Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 3/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • “Jiendesheni kwa Namna Inayozistahili Habari Njema”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kusitawisha Adabu za Kikristo Katika Ulimwengu Usio na Adabu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1989
  • Kuwa na Adabu Nzuri Ni Sifa ya Watu wa Mungu
    Huduma Yetu ya Ufalme—2001
  • Je, Ni Muhimu Kuwatendea Wengine kwa Adabu?
    Vijana Huuliza
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 3/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Adabu Mbaya Kwa muda mrefu kadiri niwezavyo kukumbuka, nilikuwa nimeonyesha adabu mbaya. Kulikuwa na nyakati ambapo hata nilihisi fahari kutosema maneno ya hisani na ufikirio, kama vile “Asante,” “Tafadhali nisamehe,” na “Nasikitika.” Halafu nikasoma makala “Kuzorota kwa Adabu” na sehemu za Biblia zilizonukuliwa ndani yayo. (Julai 22, 1994) Nilijifunza kuwa nyakati zote Mungu ni mwenye adabu anaposhughulika na wale wa hali ya chini, mara nyingi akiongezea “tafadhali” kwenye maombi yake. Nilishangaa sana kuona hilo katika Biblia. Imenihamasisha kujaribu kumwiga Mungu. Asante nyingi sana ziwaendee.

M. E. J., Nigeria

Nilithamini sana makala hiyo. Inayohusianishwa kwa ukaribu zaidi na adabu ni heshima kwa haki na mali za wengine. Nyakati fulani unapoalika marafiki nyumbani kwako, watoto wao huwa hawajali kufanya lolote watakalo—kwenda ndani ya vyumba tofauti, kuchunguza-chunguza kwenye vitoto vya meza na friji, na kadhalika.

G. W., Marekani

Kila sentensi katika makala hiyo ilikuwa yenye kufaa. Ilikuwa tu nilichohitaji kwa kufunza wavulana wangu wawili matineja. Nilijifunza kwamba kulikuwa na maelezo mengi ya kina kuhusu adabu ambayo sijafunza watoto wangu. Sasa najua maelezo haya ya kina yaliyo mazuri na jinsi ya kuyatumia.

P. H., Marekani

Njia za Usafiri wa Chini ya Ardhi za Moscow Hivi karibuni nilisoma “Majumba ya Kifalme ya Moscow Yenye Kumetameta Chini ya Ardhi.” (Juni 22, 1994) Nyakati zote nimetamani kusafiri ng’ambo, na naona kwamba kusoma makala kama hizo kunanifanya nihisi kama kwamba nilikuwa hapo.

J. H., New Zealand

Nilizuru Moscow nilipokuwa nikihudhuria mkusanyiko wa hivi karibuni wa Mashahidi wa Yehova. Nilitumia wakati mwingi nikisafiri katika Metro. Sikutambua wakati huo kuwa nilikuwa nikiona moja ya njia za usafiri wa chini ya ardhi zenye umaridadi na zilizo bora zaidi ulimwenguni. Kwa hiyo niliifurahia makala hiyo kwelikweli.

P. M., Finland

Walengaji Shabaha? Katika makala “Maoni Yangu Nikiwa Mwanahistoria wa Kijeshi,” mwandishi aelezea kuingia Paris kufuatia kukombolewa kwalo mwishoni mwa Vita ya Ulimwengu 2. (Aprili 22, 1993) Anadai kuwa alifyatuliwa risasi na walengaji shabaha Wajerumani na kuwa aliacha gari lake la aina ya jeep mara kadhaa ili kutafuta mahali pa kujikinga—na kwamba hilo lilitukia katika barabara iliyo mashuhuri zaidi katika Paris! Paris ‘halikukombolewa’ kamwe bali lilisalimu amri bila pigano likiwa chini ya kamanda wa Ujerumani Dietrich von Choltitz, ambaye alitenda kinyume cha maagizo.

A. W., Italia

Mwandikaji alikuwa akisimulia ono lake mwenyewe la kibinafsi, ukumbuko ambao umehakikishwa na mashahidi wengine waliojionea wenyewe na wanahistoria. Kwa kielelezo, kitabu “Liberation,” kilichoandikwa na mwanahistoria wa kijeshi Martin Blumenson, chakubali kwamba ingawaje von Choltitz alikiuka maagizo ya Hitler ya kuchoma Paris kabisa, pigano kali lilitokea kati ya majeshi ya Ujerumani na vikosi vilivyokuwa vikivamia vya Ufaransa na Marekani katika siku zile kabla asalimu amri. Kwa habari ya pigano kwenye Champs Élysées—“barabara iliyo mashuhuri zaidi katika Paris”—hilo pia lahakikishwa na wanahistoria wengine. Ona “Six Armies in Normandy—From D-Day to the Liberation of Paris,” kilichoandikwa na John Keegan.—Mhariri.

Bishano la Kitiba Nina umri wa miaka 12. Nilisoma makala “Wala Wafanya-Mizungu Wala Miungu.” (Mei 8, 1994) Nilifurahi kuona Mkristo aliye mchanga kweli kama mimi akikabili kijasiri madaktari na madaktari-wapasuaji wa hospitali na ‘kujiepusha na damu.’—Matendo 15:20.

P. M. H., Marekani

Nina umri wa miaka 19. Jinsi imani yangu imeimarishwa kwa kusoma ono la Mercy Uwasi! Lilinitahadharisha juu ya uhakika wa kwamba uaminifu-mshikamanifu kwa Yehova hautegemei umri wa mtu bali upendo wa mtu wenye kina kumwelekea. Hili limenifanya niazimie zaidi ya wakati mwingineo wote kudumisha uaminifu-mshikamanifu wangu kwa Yehova.

S. M., Afrika Kusini

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki