Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 4/22 uku. 31
  • “Angamizo Kubwa la Kifedha”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Angamizo Kubwa la Kifedha”
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Jitihada Inayoendelea ya Kutafuta Suluhisho
    Amkeni!—2000
  • Kwa Nini Wayahudi Wengi Waliuawa? Kwa Nini Mungu Hakuzuia?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
  • Mashahidi wa Yehova na Yale Maangamizi Makubwa ya Wayahudi—Biblia Inasema Nini?
    Habari Zaidi
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2014
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 4/22 uku. 31

“Angamizo Kubwa la Kifedha”

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA NIGERIA

KULINGANA na ripoti ya UNICEF (Hazina ya Watoto ya Umoja wa Mataifa), Afrika iliyo kusini mwa Sahara imekumbwa na “angamizo kubwa la kifedha.” Karibu nusu ya idadi ya watu—yapata watu milioni 220—huishi katika umaskini hohehahe, wakishindwa kushughulikia mahitaji yao ya lazima zaidi. Mwananchi wa wastani yuko asilimia 20 maskini zaidi ya alivyokuwa mwongo uliopita.

“Katika elimu,” yasema ripoti hiyo, “miaka ya 1980 yaweza tu kuelezwa kuwa mwongo uliopotea.” Utumizi kwa mwanafunzi ulipungua kwa thuluthi moja, na uandikishaji katika shule za msingi ukashuka kutoka asilimia 79 hadi asilimia 67. Huduma za utunzi wa afya zafifia pia katika nchi nyingi za Afrika, kukiwa na kliniki zinazofunga kwa sababu ya ukosefu wa wafanyakazi na dawa.

Ripoti hiyo yaorodhesha visababishi kadhaa vya matatizo ya kiuchumi, kutia ndani matumizi ya kijeshi, biashara inayopungua, na madeni makubwa, ambayo wastadi wasema hayawezi kulipwa kamwe. “Afrika haiwezi kupata nafuu,” yasema ripoti ya UNICEF, “bila jitihada ya kimataifa kwa kiwango kikubwa ambacho bado hakijapata kuwazika.”

Je, hili laelekea kutukia? Biblia kwa uhalisi yataarifu: “Msiwatumainie wakuu, wala binadamu ambaye hakuna wokovu kwake.” (Zaburi 146:3) Suluhisho kwa matatizo ya Afrika yasiyoweza kuondoka kwa urahisi halitegemei serikali za wanadamu. Ni Ufalme wa Mungu utakaoleta kitulizo chenye kudumu—si kwa Afrika tu bali kwa ulimwengu wote.—Mathayo 6:10.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

WHO/OXFAM

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki