Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 9/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Makanisa ya Ujerumani Yakiri Lawama la Teketezo la Umati
  • Hekalu la Kutengana
  • Macho Hufanya Kazi Maradufu
  • “Mtakatifu Mfadhili” kwa Ajili ya Sinema
  • Ni Uhai wa Baada ya Kifo au Kuona na Kusikia Vitu Visivyokuwako?
  • Nusu ya Dunia Ingali Nyika
  • Wachezea Mungu Kamari?
  • Ubaya wa Kukaa Kitandani Wakati wa Ugonjwa
  • Mataifa Tajiri Kuliko Yote Ulimwenguni
  • Walsingham—Patakatifu pa Uingereza Penye Kubishaniwa
    Amkeni!—1994
  • Biblia Inabadili Maisha
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—1997
  • Je, Wakristo Wanapaswa Kuabudu Katika Maeneo Matakatifu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2016
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 9/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Makanisa ya Ujerumani Yakiri Lawama la Teketezo la Umati

Januari 1995 ulitia alama miaka 50 tangu kuwekwa huru kwa kambi za mateso katika Auschwitz, Poland, ambapo Wanazi walinyanyasa kwa mfululizo Wayahudi, Waslavi, Wajipsi, Mashahidi wa Yehova, na wengine. Makanisa fulani katika Ujerumani yanakubali lawama. Süddeutsche Zeitung liliripoti kwamba Kongamano la Maaskofu wa Ujerumani lilifafanua ile “historia iliyojawa na hatia ya nchi yetu na pia kanisa letu,” wakikiri kwamba “kulikuwa na makosa mengi mno na hatia miongoni mwa Wakatoliki. Wakatoliki wengi walikubali mafundisho ya Usoshalisti wa Kitaifa na kubaki bila kujali uhalifu.” Mwenyekiti wa Shirika la Makanisa ya Kiprotestanti katika Ujerumani aliungama kwamba “katika njia hii chungu ya kutambua kosa na hatia, tumekuja kujua kwamba hata theolojia ya Kikristo na kanisa vilikuwa na sehemu katika historia ndefu ya kujiepusha na kuwa na uadui kuelekea Wayahudi.”

Hekalu la Kutengana

Watu wanaotumaini kupata talaka au kutengana katika mahusiano mengine wasiyotaka wanaenda kwa idadi kubwa kwenye hekalu la Shinto katika Ashikaga, kilometa 80, kaskazini mwa Tokyo. Likiitwa Hekalu la Kuvunja Kifungo cha Jamaa, hilo yaonekana kuwa ndilo hekalu pekee la Shinto katika Japani lenye kukubali maombi kwa ajili ya talaka, lasema gazeti Asahi Evening News. Kila siku, waabudu wengi hufika. Kila mmoja huandika ombi lake kwenye ema, kibao chembamba, kukining’iniza katika kitalu cha hilo hekalu, na kusali kwamba miungu ijibu. Hilo gazeti laeleza kwamba miaka mia moja hivi iliyopita, hilo hekalu lilipoanzishwa, “wake za wafanya biashara matajiri wenyeji waliandika sala zao kwamba waume zao waache wapenzi wao na kuwarudia.” Ingawa hivyo, leo, maombi yenye bidii yanayotolewa si ya kurudiana tena.

Macho Hufanya Kazi Maradufu

Jicho la binadamu lina kazi zaidi ya moja, watafiti wasema. Moja, bila shaka, ni kutupa mwono. Ile nyingine, iliyogunduliwa majuzi na kuripotiwa katika The New England Journal of Medicine, ni kupokea mipwito ya nuru ambayo hurekebisha saa ya kila siku ya ndani ya mwili. Kwa kuwa kazi hii ya pili hutenda bila uhusiano na uwezo wa kuona, hata watu ambao ni vipofu kabisa na wasio na utambuzi wa nuru wanaweza kuwa na saa za ndani ya mwili zifanyazo kazi kikawaida. Huo ugunduzi waweza kuongoza kwenye mabadiliko katika kutibu vipofu. Kwa kielelezo, zoea moja la kawaida ni kuondoa macho ya walio vipofu kabisa na kuyabadilisha na macho ya kutengenezwa ambayo yana sura yenye kuvutia. Pia, watu walio vipofu kabisa kwa kawaida hawachunguzwi magonjwa kama glaukoma, ambayo hukinga uwezo wa retina wa kupokea nuru. Kama tokeo, akasema Dakt. Charles A. Czeisler, msimamizi wa hicho kikundi cha utafiti, wengi wa watu hawa hawawezi tena kurekebisha saa za ndani kwa ile kawaida ya usiku-na-mchana ya muda wa saa 24, ikitokeza tatizo la kudumu la usingizi ambalo linafanana na uchovu unaotokana na kusafiri kupitia kanda tofauti za majira.

“Mtakatifu Mfadhili” kwa Ajili ya Sinema

Biashara ya sinema karibuni itapata “mfadhili mtakatifu” wayo yenyewe, laripoti El País, gazeti la Madrid, Hispania. Ili kuadhimisha mwaka wa mia moja wa kwanza wa biashara ya sinema, Vatikani inachanganua washindanaji wawezekanao. Mtakatifu anayependwa na wengi ni Francis wa Assisi, mvumbuzi wa mandhari ya kuzaliwa kwa Yesu, ambayo wafanya-filamu wengi huona kuwa hatua ya mapema ya “mandhari ya Hollywood.” Jina jingine lililodokezwa ni Juan Bosco, kasisi Msalesia ambaye alitumia utumbuizo kuwa chombo cha kufundishia watoto. Mkurugenzi mmoja wa filamu alidokeza “Mtakatifu Domingo de Guzmán, aliyevumbua Baraza la Kuhukumu Wazushi, moja ya maonyesho ya kwanza ya kutazamisha zaidi.” Televisheni, shani ya majuzi zaidi, tayari ina “Santa” Clara akiwa “mtakatifu mfadhili.” Yeye alichaguliwa kwa kuwa alikuwa akihudhuria Misa kwa kutazama kupitia dirisha la jela aliyokuwa amefungiwa. Hata hivyo, hakuna uthibitisho kwamba watakatifu wana uwezo wa kusimamia kupanga programu.

Ni Uhai wa Baada ya Kifo au Kuona na Kusikia Vitu Visivyokuwako?

Vyombo vya habari kwa kawaida hutangaza maono ya “kunusurika kifo,” ambapo wagonjwa waliokaribia kufa baadaye hudai kwamba walipata miono ya uhai wa baada ya kifo. Majaribio ya kikundi cha wanurolojia Wajerumani yalidokeza majuzi kwamba maono hayo yanasababishwa na ukosefu wa oksijeni, ambao husababisha kuona na kusikia vitu visivyokuwako. Kulingana na gazeti la Kiholanzi De Gooi en Eemlander, hicho kikundi kilichunguza vijana 42 wenye afya ambao walifanywa wazimie kwa muda usiopita sekunde 22 kwa upishaji hewa safi kupita kiasi. Baadaye, hao vijana walifafanua hisi na maono yanayofanana kwa njia ya kutazamisha na “maono ya kunusurika kifo.” Baadhi yao waliripoti kwamba waliona rangi na nuru kali mno, wakijiona kutoka mwono wa angani, wakiwaona wapendwa katika mazingira yenye kupendeza, na kadhalika. Vijana wengi walifafanua hizo hisi kuwa zenye kupendeza na zenye amani—kwa kiwango cha kwamba hawakutaka kurudia fahamu.

Nusu ya Dunia Ingali Nyika

“Japo jitihada bora zaidi za wanadamu, ni zaidi tu ya nusu ya uso wa bara la sayari Dunia iliyo nyika,” laripoti gazeti New Scientist. Uchunguzi mpya “ulipata kwamba kilometa za mraba milioni 90 za bara, asilimia 52 hivi ya eneo lote la bara, bado ni nyika.” Kwa nini uchunguzi huu uko juu sana kuliko matokeo ya uchunguzi wa 1989, ambayo yaliorodhesha thuluthi tu ya dunia kuwa nyika? Kwa sababu uchunguzi huu wa karibuni zaidi, uliofanywa na Lee Hannah wa Conservation International, ulitia ndani maeneo yaliyo madogo kiwango cha kilometa 1,000 za mraba, badala ya kilometa 4,000 za mraba za kiwango cha chini kilichotumiwa wakati uliopita. “Hata uchunguzi wa kina zaidi yaelekea ungefunua asilimia nyingine kubwa zaidi tena ya sayari iliyo nyika,” hiyo makala ilitaarifu. Hata hivyo, Hannah alitaja kwamba sehemu kubwa sana ya bara lililo nyika ni “mwamba, barafu na mchanga wenye dharuba,” isiyoweza kukalika na wote binadamu na wanyama. “Makao ya asili yameondolewa na usumbufu wa binadamu kwa zaidi ya robo tatu ya ardhi iwezayo kukalika ya sayari,” yeye alisema. Sehemu tatu za huo uchunguzi zilikuwa: nyika (asilimia 52), maeneo yaliyokaliwa kwa sehemu (asilimia 24), na maeneo yaliyokaliwa kikamili (asilimia 24).

Wachezea Mungu Kamari?

Kila mwaka, watu wapatao milioni 29 humiminika kwa idadi kubwa kuelekea Las Vegas, Nevada, Marekani, kutoka ulimwenguni pote. Wengi wao, bila shaka, wako pale ili kucheza kamari, lakini wengi wao wanataka kusali na kuabudu vilevile. Kwa hiyo dayosisi ya Katoliki katika eneo hilo hivi majuzi lilijenga kanisa la gharama ya dola milioni 3.5, lenye viti 2,200 jengo moja tu kutoka mahali ambapo pana kasino kubwa za hoteli nne zilizo kubwa kuliko zote jijini, laripoti The New York Times. Kwa kuwa asilimia 80 ya waabudu katika hilo kanisa ni watalii, kanisa huwakaribisha kuweka visarafu vya kasino katika sahani ya kukusanya sadaka. Hilo kanisa pia lina duka la zawadi, ambapo wanunuzi wanakaribishwa kutumia visarafu vyao kama fedha. Hilo duka hata linatoa kisarafu cha kumbukumbu cha kuchezea kamari chenye mfano wa Yesu Kristo. Kwa muda fulani hilo kanisa lilimwajiri mtawa wa Kifransiska ili kuzunguka kila juma katika kasino zote ili kubadilisha na kupata pesa kwa visarafu vilivyochangwa kwa ajili ya kanisa.

Ubaya wa Kukaa Kitandani Wakati wa Ugonjwa

“Kukaa kitandani kwa muda mrefu kwaweza kusababishia wagonjwa umizo zaidi badala ya kuwasaidia,” ladai The Times la London. Yapata miaka 50 iliyopita, tabibu Sir Richard Asher alitilia shaka kawaida hii ya kitiba ikubaliwayo kote naye akavuta fikira kwa hatari za kitiba kama vile kuganda kwa damu, kufinyaa kwa misuli, kupoteza Kalsiamu katika mifupa, vijiwe vya figo, kufunga choo, na mshuko-moyo. Uchunguzi umehakikisha onyo hili, na chunguzi zimeonyesha kwamba hatari ya kuganda kwa damu ikifuatiwa na kufinyika kwa mishipa ya damu katika mapafu kwenye kufisha kunahusiana moja kwa moja muda wa kukaa kitandani kabla ya kifo. Kwa upande ule mwingine, madaktari huunga mkono kukaa kitandani katika visa vya maumivu makali ya mshipa wa fahamu wa mgongo na matatizo ya baadaye ya ujauzito. Kwa kweli, kwa habari ya magonjwa mengine yenye maumivu makali au yaliyo hatari, huenda kusiwe na kibadala kingine ila kupumzika. Hata hivyo, madaktari wanaamini kwamba mara tu tatizo lipitapo, kuamka na kutembeatembea huharakisha hali ya kupata nafuu.

Mataifa Tajiri Kuliko Yote Ulimwenguni

Uswisi ndilo taifa tajiri kuliko yote ulimwenguni, kulingana na ripoti iliyotolewa na Banki ya Ulimwengu. Pato layo kwa kila mtu—thamani ya vitu vyote na utumishi vinavyotokezwa—lilikuwa dola 36,410 katika 1993. Hii ilikuwa karibu dola 12,000 zaidi ya Marekani, ambayo ilikuwa ya saba katika orodha. Baada ya Uswisi kulikuwa Luxembourg, Japani, Denmark, Norway, Sweden, Marekani, Iceland, Ujerumani, na Kuwait. Msumbiji ilibaki kuwa taifa maskini kuliko yote ulimwenguni, ikitokeza dola 80 kwa mtu mmoja. Mataifa yaliyokosekana katika hii orodha ya karibuni ya kumi bora yalikuwa mataifa kadhaa ya Mashariki ya Kati yenye kutokeza mafuta, jambo linaloonyesha kushuka kwa bei za mafuta. Hata hivyo, orodha yabadilika ukifikiria uwezo wa kununua. Kwa sababu bei za bidhaa ziko chini katika Marekani zaidi ya nchi nyingi tajiri, Wamarekani hupata thamani zaidi kwa fedha zao zaidi ya taifa jinginelo lote isipokuwa Luxembourg. Kisha hiyo orodha yabadilika kuwa: Luxembourg, Marekani, Uswisi, Muungano wa Falme za Kiarabu, Qatar, Hong Kong, Japani, Ujerumani, Singapore, na Kanada.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki