Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 9/22 uku. 31
  • Jumuiya Inayoishi Kwenye Milonjo

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jumuiya Inayoishi Kwenye Milonjo
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka Kuwa Maficho Hadi Kivutio cha Watalii
  • Ziwa Viktoria—Ziwa Kuu la Afrika
    Amkeni!—1998
  • Mtumbwi—Usafiri Unaofaa Zaidi Nchini Kanada
    Amkeni!—2010
  • Mahali Mto Unaporudi Nyuma
    Amkeni!—2008
  • Uzuri wa Ziwa Kubwa Zaidi Amerika ya Kati
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 9/22 uku. 31

Jumuiya Inayoishi Kwenye Milonjo

Na mleta-habari wa Amkeni! katika Benin

“GANVIÉ ni mojawapo vivutio vikubwa vya watalii vya Benin,” chasema kitabu fulani cha mwongozo cha Afrika Magharibi. Kitabu kingine chasema: “Waafrika wenyewe huvutiwa na Ganvié; utawaona watalii Waafrika walio wengi kama watu wa magharibi.”

Kwa kweli Ganvié ni mahali pa kipekee. Hicho ni kijiji cha wakazi wapatao 15,000 ambacho kimejengwa kwenye milonjo juu ya maji ya Ziwa Nokoué, kaskazini mwa Cotonou, Benin. Hakuna baiskeli, wala magari, wala vijia vya kando ya barabara, wala barabara katika Ganvié. Wakazi wakitaka kwenda shuleni, sokoni, kituo cha afya, nyumba ya jirani, au mahali popote pale, wao hupanda mtumbwi uliochongwa kutoka kwa mti uitwao iroko.

Familia nyingi zina mitumbwi kadhaa—mmoja wa baba, mwingine wa mama, na nyakati nyingine mmoja wa watoto. Watoto hujifunza kupiga makasia mapema. Kufikia umri wa miaka mitano, mtoto aweza kuendesha mtumbwi akiwa peke yake. Upesi yeye hupata ujasiri wa kutosha kuweza kusimama katika mtumbwi ili kurusha wavu wa kuvua samaki. Vijana wengine hufurahia kujionyesha kwa wageni kwa kusimama kwa kichwa katika mitumbwi yao.

Katika soko linaloelea la Ganvié, wafanyabiashara, wengi wao wakiwa wanawake, huketi katika mitumbwi yao bidhaa zao zikiwa zimerundamana mbele yao—vikolezo, matunda, samaki, dawa, kuni, pombe, na hata redio. Wakiwa wamekingwa na kofia pana za nyasi dhidi ya jua la kitropiki, wao huuzia wateja wenye kuwajia kwa mitumbwi ili kununua vitu. Nyakati nyingine wauzaji ni wasichana wachanga. Usidanganyike na umri wao! Wao hujifunza mapema ustadi wa kufanya biashara.

Huku wanawake wakinunua na kuuza sokoni, wanaume hujishughulisha na uvuvi, au kihususa kufuga samaki. Njia yao ya kuvua samaki hutia ndani kuchoma mamia ya matawi katika sakafu ya wangwa yenye matope mengi, jambo linalotokeza msitu mkubwa wa vijiti. Samaki huja kwa wingi kula matawi yenye kuoza. Baada ya siku kadhaa wanaume hurudi wakiwa na nyavu zao ili kuvuna samaki.

Kutoka Kuwa Maficho Hadi Kivutio cha Watalii

Watoffinu wa Ganvié hawakuwa “Watu wa Maji” sikuzote, kama ambavyo wao huitwa leo. Mapema katika karne ya 18, wao walikimbilia ziwa na mabwawa ili kutoroka mnyanyaso wa ufalme jirani wa Kiafrika. Wasomi husema kwamba jina Ganvié huonyesha historia hiyo, kwa kuwa katika lugha ya Kitoffin, neno gan laweza kutafsiriwa “tumeokolewa” na neno vie lamaanisha “jumuiya.” Hivyo, jina la jiji hili kuu la vijiji vya ziwa huenda likatafsiriwa kwa njia isiyo hususa kuwa “jumuiya ya watu ambao hata hivyo wamepata amani.”

Kutafuta kuokoka katika eneo lenye bwawa kuzunguka Ziwa Nokoué kulikuwa mbinu nzuri, kwa kuwa itikadi za kidini za ufalme wenye kuwapinga hazikuruhusu mwanajeshi yeyote kuingia majini au maeneo ambayo yangeweza kupatwa na mafuriko. Hivyo, ziwa hilo likawa njia ya kupata riziki na vilevile himaya kutoka kwa adui. Ni jambo la kushangaza kwamba sasa jumuiya hii maarufu, ambayo halaiki za watalii huzuru kwa motaboti, pindi moja ilikuwa mahali pa kujificha.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki