Je, Mchezo Huu Unakufaa?
“IKITEGEMEA mtazamo wa mtu, Doom ni ama mchezo wenye milipuo inayofanya moyo kupiga kwa haraka unaoweka michezo ya kompyuta katika kiwango kipya cha utata wa kiufundi ama ufurahiaji wa jeuri ipitayo kiasi ambayo huweka michezo ya kompyuta katika kiwango cha adili kilichoshuka mno zaidi ya wakati mwingineo wote.” Ndivyo alivyoandika Peter Lewis katika “Personal Computers” safu ya The New York Times. Bila shaka, michezo mingi ya kompyuta ni mficho wenye kutilika shaka wa jeuri, mauaji yasiyo na huruma, au hata pornogrfia ya wazi hadharani. Mwongezo wa karibuni—Doom 2—watarajiwa kuwa kiuzwaji bora zaidi hata ingawa wagharimu dola 69.95. Je, mchezo wa aina hii wafaa kwa Wakristo wapenda amani? Maelezo yanayoendelea ya Lewis huenda yakakusaidia kuamua.
“Mchezaji anajifanya kwamba yeye ni Mwanamaji ambaye yuko kwenye moja ya miezi inayohusianishwa na sayari Mihiri wakati aksidenti ya kiwanda inapofungua ukumbi kuelekea Helo. . . . Mwanamaji alazimika kwenda kupitia kumbi zenye vipengee na matatanisho, . . . akipiga makonde, kupiga risasi, kuchoma na kukata kwa msumeno-umeme mashetani na waliokuwa binadamu hapo mbeleni kwa kuendelea. . . .
“Ukuzi katika Doom 2 hufanyiwa muhtasari hivi: Mashetani zaidi, kumbi zaidi za ogofyo la nafasi nyembamba, silaha zaidi na uchu wa damu zaidi.”
Likitoa maelezo juu ya mkusanyiko wa kompyuta katika Las Vegas, Nevada, The New York Times lilitaarifu hivi: “Shani ya wazi zaidi ya mwaka huu ilikuwa pornografia katika sehemu nyingi za vyombo vya habari. . . . Ilivutia mojapo umati mkubwa zaidi ya wowote wa mkutano huo.”
Mwandikaji wa Biblia Yakobo alisema: “Hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema.” (Yakobo 3:17) Wazazi, je, mmechunguza michezo ya kompyuta ya nyumbani kwenu wanayotumia watoto wenu kwa wakati huu? Twahitaji kusema zaidi?