Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g95 7/8 uku. 27
  • Onyo kwa Madereva-Wasinziaji

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Onyo kwa Madereva-Wasinziaji
  • Amkeni!—1995
  • Habari Zinazolingana
  • Aksidenti za Magari Je, U Salama?
    Amkeni!—2002
  • Jinsi ya Kuzuia Aksidenti za Barabarani
    Amkeni!—2011
  • Uchovu—Mtego Usiotambuliwa na Madereva wa Lori
    Amkeni!—1997
  • Jinsi ya Kuboresha Usingizi Wako
    Amkeni!—2003
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1995
g95 7/8 uku. 27

Onyo kwa Madereva-Wasinziaji

HUSABABISHA aksidenti zinazokadiriwa kuwa 600,000 na vifo 12,000 vya barabara kuu kila mwaka katika Marekani. Huo hulaumiwa kwa ajili ya asilimia 40 ya migongano yenye maafa katika miaka ya majuzi kwenye Barabara kuu ya New York State. Maangamizo haya yote yalisababishwa na kuendesha magari chini ya athari, si ya dawa za kulevya au alkoholi, bali chini ya athari ya usinziaji. Wataalamu fulani wanaamini kwamba hilo tatizo linasababishwa, si na matatizo ya kulala, kama vile apnea au insomnia, bali kwa usahili linasababishwa na mtindo-maisha wa 1990. “Wamarekani wamekuwa walionyimika usingizi zaidi ya miaka michache iliyopita,” asema Dakt. William Dement wa Kitovu cha Utafiti wa Usingizi cha Chuo Kikuu cha Stanford. Dave Willis, mkurugenzi mkuu wa American Automobile Association Foundation for Traffic Safety, asema hivi: “Watu wanajishughulisha sana bila kupata pumziko.”

Jambo lenye kusumbua sana ni uhakika wa kwamba madereva wengi wenye kusinzia wanaingia na kutoka usingizini bila kujua. “Microsleep,” kama wanavyouita wataalamu, waweza kudumu sekunde chache tu, lakini matokeo ya jumla yaweza kuwa yenye kuogofya. “Nilikumbuka nikipita kitokeo cha 17, halafu ishara za kitokeo cha 21,” aeleza dereva mmoja. “Ningefikiri, nilikuwa wapi katika vitokeo vilivyokuwa katikati? Unatambua ni muujiza kwamba hata ulifika mahali ulipokuwa ukienda.”

Njia bora zaidi ya kupambana na uchovu wa uendeshaji gari ni kusimama na kupumzika. Usingizi kidogo wa dakika 10 hadi 20 katika mahali salama waweza kuwa ndio jambo tu linalohitajika. Hata hivyo, ingekuwa vyema kuwa mwenye kuangalia mambo kihalisi unapopanga safari. Usijaribu kwenda umbali usiouweza. Pia, stahi saa yako ya ndani ya mwili kwa kuepuka uendeshaji mrefu sana wa usiku na kwa kupata pumziko jingi kabla ya kuanza safari. Zaidi ya yote, usidharau kamwe hatari ya kuendesha gari huku ukisinzia. Asema Mark Hammer wa New York’s Institute for Traffic Safety Management and Research: “[Ni] vibaya tu kama kunywa chupa tano na kuingia ndani ya gari.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki