Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 2/22 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Lile Fumbo la “Ujiuaji Makusudi” la Mbwa
  • Vyombo vya Kujisalimisha
  • Hatari za Afya Kutokana na Ukulima
  • Makasisi Waanglikana na Mungu Wao wa Kubuni
  • Ukosefu wa Usalama Duniani Kote
  • Mbwa Kabambe Wanaotangatanga
  • Baraza Kuu Jipya la Maaskofu Katika Australia
  • Mizigo Isiyodaiwa
  • Kijengo Kitakatifu cha Ushindi wa Nasibu
  • Misri Ina Barabara ya Lami Iliyo ya Kale Zaidi
  • Walsingham—Patakatifu pa Uingereza Penye Kubishaniwa
    Amkeni!—1994
  • Biblia Inabadili Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1995
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kuabudu Katika Maeneo Matakatifu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
Amkeni!—1995
g95 2/22 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Lile Fumbo la “Ujiuaji Makusudi” la Mbwa

Watu wa Rosario, Argentina, wanatafuta maelezo ya kusadikisha ya kile kinachoonekana kuwa wimbi la “ujiuaji makusudi” ujaribiwao na mbwa katika jiji hilo. Tatizo hilo limeonekana hasa katika uwanja maarufu wa starehe wa Rosario ujulikanao kuwa Parque de España. Mahali pa kutembelea katika uwanja huo pameinuka kwa kama futi 90 juu ya Mto Paraná. Katika kipindi cha mwaka mmoja, kumekuwa na matukio karibu 50 ambayo mbwa kwa ghafula walijiponyoa, wakakimbia moja kwa moja hadi ukingo wa mahali pa kutembelea, na kuruka mpaka karibu kufa. Hata hivyo, kulingana na wenye ujuzi, mbwa hawawezi kuamua kujiua. Badala ya hilo, madaktari wa mifugo hufikiri kwamba mbwa huchochewa na makelele mengi mno au mwendo wa ndege au mashua ndani ya mto. Nao hukimbilia kuelekea ukingoni, lakini kabla ya kutambua, wanajikuta wakiporomoka chini ndani ya ufa.

Vyombo vya Kujisalimisha

Kulingana na The Toronto Star, Wakanada wengi zaidi wananunua vyombo vya kujisalimisha vyenye kubebeka kwa ajili ya kujilinda. Miongoni mwa vile vijulikanavyo sana ni “vipiga-makelele” au “vipiga-mayowe”—kengele za binafsi za kasimawimbi. Pia zipo chupa ndogo zilizo na kemikali zenye kuvunda zilizoundwa ili kuvunja moyo mshambuliaji na rangi za erosoli zifanyazo iwe rahisi kumtambua baadaye, aliyepuliziwa rangi ya kijani kibichi. Hata hivyo, gazeti la Star linasema kwamba “vyombo vya kujisalimisha havihakikishi kwamba mtu hatatendwa uhalifu. Kujikinga kwa kutumia akili ya mtu mwenyewe, kulingana na wasemavyo polisi, kwaweza kuwa kwa maana zaidi kuliko vyombo vya tekinolojia.”

Hatari za Afya Kutokana na Ukulima

Viuakuvu, viuamagugu, na viuawadudu vimesaidia wakulima kupunguza kuharibika kwa mimea yao. Hata hivyo, ripoti kutoka Shirika la Kimataifa la Wafanyakazi yasema kwamba kemikali za ukulima zinahusika moja kwa moja na vifo vya wafanyakazi wa shamba kama 40,000 kila mwaka. Inakadiriwa kwamba kemikali hizi zinaathiri sana afya ya watu wengine milioni 3.5 hadi milioni 5.

Makasisi Waanglikana na Mungu Wao wa Kubuni

Hivi karibuni Kanisa la Uingereza liliondoa mmoja wa makasisi walo. Kasisi huyo alikuwa akifundisha waziwazi kutoamini katika Mungu mwenye uwezo upitao ule wa asili, katika mamlaka ya Biblia, na katika Yesu akiwa mwokozi. Ajapokosa kuheshimu mafundisho ya Biblia na ya kanisa waziwazi, kuondoshwa kwake kulitokeza sikitiko kwa makasisi wengine. Makasisi 75 wa Kanisa la Uingereza walitia sahihi barua ya watu wote wakiomba kwamba kasisi aliyeondolewa aruhusiwe kuendelea akiwa kasisi. Makasisi fulani hudai kwamba kuna mamia ya makasisi wenzao Waanglikana wasioamini katika Mungu mwenye uwezo upitao ule wa asili.

Ukosefu wa Usalama Duniani Kote

Kuhusu Mkutano wa Viongozi wa Ulimwengu Kwa Ajili Ya Maendeleo ya Kijamii katika Machi 1995, kile chama cha UNDP (Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa) kilitoa barua kikieleza hangaiko lacho kwa ajili ya usalama wa wanadamu. Barua hiyo, iliyotoa maneno yayo katika Human Development Report 1994, ilionelea kwamba “mwanzoni mwa karne hii, karibu asilimia 90 ya majeruhi wa vita walikuwa wanajeshi. Leo, karibu asilimia 90 ni wananchi—badiliko lenye msiba katika usawaziko wa mambo.” Kile chama cha UNDP kinakubali kwamba usalama wa kibinadamu unatishwa bila kujali mahali unapoishi. Gazeti la Human Development Report laongeza kwamba “njaa, magombano ya kikabila, kushuka kwa ustaarabu, ugaidi, uchafuzi na usafirishaji wa dawa za kulevya yameacha kuwa matukio ya mara kwa mara, yaliyomo katika mipaka ya kitaifa. Matokeo yayo yameenea duniani kote.”

Mbwa Kabambe Wanaotangatanga

Kulingana na The New York Times, majiji mengi ya upande wa Mashariki ya Marekani yanakabiliwa na tatizo linaloongezeka la mbwa kabambe wanaotangatanga barabarani. Tom Simon, ofisa wa Ofisi ya Kudhibiti Mbwa aeleza kwamba si lazima iwe mbwa hao wote ni hatari. Yeye alisema kwamba “ikiwa wanazoezwa ifaavyo, wanaweza kuwa mbwa wapole na vipenzi wa kuvutia.” Lakini jambo baya la uhakika ni kwamba mbwa hao hatari waliotajwa hapo juu kwa silika ni wapiganaji wenye jeuri na wamezoezwa kuwa hivyo. Mbwa fulani wanateswa kikatili “ili kuwafanya kuwa wabaya zaidi,” mstadi mmoja akasema. Baada ya kushiriki katika mapigano jeuri na katili ya mbwa, mbwa wengi wanashindwa kupigana tena. Jambo hili litokeapo, mara nyingi wenye mbwa hao wanawaachilia mbwa hao hatari watangetange barabarani.

Baraza Kuu Jipya la Maaskofu Katika Australia

Katika 1946, idadi kadhaa ya makanisa katika Australia yaliunda Baraza la Makanisa la Australia. Kanisa Katoliki la Kiroma halikupata kuwa mwanachama lakini liliruhusiwa kujua yanayoendelea kwa miaka mingi. Sasa, karibu miaka 50 baadaye, baraza hilo limepewa jina jipya, Baraza la Kitaifa la Makanisa katika Australia. Washiriki walo wameongezeka kwa mmoja tu—Kanisa Katoliki. Kanisa la Lutheri lilialikwa kujiunga na shirika hilo jipya, lakini lilikataa mwaliko huo, kwa sababu si wengi wa washiriki walo waliopendelea jambo hilo. The Sydney Morning Herald lilisema kwamba David Gill, aliyetawazwa kuwa karani wa mambo ya ujumla ya baraza hilo jipya, alisema juu yao kuwa “wakisali kikichaa,” naye akaongeza hivi: “Mimi nafikiri kwamba kuna badiliko dogo katika jambo hilo.” Yeye alikuwa akirejezea kwa mabaraza ya awali “kuwa kama sanamu ya serikali.” Ilisemwa kwamba, “mkazo ulionekana kuwa upande wa haki za kijamii badala ya kueneza Habari Njema.” Gazeti hilo liliongeza hivi: “Kukosa kurudia yale waevanjeli huyaita ‘maswala ya gospeli’ kumetokeza tatizo kubwa, ambalo bado halijatatuliwa.”

Mizigo Isiyodaiwa

Mizigo yote isiyodaiwa iwachwayo kwenye shirika kuu la usafirishaji la Marekani hufanywa nini? Hiyo huuzwa kwa kampuni ya Scottsboro, Alabama, iitwayo Kitovu cha Mizigo Isiyodaiwa. Hapo hufunguliwa, husafishwa, huchunguzwa kama ina pesa, kisha huuzwa upya kwa wananchi. “Mtazamo mfupi tu ndani ya Mizigo Isiyodaiwa unatosha kumfanya hata msafiri wa ndege mwenye utumainifu mwingi zaidi awe akibeba mizigo myepesi tu,” lasema The Wall Street Journal. “Maduka manne makubwa huuza kila kitu kuanzia makoti ya manyoya na ndoana hadi T-shati na kamera. . . . Pia unaweza kupata vikaanga-tosti, virembeshi, pembe za paa, kanda za nyimbo za kitamaduni za Hungaria, hata jeneza.” Wafanyakazi wa ndege hubeba karibu vifurushi milioni mbili kila siku, na ingawa wanapoteza au hawapati karibu 10,000 hadi 20,000 za vifurushi hivyo, vichache kuliko 200 havirudishiwi wenyewe. Wasafiri hupewa miezi mitatu ili kudai vifurushi vyao vilivyopotea kabla havijasafirishwa vikauzwe. “Kampuni za ndege zisemapo haziwezi kuwapata wenye vifurushi hivyo vyenye kusafirishwa Scottsboro, makarani huko husema kwamba wanatumia saa nyingi wakipasua na kufuta majina na anwani zilizosafirishwa navyo kabla ya kuviuza,” ndivyo gazeti Journal lisemavyo.

Kijengo Kitakatifu cha Ushindi wa Nasibu

Kisiwa kidogo, kilichokuwa bila umaarufu katika kusini mwa Japani kwa ghafula kimekuwa maarufu, hayo yote kwa ajili ya jina la kijengo kitakatifu cha Shinto. Jina lacho, Hoto, humaanisha “pata hazina kwa nasibu,” na kikundi cha wenyeji chenye maendeleo kimekichuma kwa matokeo yapitayo matazamio yacho makubwa. Walifanya kijengo hicho kitakatifu kuwa mahali pa kuuzia mifuko ambamo watu wangeweza kuweka tikiti zao za bahati nasibu. Wakitumia hii “mifuko ya bahati nasibu” iliyonunuliwa kutoka kijengo hicho kitakatifu, wao wakasema, kunahakikisha tikiti hizo za bahati nasibu zitapata donge kubwa. Tangu hapo, “watu wanaotazamia kushinda fedha nyingi kwa bahati nasibu wamekuwa wakimiminika kuteremka huko kwenye Kijengo Kitakatifu cha Hoto,” lasema Asahi Evening News. Hata hivyo, si “mamiminiko” haya bali ni kijengo kitakatifu hicho kimechuma donge kubwa, kwa kuuza mifuko kwa dola 10 na dola 30 kila mmoja.

Misri Ina Barabara ya Lami Iliyo ya Kale Zaidi

Wachunguzi wa ardhi wamegundua barabara ya mawe ya kilometa 12 iliyopita jangwani kilometa 69 kusini-magharibi mwa Cairo. Barabara hiyo ya kale, iliyotengenezwa kwa chokaa-mawe, changarawe, na kwa miti iliyofanywa migumu, imejulikana tangu 2600 mpaka 2200 K.W.K., katika kipindi cha ule Ufalme wa Kale. Ina upana wa wastani wa meta mbili. Barabara hiyo ilitengenezwa ili kurahisisha usafirishaji wa mawe mazito kutoka kware kubwa ya mawe meusi magumu hadi ukingo wa ziwa la kale lililoungana na mto Naili ulipofurika. Ziwa hilo halipo tena. Mawe meusi hayo yalipendelewa na watawala Wamisri wa kale kwa ajili ya utengenezaji wa majeneza ya mawe na mapito yaliyotandazwa ndani ya mahekalu ya Giza ya mahali pa kuhifadhia maiti. “Barabara hii ni ushindi mwingine wa tekinolojia unaosifu Misri ya kale,” akasema profesa mwanajiolojia Dakt. James A. Harrell. Barabara ya mawe katika Krete, iliyojulikana tangu 2000 K.W.K., hapo mbeleni ndiyo iliyokuwa barabara ya lami iliyo ya kale zaidi.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki