Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 5/8 kur. 20-22
  • Je, Umepata Kujiuliza?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Umepata Kujiuliza?
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Majibu ya Biblia
  • Mfano wa Maria Unatufundisha Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Alipewa Neema na Yehova
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • “Tazama! Kijakazi wa Yehova!”
    Igeni Imani Yao
  • Alikabiliana na Upanga wa Majonzi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 5/8 kur. 20-22

Je, Umepata Kujiuliza?

BIBLIA husema nini hasa kuhusu Mariamu, mama ya Yesu? Waumini wengi katika Jumuiya ya Wakristo huamini kwa dhati lile fundisho kwamba Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu, na Roho Takatifu ni Mungu lakini kwamba wao si miungu watatu, bali watatu katika mmoja. Kwa neno jingine, Utatu. Kwa sehemu kubwa za Jumuiya ya Wakristo (Katoliki, Anglikana, na Othodoksi), fundisho hili kiakili liliongoza kwenye itikadi kwamba, Mariamu, mama ya Yesu, ni “Mama ya Mungu.” Je, ndivyo ilivyo kweli? Yesu alimwonaje mama yake? Wanafunzi walimwonaje? Ebu tuone jinsi inavyojibu Biblia:

1. Ni wakati gani Mariamu anatajwa kwa mara ya kwanza katika Biblia?—Mathayo 1:16.

2. Mariamu alikuwa wa dini gani wakati wa kuzaliwa kwa Yesu?—Luka 2:39, 41.

3. Je, Mariamu alitoa toleo kwa ajili ya dhambi zake?—Luka 2:21-24; linganisha Mambo ya Walawi 12:6, 8.

4. Je, Mariamu alikuwa bikira alipopata mimba ya Yesu? Kwa nini hilo lilikuwa muhimu?—Mathayo 1:22, 23, 25; Luka 1:34; Isaya 7:14; Waebrania 4:15.

5. Mariamu alipataje mimba?—Luka 1:26-38.

6. Mariamu aliitikiaje hali zake za kipekee?—Luka 1:46-55.

7. Mariamu alionyeshaje kwamba alikuwa mama mwenye kujali?—Luka 2:41-51.

8. Je, Mariamu alikuwa na watoto wengine baadaye?—Mathayo 13:55, 56; Marko 6:3; Luka 8:19-21; Yohana 2:12; 7:5; Matendo 1:14; 1 Wakorintho 9:5.

9. Twajuaje kwamba ndugu na dada za Yesu hawakuwa binamu zake hasa?—Linganisha Marko 6:3; Luka 14:12; na Wakolosai 4:10.

10. Je, Yesu alimwona Mariamu kuwa “Mama ya Mungu”?—Yohana 2:3, 4; 19:26.

11. Je, Mariamu alijiona kuwa “Mama ya Mungu”?—Luka 1:35; Yohana 2:4, 5.

12. Je, Yesu alimpa mama yake sifa nyingi au heshima yoyote ya kipekee?—Marko 3:31-35; Luka 11:27, 28; Yohana 19:26.

13. Mariamu alionaje fungu lake katika makusudi ya Yehova?—Luka 1:46-49.

14. Je, Mariamu ni mpatanishi wa kike kati ya Mungu na mwanadamu?—1 Timotheo 2:5.

15. Mariamu hutajwa katika vingapi vya vitabu vya Biblia 66?

16. Je, waandikaji Wakristo walimkweza Mariamu katika vitabu na barua zao?—Yohana 2:4; 2 Wakorintho 1:1, 2; 2 Petro 1:1.

17. Mariamu hutajwa kwa jina mara ngapi katika barua 21 zilizoandikwa na Paulo, Petro, Yakobo, Yohana, na Yuda?

18. Mariamu alikuwa na tumaini jipi akiwa mfuasi wa Yesu?—1 Petro 2:5; Ufunuo 14:1, 3.

19. Je, Mariamu ndiye mwanamke anayerejezewa kwenye Mwanzo 3:15 na Ufunuo 12:3-6?—Isaya 54:1, 5, 6; Wagalatia 4:26.

20. Ni ipi iliyo hali ya wakati huu ya Mariamu?—2 Timotheo 2:11, 12.

Majibu ya Biblia

1. “Yakobo akamzaa Yusufu mumewe Mariamu aliyemzaa YESU aitwaye Kristo.”—Mathayo 1:16.

2. “Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti. Basi, wazee [“wazazi,” NW] wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka.” (Luka 2:39, 41) Wakiwa Wayahudi, walifuata Sheria ya Musa.

3. “Zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, (kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana).” (Luka 2:22, 23) “Hizo siku za kutakaswa kwake zitakapotimia, kwa ajili ya mwana, au kwa ajili ya binti, ataleta mwana-kondoo wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa na kinda la njiwa, au hua, kuwa sadaka ya dhambi, awalete mlangoni pa hema ya kukutania, na kumpa kuhani. Kama mali yake huyo mwanamke haimfikilii mwana-kondoo, hapo ndipo atakapochukua hua wawili, au makinda mawili ya njiwa; mmoja kuwa sadaka ya kuteketezwa, na wa pili kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atakuwa safi.”—Mambo ya Walawi 12:6, 8.

4. “[Yusufu] asimjue [Mariamu] kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.” (Mathayo 1:25) “Mariamu akamwambia malaika, Litakuwaje neno hili, maana sijui mume?” (Luka 1:34) “Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.” (Isaya 7:14) “Hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.”—Waebrania 4:15.

5. “Malaika akajibu akamwambia, Roho Mtakatifu atakujilia juu yako, na nguvu zake Aliye juu zitakufunika kama kivuli; kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. . . . Hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.”—Luka 1:35, 37.

6. “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu . . . Mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu.”—Luka 1:46, 47, 49.

7. “Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu?”—Luka 2:48, 49.

8. “Huyu si mwana wa seremala? mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda? Na maumbu yake wote hawapo hapa petu?” (Mathayo 13:55, 56) “Akashuka mpaka Kapernaumu, yeye na mama yake na ndugu [Kigiriki, a·del·phoiʹ] zake na wanafunzi [Kigiriki, ma·the·taiʹ] wake; wakakaa huko siku si nyingi.”—Yohana 2:12.

9. Kuna maneno ya Kigiriki ya kutofautisha ndugu na binamu. “Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu [Kigiriki, a·del·phosʹ] yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? na maumbu [Kigiriki, a·del·phaiʹ] yake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.” (Marko 6:3) “Usiwaite . . . jamaa [Kigiriki, syg·ge·neisʹ] zako.” (Luka 14:12) “Marko binamu [Kigiriki, a·ne·psi·osʹ] ya Barnaba . . .” (Wakolosai 4:10, NW)—Ona The Kingdom Interlinear Translation of the Greek Scriptures.

10. “Yesu akamwambia: ‘Nina jambo gani na wewe, mwanamke? Saa yangu haijaja bado.’” “Yesu, kwa kuona mama yake na mwanafunzi ambaye yeye alimpenda wamesimama kando, akamwambia mama yake: ‘Mwanamke, ona! Mwana wako!’” (Yohana 2:4; 19:26, NW) Utumizi wa Yesu wa neno “mwanamke” haukuwa kukosa heshima kulingana na utumizi wa wakati huo.

11. Hakuna andiko la Kibiblia ambalo hutumia msemo “Mama ya Mungu.”

12. “Mwanamke mmoja katika mkutano alipaza sauti yake, akamwambia, Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya. Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.”—Luka 11:27, 28.

13. “Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, . . . kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa.”—Luka 1:46, 48.

14. “Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu.”—1 Timotheo 2:5.

15. Vitano—Mathayo, Marko, Luka, Yohana, na Matendo. Atajwa kuwa “Mariamu” mara 19, kuwa “mama” ya Yesu mara 24, na “mwanamke” mara mbili.

16. Isipokuwa na waandikaji wanne wa Gospeli, Mariamu hatajwi kamwe—si hata katika matangulizi ya barua za kimitume. “Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, . . . Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.” (2 Wakorintho 1:1, 2) “Simoni Petro, mtumwa na mtume wa Yesu Kristo, . . . kwa uadilifu wa Mungu wetu na Mwokozi Yesu Kristo.”—2 Petro 1:1, NW.

17. Hatajwi hata mara moja.

18. “Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.” (1 Petro 2:5) “Nikaona, na tazama, huyo Mwana-Kondoo amesimama juu ya mlima Sayuni, na watu mia na arobaini na nne elfu pamoja naye, wenye jina lake na jina la Baba yake limeandikwa katika vipaji vya nyuso zao. . . . Na kuimba wimbo mpya mbele ya kile kiti cha enzi, . . . wala hapana mtu aliyeweza kujifunza wimbo ule, ila wale mia na arobaini na nne elfu, walionunuliwa katika nchi.”—Ufunuo 14:1, 3.

19. “Imba, wewe uliye tasa, wewe usiyezaa; paza sauti yako kwa kuimba, piga kelele, wewe usiyekuwa na utungu; maana watoto wake aliyeachwa ni wengi kuliko watoto wake yeye aliyeolewa, asema BWANA. Kwa sababu Muumba wako ni mume wako; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; na Mtakatifu wa Israeli ndiye Mkombozi wako; Yeye ataitwa Mungu wa dunia yote.” (Isaya 54:1, 5) “Yerusalemu wa juu ni mwungwana, naye ndiye mama yetu sisi.” (Wagalatia 4:26) Mwanamke wa Mungu wa ufananisho, Sayuni wa kimbingu, tengenezo la Yehova la kimbingu, linalinganishwa na mke na mama, naye ni “mwanamke” wa maandiko haya.

20. “Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, kama tukifa pamoja naye tutaishi pamoja naye pia; kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi.” (2 Timotheo 2:11, 12) Ikiwa Mariamu alithibitika kuwa mwaminifu hadi kifo, yeye sasa atawala mbinguni pamoja na wengine wa 144,000, ambao wanatawala pamoja na Kristo.—Ufunuo 14:1, 3.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki