Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g96 10/22 kur. 5-7
  • Kufunua Visababishi vya Usemi Wenye Kuudhi

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kufunua Visababishi vya Usemi Wenye Kuudhi
  • Amkeni!—1996
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Jinsi Unavyoanza
  • Uwezo wa Wakandamizaji
  • Kutoka Maneno Yaumizayo Hadi Maneno Yaponyayo
    Amkeni!—1996
  • Jinsi ya Kuepuka Maneno Yenye Kuumiza
    Amkeni!—2013
  • Waume, Waheshimuni Wake Zenu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2025
  • Sema Lililo “Jema kwa Ajili ya Kujenga”
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1996
g96 10/22 kur. 5-7

Kufunua Visababishi vya Usemi Wenye Kuudhi

“Kinywa cha mtu hunena yaujazayo moyo wake.”—MATHAYO 12:34.

MILEANI mbili hivi zilizopita, Yesu Kristo alitaarifu maneno yaliyo juu. Ndiyo, maneno ya mtu mara nyingi huonyesha hisia zake za ndani na nia zake. Hayo huenda yakawa yenye kustahili sifa. (Mithali 16:23) Kwa upande ule mwingine, huenda yakawa yenye hila.—Mathayo 15:19.

Mwanamke mmoja alisema hivi kuhusu mwenzi wake: “Yeye huelekea kukasirika ghafula, na kuishi naye mara nyingi ni kama kutembea katika eneo lililo na mabomu ya kutegwa ardhini—hujui kamwe ni nini kitakachochochea mlipuko.” Richard afafanua hali sawa na hiyo kuhusu mke wake. “Lydia sikuzote yuko tayari kwa vita,” yeye asema. “Yeye hazungumzi tu; yeye hushambulia kwa maneno kwa njia ya kivita, akinielekezea kidole kana kwamba mimi ni mtoto.”

Bila shaka, mabishano yaweza kuzuka hata katika ndoa bora zaidi, na wote waume na wake husema mambo ambayo baadaye hughairi. (Yakobo 3:2) Lakini usemi wenye kuudhi katika ndoa ni zaidi ya hilo; huo hutia ndani usemi wenye kushushia heshima na wenye kuchambua ambao unanuiwa kutawala, au kudhibiti mwenzi. Nyakati fulani, usemi wenye kudhuru hujificha katika mwonekano wenye kudanganya wa upole. Kwa kielelezo, mtunga-zaburi Daudi alimfafanua mtu ambaye alikuwa mpole, lakini ndani ni mwovu: “Kinywa chake ni laini kuliko siagi, bali moyo wake ni vita. Maneno yake ni mororo kuliko mafuta, bali hayo ni panga wazi.” (Zaburi 55:21; Mithali 26:24, 25) Uwe ni wenye kudhuru au uliofichika, usemi mkali waweza kuharibu ndoa.

Jinsi Unavyoanza

Ni nini kimfanyacho mtu atumie usemi wenye kuudhi? Kwa ujumla, utumizi wa usemi kama huo waweza kufuatiwa kwenye kile ambacho mtu huona na kusikia. Katika mabara mengi kukejeli, matukano, na maneno ya kuaibisha mtu hukubaliwa na hata kuonwa kuwa yenye ucheshi.a Waume hasa huenda wakaathiriwa na vyombo vya habari, ambavyo huonyesha wanaume “kamili” kuwa wenye kutawala na wakali.

Vivyo hivyo, wengi ambao hutumia usemi wenye kushusha heshima walilelewa katika nyumba ambamo hasira, chuki, na ugomvi wa mzazi ulitokea kwa ukawaida. Hivyo, tangu umri mchanga, walifahamu kwamba namna hii ya mwenendo ni ya kawaida.

Mtoto aliyelelewa katika mazingira kama hayo huenda akajifunza zaidi ya tabia hiyo ya usemi; yeye aweza pia kuingiza akilini maoni yaliyopotoka kujihusu na kuhusu wengine. Kwa kielelezo, ikiwa usemi mkali unaelekezewa mtoto, huenda akakua akihisi kuwa bure, hata kuchochewa kuwa mwenye hasira. Lakini namna gani ikiwa mtoto asikia tu kwa mbali baba yake akimshambulia mama yake kwa maneno? Hata kama mtoto huyo ni mchanga sana, yeye aweza kuweka akilini madharau ya baba yake kwa wanawake. Mvulana aweza kujifunza kutokana na mwenendo wa baba yake kwamba mwanamume ahitaji kudhibiti wanawake na kwamba njia ya kuwadhibiti ni kuwatisha au kuwaumiza.

Mzazi mwenye hasira huenda akamlea mtoto mwenye hasira, ambaye hatimaye atakua na kuwa “bwana mkubwa wa hasira” ambaye hutenda “makosa mengi sana.” (Mithali 29:22, NW, kielezi-chini) Hivyo matokeo ya usemi wenye kuumiza yaweza kupitishwa kutoka kizazi kimoja hadi kifuatacho. Akiwa na sababu nzuri, Paulo aliwashauri akina baba: “Msiwe mkichochea watoto wenu wakasirike.” (Wakolosai 3:21, NW) Ni jambo la maana kwamba neno la Kigiriki lililotafsiriwa “kuchochea ili kukasirika,” kulingana na Theological Lexicon of the New Testament, laweza kuwa na maana ya “kutayarisha na kuchochea kwa ajili ya pambano.”

Bila shaka, uvutano wa kimzazi hauvumilii kushambulia wengine, kwa maneno au vingine; lakini husaidia kueleza jinsi mwelekeo wa usemi wenye kudhulumu uwezavyo kuwa wa kina kirefu. Mwanamume kijana huenda asimtendee vibaya mke wake kimwili, lakini je, yeye humtendea vibaya kwa maneno yake na hisia zake za moyo zenye kubadilika-badilika? Kujichunguza huenda kukamfunulia mtu kwamba ameingiwa akilini na dharau la baba yake kwa wanawake.

Kwa wazi, kanuni zilizo juu zaweza pia kutumika kwa wanawake. Ikiwa mama anamtendea vibaya mume wake kwa maneno, huenda binti akamtendea mume wake kwa njia hiyo hiyo anapoolewa. Mithali ya Biblia yasema: “Ni bora kuwa ukiishi katika bara lililo ukiwa, kuliko na mwanamke mwenye ulimi-mchungu na mwenye hasira.” (Mithali 21:19, The Bible in Basic English) Hata hivyo, mwanamume apaswa kutahadhari hasa kuhusu jambo hili. Kwa nini?

Uwezo wa Wakandamizaji

Kwa kawaida mume huwa na uwezo zaidi katika ndoa kuliko mke. Sikuzote yaelekea yeye ni mwenye nguvu zaidi kimwili, ikifanya vitisho vya madhara ya kimwili viwe vyenye kuhofisha hata zaidi.b Kwa kuongezea, mara nyingi mwanamume ana stadi nzuri zaidi za kazi, stadi nyingi zaidi za kujiruzuku bila kutegemea wengine, na faida kubwa zaidi za kifedha. Kwa sababu ya hili, yaelekea mwanamke mwenye kushambuliwa kwa maneno atahisi amenaswa katika mtego na akiwa mpweke. Huenda akakubaliana na taarifa ya Mfalme Sulemani mwenye hekima: “Nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji.”—Mhubiri 4:1.

Huenda mke akavurugika ikiwa mume wake hubadilika-badilika sana—mwenye fadhili dakika moja, mwenye kuchambua dakika ifuatayo. (Linganisha Yakobo 3:10.) Na zaidi, ikiwa mume wake anaandaa vizuri kimwili, mke ambaye ni shabaha ya usemi mkali huenda akahisi kuwa mwenye hatia kwa kufikiri kwamba kuna jambo baya katika ndoa. Huenda hata akajilaumu kwa mwenendo wa mume wake. “Kama tu mke mwenye kupigwa kimwili,” aungama mwanamke mmoja, “mimi sikuzote nilikuwa nikijifikiria kuwa kisababishi.” Mke mwingine asema: “Nilifanywa niamini kwamba ikiwa ningejaribu zaidi tu kumfahamu na ‘kuwa mwenye subira’ naye ningepata amani.” Kwa kuhuzunisha, mara nyingi kutendwa vibaya huendelea.

Kwa kweli ni jambo lenye kuhuzunisha kwamba waume wengi hutumia vibaya uwezo wao kwa kumtawala mwanamke ambaye huenda walitoa nadhiri kumpenda na kumtunza. (Mwanzo 3:16) Lakini ni nini kiwezacho kufanywa kuhusu hali kama hiyo? “Sitaki kuondoka,” asema mke mmoja, “Nataka tu aache kunitenda vibaya.” Baada ya miaka tisa ya ndoa, mume mmoja akiri hivi: “Natambua kwamba niko katika uhusiano wenye maneno yenye kuudhi na kwamba mimi ndiye mwenye kuudhi. Bila shaka nataka kubadilika, si kuondoka.”

Kuna msaada kwa wale ambao ndoa zao zimepatwa na usemi wenye kuumiza, kama makala ifuatayo itakavyoonyesha.

[Foonotes]

a Kwa wazi, ndivyo ilivyokuwa katika karne ya kwanza. The New International Dictionary of New Testament Theology hutaja kwamba “kwa Wagiriki ulikuwa mmojapo usanii wa maisha kujua jinsi ya kutukana wengine au kustahimili matukano.”

b Ukatili wa maneno waweza kuwa jiwe la kukanyagia kuelekea jeuri ya nyumbani. (Linganisha Kutoka 21:18.) Asema mshauri mmoja wa wanawake wenye kupigwa: “Kila mwanamke anayekuja ili kupata amri ya kisheria ya ulinzi dhidi ya kupigwa, kudungwa kisu, au kusongwa pumzi ambako kwahatarisha uhai wake amekuwa, kwa kuongezea, na historia ndefu yenye maumivu ya kuudhiwa kusiko kwa kimwili.”

[Blabu katika ukurasa wa 6]

Kwa kuhuzunisha, waume wengi hutumia vibaya uwezo wao kwa kumtawala mwanamke ambaye huenda walitoa nadhiri kumpenda na kumtunza

[Picha katika ukurasa wa 7]

Mtoto huathiriwa na jinsi ambavyo wazazi wanatendeana

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki