wanabiashara na wavumbuzi walipata ugavi wao. Kwa kweli, wengi wa wavumbuzi wa Afrika walio Wazungu katika karne ya 19 walipitia kisiwa kidogo hiki! Si ajabu kilikuja kuitwa Lango la Afrika.

Karafuu na Utumizi Wazo

Sultani wa Omani, Sayid Said, aliacha nchi alikozaliwa kwenye Ghuba ya Uajemi na kukaa Zanzibar katika nusu ya kwanza ya miaka ya 1800. Akiwa mtawala wa kisiwa kidogo hiki, aliwafanya Waarabu wenye mashamba waache kupanda nazi na badala ya hivyo wapande mmea wenye faida zaidi: karafuu. Kufikia mwisho wa maisha yake, faida za karafuu zilipitwa tu na biashara ya watumwa na pembe za ndovu. Kwa hiyo biashara ya watumwa ilipokomeshwa, Zanzibar kilikuja kuitwa Kisiwa cha Vikolezo. Leo ndicho chanzo kikuu cha karafuu duniani.

Karafuu hasa ni matumba ya maua yaliyokaushwa ya mti fulani wa kitropiki usiokauka. Jina la kisayansi la mti huo ni Eugenia caryophyllata. Katika Zanzibar, mti wa wastani una kimo cha meta 9. Kwa kawaida matumba ya maua huvunwa yanapokuwa yenye rangi nyekundu-kahawia na yakiwa na ukubwa wa sentimeta 1.3 hivi. Mti wenye afya waweza kutokeza hadi kilogramu 34 za matumba. Baada ya kuvunwa yanaanikwa ili yakauke katika jua kali la kitropiki.

Kwa sababu ya harufu yazo ya kunukia na ladha nzito, karafuu hutumiwa hasa katika upishi. Utamu wa vyakula vya nyama na mboga huongezwa kwa kutumia karafuu. Au waweza kuponda-ponda kijuu-juu matumba manne au matano, uyaongeze katika maji yachemkayo, na kutayarisha chai iliyokolezwa! Na katika siku baridi ya kipupwe, divai nyekundu yaweza kufanywa kuwa kinywaji chenye kuburudisha kwa kuipasha moto na kuongeza karafuu chache. Wengine hutumia karafuu ili kufanya bafu zao zinukie kwa kutia ndani ya chungwa karafuu 20 na kulining’iniza kwa juma moja hivi. Madaktari wa meno wametumia mafuta ya karafuu kuwa nusukaputi ya kienyeji ya kutuliza maumivu ya jino. Karafuu hutumiwa pia katika dawa za kusukutulia mdomo na manukato. Si ajabu kwamba kisiwa hiki duni chajulikana sana kwa mmea wake wa vikolezo!

Watu

“Kikolezo” halisi cha Zanzibar ni wenyeji wa huko. Mara tu ukanyagapo kwenye kisiwa hicho, wakaribishwa kwa uchangamfu na Wazanzibari. Wao waonekana wakiwa watulivu na huchukua wakati kusemezana. Wanapokuwa wakiongea, huenda wakasalimiana kwa mikono kwa kurudia-rudia, labda mara tatu au nne katika muda wa dakika kumi. Hivi ndivyo wao huitikia kiasili kwa chochote kisemwacho chenye ucheshi.

Ukitembelea moja ya nyumba zao, utakaribishwa kwa ukarimu wao ujulikanao sana. Mgeni kila wakati lazima apewe kilicho bora kabisa. Afikapo pasipo kutazamiwa wakati wa mlo, hakuna shaka: Lazima ajiunge na kula hadi kutosheka. Ukarimu kama huo ni kumbukumbu la nyakati za Biblia.—Linganisha Mwanzo 18:1-8.

Wazanzibari pia ni wenye umaridadi na wa kipekee. Wanawake huvalia buibui waendapo nje ya nyumba. Kwa kupendeza, hili laweza kuvaliwa juu ya vazi la mtindo wa nchi za Magharibi. Kwa habari ya wanaume, wao huonekana wakiwa wamevalia kanzu. Wao huvalia kofia iliyosokotwa.

Akitembea kupitia sehemu ya kihistoria ya jiji la Zanzibar inayoitwa Mji wa Mawe, mtu huhisi kama kwamba amerudishwa nyuma katika wakati uliopita. Ule mzingo wa barabara na vichochoro hauna vijia. Milango ya maduka kadhaa hufunguka moja kwa moja kwenye barabara! Halafu kuna wachuuzi wa barabarani, kama wale wanaouza Kahawa tamu ya Kiarabika, iliyokolezwa kwa tangawizi.

Hata hivyo, wala maneno wala picha hazielezi vya kutosha uvutio wa Zanzibar. Sifa yacho kikiwa “kisiwa cha vikolezo” yastahiliwa sana katika njia nyingi.

[Ramani katika ukurasa wa 16]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

ZANZIBAR

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 17]

Afrika na ramani ya mipaka: The Complete Encyclopedia of Illustration/J. G. Heck

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki