Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 5/22 kur. 14-16
  • Ukuzaji Samaki—Samaki Wakiwa “Mifugo”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ukuzaji Samaki—Samaki Wakiwa “Mifugo”
  • Amkeni!—1995
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka Ng’ofu Hadi Samaki kwa Ajili ya Soko
  • Mafumbo ya Kibiolojia na Utofautiano
  • Uchafuzi na Mashambulizi ya Mwani
  • Kushughulikia Maradhi
  • Utendaji Wenye Ukuzi
  • Unapokuwa Mgonjwa kwa Kula Samaki
    Amkeni!—2006
  • Uwezo wa Samaki wa Kuogelea Katika Vikundi
    Amkeni!—2012
  • Mbinu za Ndege za Kuvua Samaki
    Amkeni!—2011
  • Samaki wa Mtakatifu Petro
    Amkeni!—2002
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 5/22 kur. 14-16

Ukuzaji Samaki—Samaki Wakiwa “Mifugo”

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA NORWAY

MAELFU ya miaka iliyopita, Wachina na Wamisri walitengeneza vidimbwi vya maji matamu ambamo waliweka na labda kulisha samaki walio hai. Siku hizi kukuza samaki kumekuja kuwa utendaji. Huitwa ukuzaji samaki. Webster’s Ninth New Collegiate Dictionary huufafanua kuwa “ulimaji wa mazao ya asili ya maji.” Hili hutia ndani ufanyizaji wa hali zifaazo za ukuzi na uzalishaji na ukuzaji wa wanyama na mimea ya majini katika maji ya chumvi au maji matamu.

Kufikia wakati huu, ukuzaji mkubwa na uzalishaji wa samaki ni namna za kawaida zaidi za ukuzaji samaki. Katika nchi nyingi, hasa mahali ambapo halijoto za maji matamu ziko juu kiwango fulani, ukuzaji samaki wa maji matamu katika mapipa makubwa na vidimbwi umeenea sana. Mataifa mengine yamekazia fikira zaidi kwenye kutumia sehemu zao za baharini. Norway ni kielelezo cha ukuzaji katika sehemu za baharini. Ikiwa na moja ya fuo ndefu zaidi ulimwenguni, halijoto zifaazo za bahari na maji safi kwa kulinganishwa, nchi hii ina faida ya kiasili katika ukuzaji samaki katika maji ya bahari. Norway imekuwa nchi yenye kutokeza namna mpya za mambo, hasa katika kufuga salmoni wa Atlantiki na tirauti katika bahari.

Kutoka Ng’ofu Hadi Samaki kwa Ajili ya Soko

Utokezaji huanza kwenye kianguaji wakati wa vuli. Samaki jike “hupapaswa” ili kutoa ng’ofu yao, na ng’ofu hiyo hutungishwa kwa shahawa kutoka kwa dume walioteuliwa. Ng’ofu iliyotungishwa hutumia kipindi cha vuli chini ya uangalizi wenye uangalifu katika kianguaji, na uanguzi hutokea baada ya miezi sita. Kwa majuma machache ya kwanza, samaki mchanga hulishwa kutokana na kifuko cha kiiniyai kilichoko kwenye tumbo lake; halafu ulishaji wa kwanza wenye uangalifu huanza. Katika hali za kutofugwa, salmoni mchanga hutumia miaka miwili hadi mitatu katika mto ambao alianguliwa, kabla ya kuhama hadi kwenye bahari yenye lishe zaidi ili kupata chakula. Katika kianguaji samaki mchanga hupata ukuzi na kuwa simolti (samaki salmoni aliye tayari kuhama) katika mwaka mmoja na nusu.

Halafu samaki hao huhamishwa kutoka maji matamu hadi kwenye maji ya chumvi. Kwa kawaida huwekwa katika viweko, mazizi au vizimba vinavyoelea, baharini. Baada ya mwaka mmoja au miwili katika shamba la baharini, salmoni wamefikia saizi ifaayo na wanachukuliwa kwa ajili ya matayarisho ya kuuzwa. Yote hayo yasikika kuwa sahili mno, rahisi mno. Hata hivyo, kuwa na samaki wakiwa “mifugo” hutokeza magumu kadhaa.a

Mafumbo ya Kibiolojia na Utofautiano

Wakuzaji wa mapema wa samaki walianza bila kuwa na uzoefu wowote na iliwalazimu kupata ujuzi mwingi wa uzalishaji, mapendezi tofauti ya chakula, na silika za spishi tofauti. Kulionekana kuwa na idadi isiyo na mwisho ya mafumbo ya kibiolojia yaliyokuwa hayajatatuliwa na mambo ambayo yangeenda mrama. Je, ingewezekana wakati wowote kutosheleza mahitaji yenye kutofautiana kwa kuendelea ya samaki wachanga na wakubwa kuhusu ubora wa maji, halijoto, chakula, na nuru?

Mengi ya matatizo haya yameshatatuliwa kitambo. Idadi kadhaa ya programu za utafiti hukazia fikira juu ya jinsi ukuzi na tabia za spishi mbalimbali ziwezavyo kudhibitiwa na hali kama mazoezi, kutumiwa kwa nuru, na kiwango kifaacho na ubora wa chakula.

Uchafuzi na Mashambulizi ya Mwani

Mazingira safi ni ya muhimu katika ukuzaji samaki. Kwa hivyo, mifumo ya kimazingira isiyosawazika na viwango vya uchafuzi hutokeza matatizo katika utendaji wa ukuzaji samaki. Samaki wasiofugwa ambao huvumbua sumu katika maji hujaribu kuepuka hatari hiyo. Samaki waliokuzwa katika mashamba ya baharini hawawezi, wakiwa wamezuiliwa katika mazizi. Kwa hiyo mimwagiko ya mafuta au mivujo ya kemikali zenye sumu yana uwezekano wa kuwa na madhara kwa mashamba ya samaki.

Watu wengine walipata mshtuko katika mwaka 1988 wakati kulikuwa na ukuzi wenye kupita kiasi wa planktoni ya mwani wenye sumu kwenye pwani ya kusini-magharibi mwa Sweden na kwenye fuo za kusini mwa Norway. Katika mahali pengi mno mwani uliua samaki na uhai mwingine baharini. Mashamba kadhaa ya samaki yalifanywa kuwa matupu, kwa sehemu sababu ikiwa mwani wenyewe na kwa sehemu sababu ikiwa kufanyiwa matayarisho ya ghafula ya kuuzwa. Lakini viweko vingi viliokolewa kutokana na kifo cha kimwani kwa kuwa wakuzaji wa samaki waliburuta mazizi kwa usalama wa horini. Wengine waliita msiba huu wa kimwani “aksidenti ya pwani ya kinyukilia ya Chernobyl,” na wastadi walidai kwamba uchafuzi uliozidi labda ulikuwa jambo lenye kuchangia katika kusababisha ukuzi wa kupita kiasi wa planktoni ya mwani wenye sumu.

Mazizi ya samaki baharini yako katika kila aina ya halihewa na hulazimika kustahimili barafu, bahari zilizochafuka, na dhoruba. Wakati kiweko kinapoharibiwa na samaki kutoroka, mkuzaji samaki hupoteza mali yenye thamani. Isitoshe, samaki waliotoroka wanaweza kueneza maradhi kwa samaki wasiofugwa, na hili limekuwa tatizo zito. Samaki waliotoroka pia watashindania chakula na maeneo ya kuzalia na samaki wasiofugwa, na kuna hofu kwamba hili laweza kuwa na matokeo hasi kwenye uzao wa mahali hapo.

Kwa hiyo kuna mwafaka kamili kwamba viweko vya baharini lazima vilindwe vyema ili kuepuka utorokaji. Maendeleo yamefanywa katika sehemu hii pia. Aquaculture in Norway lasema kwamba katika miaka ya majuzi “mengi [yamefanywa] kwa upande wa kutengeneza viweko vya ukuzaji samaki viwezavyo kustahimili halihewa mbaya.”

Kushughulikia Maradhi

Kila kitu kinachohitilafiana na asili ya samaki au kuwa kinyume cha mazingira yao ya kawaida husababisha mkazo, na hili huumiza mfumo wao wa kinga. Mchanganyiko wa mambo, kama vile samaki wengi katika sehemu moja, ulishaji mwingi mno, kukusanyika kwa mata ya kikaboni, na viwango vilivyoongezeka vya unamna wa pathojeni za samaki, umetokeza matatizo makubwa mno ya maradhi miongoni mwa samaki wafugwao zaidi ya samaki wasiofugwa. Hili limesababisha hasara kubwa sana kwa utendaji huo.

Kwa kweli, mengi ya maradhi ya samaki yaweza kutibiwa kwa kielelezo na, viuajisumu, lakini utumizi wa muda mrefu wa viuajisumu ni tisho kwa mazingira, kwa msingi sababu ikiwa kwamba huo hutokeza bakteria yenye kukinza, hiyo ikihitaji kutokezwa kwa dawa mpya. Dawa pia zaweza kudhoofisha, zikifanya iwe rahisi zaidi kwao kupatwa na maradhi mengine. Bila shaka, wafugaji samaki wametaka kuepuka kawaida hii isiyo nzuri.b

Ule msemo wa kale kwamba kuzuia ni bora kuliko kuponya hutumika pia katika ukuzaji samaki. Jitihada kubwa imetumiwa ili kupata ujuzi zaidi juu ya jinsi ya kutegemeza kinga za kiasili za samaki. Utafiti huu unaelekezwa kuelekea maeneo kama vile utaratibu wa ulishaji, mazingira ya ukuzaji na kawaida za ufanyaji kazi, na ustawishaji wa chanjo zenye matokeo na mbinu za uchanjaji. Kazi hii imeleta matokeo, na yaonekana kwamba utendaji wa ukuzaji samaki hudhibiti katika vita dhidi ya maradhi.

Utendaji Wenye Ukuzi

Ukuzaji samaki ni utendaji halisi wa kimkoa wa umuhimu mkubwa kwa makao kadhaa ya kipwani. Tangu utendaji wa ukuzaji samaki ulipoanzishwa, ukuzi wa ajabu umetokea. Katika 1990, utokezaji mazao wa ulimwenguni pote ulikuwa na thamani ya jumla ya zaidi ya dola bilioni 23. Norway hutoa zaidi ya nusu ya salmoni wa Atlantiki wafugwao ulimwenguni pote, ikipeleka nje salmoni kwa zaidi ya nchi 90 tufeni pote.

Ingawa salmoni wa Atlantiki amekuwa bidhaa kubwa kutoka ukuzaji wa baharini kufikia wakati huu, tayari kuna viwango vichache vya chewaulaya wafugwao na halibati kwenye soko. Utendaji wa ukuzaji samaki watamani kuwa mgavi mwenye kutegemeka wa samaki wa karibuni, walio bora wakati wote mwakani.

Kwa kusikitisha, binadamu mara nyingi wanajiruhusu kusukumwa na pupa, na hili limetokea katika utendaji wa ukuzaji samaki. Katika visa fulani, ufikirio wa kimazingira umekubali kushindwa na tamaa ya kufanya faida ya haraka. Wakuzaji samaki wenye kufikiri kama huko wahitaji kujua jinsi hali ya asili iwezavyo kuleta madhara; wanapaswa kutambua kwamba kutunza mazingira kuko katika upendezi wao wenyewe. Hivi karibuni au baadaye, sikuzote huthibitika kuwa hekima kusimamia rasilimali za dunia kulingana na kusudi la Muumba la mwanzoni—kwa upatano na hali ya asili na mifumo yayo yenye utata ya kimazingira.

[Maelezo ya Chini]

a Ikitegema habari katika broshua Aquaculture in Norway, iliyotangazwa na Shirika la Wafugaji wa Samaki wa Norway.

b Zikifikiria wateja mamlaka za Norway, zimeweka masharti magumu kwenye utumizi wa dawa. Wafugaji samaki wanaweza kupata dawa kupitia kwa Daktari wa mifugo tu, na samaki walio na dawa hutengwa ili kuhakikisha kwamba samaki wote hawana dawa kabla ya kuuzwa.

[Picha katika ukurasa wa 15]

Samaki huwekwa katika mazizi yaeleayo baharini

Samaki jike hupapaswa ili kutoa ng’ofu yao

Samaki wafikapo saizi ifaayo, huchukuliwa na kutayarishwa

[Hisani]

Picha: Vidar Vassvik/Norwegian Seafood Export Council

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki