Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 3/8 kur. 12-14
  • Kupatwa kwa Jua na Ule Uvutio wa Astronomia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kupatwa kwa Jua na Ule Uvutio wa Astronomia
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Lile Fumbo la Kupatwa Kuzito
  • Wayesuiti Walivyotumia Kupatwa kwa Jua
  • Astronomia Katika Biblia
  • Giza Lililotokea Adhuhuri
    Amkeni!—2002
  • “Usiku Ulipoingia Mchana”
    Amkeni!—2008
  • Hali ya Pekee ya Jua Letu
    Amkeni!—2001
  • “Hakika Mtu Huyu Alikuwa Mwana wa Mungu”
    Yesu—Njia, Kweli, na Uzima
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 3/8 kur. 12-14

Kupatwa kwa Jua na Ule Uvutio wa Astronomia

MEI 10, 1994, ilikuwa siku isiyo na kifani, kwa baadhi ya watu katika Amerika Kaskazini. Kilikuwa kipindi cha mwezi kulipata jua kwa sehemu. Kwa saa chache, mamilioni waligutushwa na ule uvutio wa sayansi ya astronomia. Lakini kupatwa ni nini hasa?

Kupatwa hutukia wakati kunakuwa na “kuzuiwa kwa sehemu au kuzima, kwa gimba moja la kianga kunakofanywa na lingine, kukitegemea mahali alipo mtazamaji.” (The American Heritage Dictionary of the English Language) Kupatwa kwa jua au mwezi kwaweza kutukia wakati dunia, jua, na mwezi zimo karibu katika mstari mmoja. Hivyo basi, ikiwa kuna kupatwa kwa jua au mwezi hutegemea ni gimba lipi la kianga limezuiliwa. Nyakati nyingine dunia humwesha kivuli chayo kwenye mwezi, ikitokeza kupatwa kwa mwezi. Kwa upande ule mwingine, katika Mei ya mwaka jana, mwezi ulimwesha kivuli chawo kwenye dunia, katika ukanda mwembamba uliotofautiana kuanzia kilometa 230 hadi 310 kwa upana. Mwezi ulipokuwa ukipita polepole katikati ya dunia na jua, ulikuwa karibu kulizuia kabisa jua. Kijia cha kivuli hicho kilielekea kuvuka Bahari ya Pasifiki na kisha Amerika Kaskazini kutoka kusini-magharibi hadi kaskazini-mashariki. Mwezi ulionekana kupita polepole mbele ya jua. Kwa kweli, kivuli hicho kilisafiri kuvuka dunia kwa mwendo uliokadiriwa kuwa kilometa 3,200 kwa saa.

Mbinu za aina zote zilitumiwa ili kutazama kupatwa huko bila kuharibiwa macho. Wengine walitazama kupitia kisetiri-macho cha mlehemishaji. Wengine walitumia vioo vyenye rangi. Hata hivyo wengine walifanyiza picha ya kupatwa huko kupitia kwa karatasi kupitia kwa kitoboleo. Mpiga-picha mmoja alimfanya mtu ashikilie sinia lililotobolewa vishimo, na mwangaza ulipopitia vishimoni, ulitokeza taswira pacha-pacha ya kupatwa kwenye mchanga. Matokeo yanayofanana na hiyo yalionekana mwangaza ulipopita kupitia majani ya miti. Mbinu nyingine ilikuwa kupitishia mwanga huo kwenye darubini ya macho mawili ili kupata taswira marudufu kwenye uso wenye giza.

Kupatwa kwingi kufikia mipato ya jua tano na kufikia mipato ya mwezi tatu yaweza kutukia kwa mwaka mmoja. “Angalau kupatwa kwa jua kwa aina fulani lazima kutukie mara mbili kila mwaka,” lasema The International Encyclopedia of Astronomy. Hata hivyo, kila kumoja kwaonekana kutoka mahali tofauti tofauti. Hivyo basi yeyote aliye katika ukanda wa Marekani aliyekosa kuona kupatwa kwa 1994 itambidi kungojea hadi mwaka wa 2012 kwa ajili ya fursa nyingine au asafiri hadi Peru, Brazili, au Siberia ili aone kupatwa kwa mapema.a

Lile Fumbo la Kupatwa Kuzito

Kupatwa kuzito kwa jua, mwezi uzuiapo jua kabisa, kulitokeza hofu na fadhaiko katika karne zilizopita. Kwa nini ilikuwa hivyo? The International Encyclopedia of Astronomy iliandika hivi: “Lile fumbo la kupatwa kuzito husitawi kwa sababu kule kuanza hakutoi onyo la tukio linalokaribia kutokea kwani Mwezi hauwezi kuonekana ukikaribia Jua.” Tamasha hiyo hutia ndani maonyesho kama haya: “Anga linakuwa jeusi zaidi, mara nyingi kukiwa na utusitusi wa kijani ambao hauwezi kuelezeka usiofanana kabisa na weusi usababishwao na mawingu. . . . Wakati wa sekunde za mwisho kufichwa kwa sehemu kwa jua mwanga hupotea mara, kwa kuhisiwa kunakuwa na baridi zaidi, ndege hutulia viotani, petali za maua hujifunga, na upepo huelekea kupungua. . . . Giza hukumba maeneo ya mashambani.”

Katika kitabu chake The Story of Eclipses, George Chambers aripoti juu ya “mojapo mipato iliyojulikana sana ya nyakati za kale . . . , ilionekana ikiwa kupatwa kuzito katika Scotland,” kulikotukia Agosti 2, 1133. William wa Malmesbury aliandika hivi: “Jua siku hiyo kwenye saa 6 lilificha uso walo wenye utukufu, . . . katika kiza chenye kutisha, kikihofisha mioyo ya wanadamu kwa kupatwa.” Anglo-Saxon Chronicle ya kale yasema kwamba “wanadamu walipapishwa sana na kutishwa.”

Chambers pia alirekodi fafanuzi la wazi la kupatwa fulani kwa mwezi kulikotukia katika Septemba 2, 1830, kulikoripotiwa na wasafiri wawili katika Afrika: “Mwezi ulipokuwa wazuiliwa polepole, hofu ilishinda kila mmoja. Kadiri kupatwa kulivyoongezeka walizidi kutishika. Wote walikimbia kwa taabu ili kumwarifu maliki wao juu ya tukio hilo, kwani hakukuwa na wingu lolote la kusababisha kivuli kizito hivyo, nao hawangeweza kufahamu asili au maana ya kupatwa huko.”

Katika nyakati za karibuni zaidi, uchunguzi wa astronomia umeondosha hofu ya binadamu kuhusu kupatwa kwa jua—twajua kwamba jua litatokea tena.

Wayesuiti Walivyotumia Kupatwa kwa Jua

Huko nyuma katika 1629, wamishonari Wayesuiti katika China waliweza kupata kibali cha maliki kwa kutumia kupatwa kwa jua. Walifanyaje hivyo?

Wayesuiti walikuwa wametambua kwamba “kalenda ya Kichina iliyotegemea mwezi ilikuwa na kosa, kama ilivyokuwa kwa karne nyingi. Waastronomia wa Maliki kwa kurudia-rudia walikuwa wamekosea katika kutabiri kupatwa kwa jua . . . Fursa kubwa iliibuka kwa Wayesuiti wakati wa kupatwa kulipokuwa kukitazamiwa kwenye asubuhi ya Juni 21, 1629. Waastronomia wa Maliki walitabiri kwamba kupatwa huko kungetukia saa 4:30 na kungedumu kwa saa mbili. Wayesuiti walitabiri kwamba kupatwa hakungetokea hadi saa 5:30 na kungedumu kwa dakika mbili tu.” Ni nini kilitokea?

“Katika siku yenye kutazamisha sana, saa 4:30 ilifika na kupita, jua liliangaza kikamili. Waastronomia wa Maliki walikosea, lakini je, Wayesuiti walikuwa kweli? Kisha, mara ilipofika saa 5:30, kupatwa kukaanza na kukadumu kwa muda mfupi wa dakika mbili, kama Wayesuiti walivyokuwa wametabiri. Maliki akawa na uhakika kamili juu yao.”—The Discoverers, na Daniel J. Boorstin.

Astronomia Katika Biblia

Habari ya Kiastronomia yapatikana hata katika Biblia. Thurea kadhaa zimetajwa katika kitabu cha Ayubu. Zaidi ya yote, Yehova aliwaalika watumishi wake ili kuzichunguza mbingu, si kwa ajili ya uchunguzi wa unajimu au ibada nyingine bandia, lakini ili kuthamini uadhama wake wa uumbaji. Isaya alipuliziwa kusema hivi: “Inueni macho yenu juu, mkaone; ni nani aliyeziumba hizi; aletaye nje jeshi lao kwa hesabu; aziita zote kwa majina; kwa ukuu wa uweza wake, na kwa kuwa yeye ni hodari kwa nguvu zake; hapana moja isiyokuwapo mahali pake.”—Isaya 40:26.

Ayubu alikubali ukuu wa Muumba aliposema hivi kumhusu: “Yeye afanyaye hizo nyota za Dubu, na Orioni, na hicho Kilimia [yawezekana ikawa thurea ya Ng’ombe], na makundi ya nyota ya kusini [yaeleweka kuwa magimba ya Kizio cha Kusini].”—Ayubu 9:7-9.

Uchunguzi wa astronomia utakuwa wenye usisimuzi ulioje wakati Yehova atawapa wanadamu watiifu uhai udumuo milele! Kisha fumbo la ulimwengu-wote-mzima litafunuliwa hatua kwa hatua kadiri tujapo kufahamu makusudi ya Mungu kuhusu ulimwengu-wote-mzima uliotanuka. Basi, tutaweza kurudisha mwangwi wa maneno ya Daudi tukiwa na hisia hata zaidi: “Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako, mwezi na nyota ulizoziratibisha; mtu ni kitu gani hata umkumbuke, na binadamu hata umwangalie?”—Zaburi 8:3, 4.

[Maelezo ya Chini]

a Kulikuwa na kupatwa kuzito kwa jua Novemba 3, 1994, kulikoonekana kuvuka sehemu za Amerika Kusini.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 12]

Picha kwa hisani ya NASA/Finley-Holiday Film Corporation

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki