Kutoka kwa Wasomaji Wetu
Mateka Mimi ni mfungwa na bado nina miaka miwili nimalize kifungo changu. Nilisoma mara mbili ile makala “Tulikuwa Mateka Wakati wa Maasi ya Gereza.” (Novemba 8, 1996) Kila wakati, ilinifanya nidondoke machozi ya shangwe na kusakamwa. Mimi hutazamia nyakati zote ziara za Mashahidi wa Yehova katika gereza hili. Ziara zao huburudisha sana!
J. K., Marekani
Sijapata kuwaandikia kamwe kuhusu makala yoyote, lakini makala kuhusu mateka ilikuwa yenye kuimairisha imani sana. Ilinipa uhakikisho upya kwamba Yehova huimarisha watu wake wanaposononeka.
K. D., Marekani
Mwongozo Nilifurahia sana makala “Maoni ya Biblia: Unaweza Kutumaini Uongozi wa Nani?” (Novemba 8, 1996) Ilikuwa yenye kufariji na yenye kutia moyo sana. Kama ilivyo na wengine wengi, nimetamaushwa sana katika wakati uliopita wakati wale niliowatazamia kwa mwongozo waliponitamausha. Kile kielezi cha mtoto akishika mkono wa babake kilifanya nidondoke machozi. Inachangamsha moyo sana kujua kwamba katika Isaya 41:13, Yehova asema ‘atashika mkono’ wa watu wake.
M. S., Marekani
Nina umri wa miaka 17 na hivi karibuni nimekuwa na matatizo mengi. Rafiki yangu mmoja aliniambia nisali na kusoma kitu cha kiroho. Baada ya kusoma makala “Unaweza Kutumaini Uongozi wa Nani?” Niliamua nisikate tamaa bali nishikilie mkono wa Baba yetu wa kimbingu hata kwa nguvu zaidi!
C. G., Marekani
Lugha ya Ishara Asanteni sana kwa makala “Nilijifunza Lugha Nyingine ili Kuwasiliana na Mtoto Wangu.” (Novemba 8, 1996) Mimi ni mama asiye na mwenzi na nina mwana kiziwi ambaye sasa ana umri wa miaka 24. Basi ninajua kutokana na mambo niliyojionea yale ambayo Cindy Adams ameyapitia, na ninaheshimu sana kile ambacho ametimiza.
H. B., Ujerumani
Makala hiyo ilinifanya nianze kujifunza lugha ya ishara ili niweze kushiriki ujumbe wa Biblia pamoja na viziwi na pia kuwasiliana na ndugu walio viziwi kutanikoni.
B. L., Venezuela
Nilijifunza Biblia na msichana tineja aliye kiziwi. Tulijifunza mengi kutoka kwa kila mmoja, japo uhakika wa kwamba sisi sote hatukujua sana lugha ya ishara. Kusoma juu ya azimio la Cindy Adams kujifunza lugha kwa sababu ya mwana wake kulinitia moyo kuboresha ustadi wangu wa lugha hii nzuri ili niweze kushiriki habari njema ya Biblia na viziwi katika jumuiya yetu.
S. T., St. Martin, Netherlands Antilles
Mimi pia nina mtoto kiziwi, nasi tulichagua njia ya mawasiliano ya kusoma mdomo. Njia hii hukazia matamshi na kuweza kusoma mdomo. Ikawa kwamba huo ulikuwa uchaguzi mzuri kwa mwana wangu. Mwanzoni hakufaidika na mikutano ya kutaniko. Lakini sasa yeye aweza kufuatisha mambo wakati mimi na wengine tunapomtafsiria. Yeye hutoa hotuba katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi naye ni mhubiri asiyebatizwa. Miaka mingi ya kazi imethawabishwa. Mambo tuliyojionea yaonyesha kwamba ama Lugha ya Ishara ya Kimarekani au njia ya kusoma mdomo yaweza kunufaisha maadamu wazazi na kutaniko la mahali hapo hufanya bidii ya kumtia moyo mtoto na kuwasiliana naye.
M. T., Marekani