Seminari za Kuboresha Mahusiano Kati ya Madaktari na Mashahidi wa Yehova
WAKRISTO wakatazwa na sheria ya Mungu kula damu kwa njia yoyote. (Matendo 15:28, 29) Utii kwa sheria hiyo nyakati fulani umeongoza kwenye kueleweka vibaya ambako kumetokeza kunyimwa kwa Wakristo utunzi wa kitiba unaopatikana au mwingineo wenye matokeo kwa ajili ya matatizo yao ya kiafya.
Ili kutoa uelewevu mzuri zaidi na kusaidia madaktari kuandaa utibabu bila kutumia damu, Mashahidi wa Yehova wametokeza huduma ya mahusiano wenye kutoa msaada. Baraza Linaloongoza la Mashahidi wa Yehova limeanzisha Huduma za Habari za Kihospitali (HHK) katika Brooklyn, New York, ili kuzoeza wazee Mashahidi walioteuliwa wafanye kazi kwenye Halmashauri za Uhusiano na Hospitali (HUH). Utafiti wa kitiba umefanywa na matokeo kutolewa katika seminari kwa ajili ya HUH. Na hatimaye, habari hii hutolewa kwa madaktari na vitovu vya utunzi wa afya. Pia, uwasilianaji na madaktari wengine wazoefu waweza kupangwa katika jitihada ya kuepuka mapingamizi.
Je, programu hii imekuwa yenye kufaulu? Je, habari ambayo imetolewa imekuwa yenye msaada kikweli? Madaktari wamekuwa na itikio gani kwayo? Maoni yafuatayo yaliyoripotiwa na daktari wa kitiba aliyehudhuria seminari ya karibuni zaidi ya HUH ni yenye kuelimisha na kutoa uhakikisho.
“Natumaini mtapata maoni haya yakiwa wazi na yenye kusaidia.
“Kwanza kabisa, acheni niwaambie kwamba lilikuwa pendeleo kuombwa kuhudhuria Seminari ya pili ya Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali iliyotolewa na wafanya-kazi wa Huduma za Habari za Kihospitali waliokuja kutoka kwenye makao makuu ya Mashahidi wa Yehova katika New York. Matarajio yangu kwa mkutano huu hayakutimizwa tu bali yalitimizwa kwa kuzidi mno. Maelezo ya ufunguzi ya mwenyekiti yalianzisha jambo kuu la kuzungumzwa katika vipindi hivyo vya siku mbili. Alikazia kwamba HUH si tu mpango wa kuitikia mahitaji ya Mashahidi wanaougua wakati wa kukaa kwao hospitalini. Halmashauri hiyo huandaa fursa ya kipekee ya kufunua wazi ngano nyingi zinazoaminiwa na watu wa kawaida na madaktari, wakuu wa hospitali, na wafanya-kazi wengine wa hospitali kuhusu Mashahidi.
“Inashangaza kwa wengi wa watu hawa kujua kwamba Mashahidi wa Yehova hawako kama Wakristo Wanasayansi katika itikadi zao za kidini. Mashahidi hawajizoezi ‘haki ya kufa’ au kujaribu kujiweka katika hali ya ufia-imani. Wala suala la damu si neno la amri la kitengenezo bali itikadi ya kibinafsi yenye kuhisiwa moyoni. Mafunuo kama hayo yanakazia makusudi ya kielimu ya HUH. Ndiyo, kwa kupendeza kama iwezavyo kuonekana, hata madaktari waweza kuelimika na wana mengi ya kujifunza kuhusu utibabu mwingineo usiotumia damu. Ninaendelea kushangazwa na mweneo na kina cha utafiti unaoandaliwa na mpango huu, mwingi wa huo ukiwa mpya kwangu. Na kazi za kielimu za HUH hazikomei hapo. Huendelea hadi kwa wakuu wa hospitali, kwa huduma za kijamii, na hata kwa maofisa wa kisheria na wa kihukumu.
“Halmashauri hizi hujitahidi kiajabu katika kutafuta, kuwasiliana na kupata msaada wa madaktari ambao hukubali itikadi za Mashahidi. Bila shaka, halmashauri hizi huenda mbali zaidi ya jumuiya ya madaktari, kwa kuwa HUH hujenga uhusiano na hospitali, wafanya-kazi wa utunzaji wa afya, mawakili, na vilevile mahakimu. Labda ujumbe wenye kutokeza zaidi wa kutolewa ni kwamba Mashahidi wa Yehova ni watu wenye kukubali sababu, si washupavu, na wanaomba matibabu mengine yanayokubalika badala ya damu. . . . Kuna hatari kubwa katika utumizi wa damu, na HUH kwa hakika hutimiza kazi ya kufunua hatari hizi na kukazia kwa jumuiya ya kitiba hatari ziwezazo kupatikana za damu na vifanyiza damu.
“Ninazidi kushangazwa na habari iliyoandaliwa kwa HUH na Huduma za Habari za Kihospitali na Watch Tower Society. Lakini kama vile fundi yeyote awezavyo kuhakikisha, karibu kila kazi yaweza kutimizwa ikiwa vifaa vya kazi vifaavyo vyatolewa. . . . Ilipendeza sana kusikia kuhusu mipango ambayo yatumika sasa ili kuitikia haraka na kwa matokeo kwa karibu dharura zozote za kitiba. Kila mshiriki wa HUH huzoezwa kupata habari inayohitajika ya uchunguzi wa tarakimu, ili kuchanganua haraka mtazamo wa madaktari na hospitali, na kuchanganua kwa usahihi kiwango cha dharura na uwezekano wa hatari ya hatua ya kisheria inayoweza kuchukuliwa na hospitali kama vile amri ya korti kwa ajili ya utiaji-damu.
“Tulichunguza njia za kurekebisha mahitaji na matakwa ya wagonjwa Mashahidi, jinsi ya kushughulika na wenzi wasioamini, hata jinsi ya kulikiza madaktari na kuhamisha mgonjwa kwenye mahali pengine pa kitiba penye kukubali zaidi mahitaji ya Mashahidi. Mwingiliano wa HUH na vyombo vya habari ulikaziwa, na miongozo ikatolewa, mara nyingine ikikazia mkazio-fikira wa msingi kwamba Mashahidi hawakatai utunzaji wote wa kitiba, damu tu. Hili laweza kulinganishwa kwa kukadiria na ukataaji wa utoaji-mimba wa Mkatoliki mchaji lakini si upasuaji wote.
“Washiriki wa halmashauri ya uhusiano wamezoezwa kushughulikia maswali ya kawaida yanayokuzwa na madaktari pamoja na hospitali, hata pindi kwa pindi na Mashahidi wenyewe. Hii yaweza kutia ndani masuala kama vile ukubali wa imunoglobulini au albumini, utumizi wa ustadi wa kupata vijidutu kutoka kwenye damu kwa kutumia halijoto ya chini kabisa au ufundi wa kitiba kama vile mchanganyo wa chembe-damu, mzunguko wa damu wa nje ya mwili, kile kiokoa-chembe, au hemodayalisisi.
“Nilifurahia mazungumzo yenye kupendeza sana ya mafikirio ya kisheria yanayohusishwa na kuelewa na kutumia sheria katika kutetea Mashahidi na itikadi zao za kidini. Maamuzi ya kihukumu yanayofanya msingi wa kutetea haki za Mashahidi kwa azimio-binafsi ndio utegemezo kwa ajili ya mazungumzo yenye kupendeza sana. Kwa wengi, kazi ya Halmashauri ya Uhusiano na Hospitali huenda ikaonekana kuwa ya kupita kiasi, hata isiyohitajika; lakini kwa kweli, mfumo huu wa utumishi wa kutegemeza ni wa maana. Kila siku mimi huona wagonjwa Mashahidi ambao hawafahamu mazingira ya hospitali na labda hawajui juu ya matibabu mengine mengi ya kitiba. Zaidi ya hilo, ni wachache wawezao kufahamu sifa ya ufahamu ya madaktari wenye nia ya kushirikiana wajulikanao na halmashauri au na haki za kisheria hususa na madaraka ambayo kila mmoja wetu anayo na anayokabiliana nayo katika kutafuta ushughulikio wa kitiba usiotumia damu.
“Acheni niache kwa kitambo habari niliyokuwa nikisema ili nisifu jitihada za HHK. Nikiwa mtaalamu wa magonjwa ya moyo nakuta kwamba kuna wakati mchache wa kusoma majarida hayo mengi yafaayo hasa kwa kazi yangu ndogo bila kutaja mweneo mkubwa wa tiba ya magonjwa yatibiwayo bila upasuaji. Ingekuwa kazi isiyowezekana kutafuta katika rundo kubwa hilo la vitabu vya kitiba kwa ajili ya marejezo ambayo yangeweza kutaja kihususa matatuzi hususa ya matatizo yanayokabiliwa katika kushughulikia wagonjwa wangu wasiotumia damu. Kwa mara nyingine tena Sosaiti hiyo yanisaidia kwa kunipa sumaku ili kutoa sindano ya utafiti ufaao katika rundo hilo la nyasi kavu la kimethali la makala za jarida.
“Habari zilizofanywa upya kutoka Brooklyn zenye kuendelea hutumika katika kuniweka katika hali ya kujua habari za karibuni zaidi za maendeleo ambayo yaweza kuathiri kazi yangu. Habari hizi ni kamili na zenye kutia nguvu kuliko utumishi wowote wa kompyuta wa pitio-jarida ambao nimezoelea. Bila shaka, yapasa kuwa hivyo, kwa kufikiria kilicho hatarini.”—Na Dakt. Stephen E. Pope, mtaalamu wa magonjwa ya moyo katika eneo la Ghuba ya San Francisco, katika California, Marekani.
[Sanduku katika ukurasa wa 20]
• Katika Marekani, yapata madaktari 18,000 wapendezwa kushirikiana na Mashahidi wa Yehova katika utunzaji wa kitiba usiotumia damu. Idadi ya ulimwenguni pote ni 50,000.
• Katika Marekani, kuna vitovu vya kitiba 45 ambapo dawa zisizo na damu na programu za upasuaji zapatikana. Idadi ya ulimwenguni pote ni 80.