Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 9/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Redio ya Darubini-Upeo Iliyowekwa Angani
  • Televisheni kwa Watoto Wadogo?
  • Tatizo la Uraibu wa Internet
  • Mradi wa Simbamarara Wafifia
  • Onekana Mzee Lakini Kufa Ukiwa Mchanga
  • Hatari ya Radi
  • Kushuka Moyo kwa Wazee-Wazee
  • Mchwa Wanaochimba Dhahabu
  • Adabu za Simu Zenye Kuchukulika
  • ‘Vioevu Vyenye Akili’
  • Simbamarara! Simbamarara!
    Amkeni!—1996
  • Simbamarara wa Siberia—Je, Ataokoka?
    Amkeni!—2008
  • Intaneti Kutumia kwa Hekima Kifaa cha Ulimwenguni Pote
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Internet—Kwa Nini Utahadhari?
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 9/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Redio ya Darubini-Upeo Iliyowekwa Angani

Taasisi ya Anga na Sayansi ya Vyombo vya Angani ya Japani hivi majuzi imepeleka angani redio ya darubini-upeo yenye kipenyo cha meta nane, laripoti gazeti Science News. Upekee wa darubini-upeo hii mpya ni kule kuunganishwa kwake na redio za darubini-upeo zipatazo 40 zilizowekwa katika sehemu mbalimbali za ulimwengu. Mfumo huu wajulikana kama Very Long Baseline Space Observatory. Vitu vinavyotoka katika vyanzo vya angani vyenye ishara za redio, kama vile kwasari na mashimo meusi, hunaswa na darubini-upeo hizo za redio zilizotapakaa kisha vitu hivyo hufanyizwa kutokeza umbo moja. Kadiri mtengano ulivyo mkubwa kati ya hizo darubini-upeo, ndivyo na umbo la mwisho lionekanavyo kuwa wazi zaidi. Muundo wa yai wa darubini-upeo hii utaichukua kilometa 20,000 kutoka duniani ikiwa mwisho zaidi. Darubini-upeo mpya iliyowekwa angani huandaa mwono wa wazi zaidi kwa mara 1,000 zaidi kuliko Darubini-Upeo ya Angani ya Hubble iwezavyo kuandaa katika nuru ya wazi. “Katika mwono huo wa wazi,” lataarifu Science News, “mtazamaji katika Los Angeles aweza kutambua punje ya mchele ikiwa Tokyo.”

Televisheni kwa Watoto Wadogo?

Ili kupata wakati wa kufanya kazi za lazima, wazazi wengi wanaosumbuliwa wa watoto wadogo wanaweza kuwa wenye mwelekeo wa kuwaweka mbele ya televisheni ili waweze kufanya kazi. Lakini kulingana na gazeti la Parents, hili hutokeza hatari kwa mtoto. “Programu zenye jeuri,” kutia na katuni nyingi, laeleza, “zimeonyeshwa kwa kauli moja kuwa huongeza hali ya uchokozi katika watazamaji wachanga.” Kwa kuongezea, uchunguzi uliofanywa na Dorothy Singer wa Chuo Kikuu cha Yale waonyesha kwamba “utazamaji wa daima wa televisheni kabla ya kuanza shule wahusianishwa na tabia mbaya na [baadaye] hukawiza utayari wa kusoma.” Singer apendekeza muda usiozidi dakika 30 kwa siku wa kutazama televisheni kwa watoto wa umri wa mwaka mmoja. Hangaikio jingine ni aksidenti ziwezazo kutokea wakati mtoto yuko peke yake na televisheni. Mtungaji Milton Chen asema: “Inachukua dakika moja tu kwa mtoto mdogo asiyechungwa na aliye mtendaji kuingia matatani.” Gazeti Parents lapendekeza kwamba umweke mtoto wako na vichezeo vichache vilivyo salama mahali pake pa kuchezea karibu nawe unapolazimika kutayarisha chakula cha mchana au kujibu simu.

Tatizo la Uraibu wa Internet

“Tokeo la karibuni zaidi la enzi ya habari za kompyuta laweza kuwa uraibu kwa Internet,” laripoti Canadian Medical Association Journal. Dakt. Kimberly Young alichunguza watu 496 wanaoitumia Internet sana, 396 wa watu hawa wakitambulishwa kuwa waraibu. Uchunguzi huo ulifunua kwamba matokeo ya uraibu wa Internet yatia ndani “kujitenga, kutopatana katika ndoa, kutofaulu katika masomo, madeni makubwa ya kifedha, [na] kuacha kazi.” Dakt. Young asema kwamba hilo tatizo “ni uraibu halisi kama vile uraibu wa alkoholi au kucheza kamari kusikoweza kudhibitiwa.” Jarida hilo liliongezea kuwa “wanaotumia kompyuta nyumbani wamo hatarini zaidi.” Ingawa mtu yeyote aweza kunaswa kupita kiasi na Internet, “mraibu halisi ni mwanamke wa makamo aliye na elimu kidogo,” asema Dakt. Young. Baadhi ya dalili za hatari ni kutumia muda mwingi mno kwenye Internet na “kuacha mambo ya muhimu ya kijamii au ya kikazi” ili kutumia Internet.

Mradi wa Simbamarara Wafifia

Katika mwaka wa 1973, Mradi wa Simbamarara ulianzishwa huko India ili kuzuia kutoweka kabisa kwa mnyama huyo wa kitaifa wa nchi hiyo. Wakati huo, idadi ya simbamarara India ilikuwa tayari imepungua hadi 1,827. Mradi huo ulifurahia tegemezo la kimataifa na fanikio la wazi. Kufikia 1989 idadi ya simbamarara wa India ilikuwa imepanda kufikia zaidi ya 4,000. Hata hivyo, sasa simbamarara yuko hatarini tena, kulingana na gazeti India Today. Idadi ya simbamarara wa India yakadiriwa kuwa imeanguka kufikia chini ya 3,000. Kwa nini? Watu fulani husema kwamba wawindaji haramu wanaua, kwa wastani, simbamarara mmoja kila siku. Mradi wa Simbamarara ulikusudiwa kuandaa kinga kwa paka huyu mkubwa. Lakini hauelekei unaweza kufanya hivyo. “Mlinda-msitu, ambaye kwa kawaida hufyatuliwa risasi, huwa amevunjika moyo na kukosa vifaa vinavyofaa,” ripoti hiyo yaeleza. Kwa simbamarara, “kuwapo kwaelekea kwenye kutoweka.”

Onekana Mzee Lakini Kufa Ukiwa Mchanga

Kama ionyeshwavyo na ripoti zifuatazo, watafiti waamini kwamba uvutaji wa sigareti waweza kuharakisha utaratibu wa kuzeeka. Wavutaji wa sigareti wa muda mrefu wana mwelekeo wa kupata mvi mapema na kuelekea kupata upaa mara mbili zaidi, kulingana na gazeti la Lancet la Uingereza. Likiripoti kuhusu hili, UC Berkeley Wellness Letter lilisema kuwa wavutaji wa sigareti huwa na makunyanzi mengi zaidi ya usoni na wana mwelekeo wa kupoteza meno mara mbili zaidi ya wasiovuta sigareti. Ripoti hiyo yarejezea kwenye uchunguzi wa juzijuzi ulioonekana kwenye British Medical Journal ulioonyesha kuwa wanaume wanaovuta sigareti muda wote wa maisha yao wana uwezekano wa nusu tu wa kufikia umri wa miaka 73 kwa kulinganishwa na wale wasiovuta sigareti. Kwa kuongezea, gazeti Good Housekeeping laripoti kuwa “watu wasiovuta sigareti wanaoishi pamoja na wavutaji wa sigareti wana uwezekano zaidi wa asilimia 20 wa kuugua maradhi ya moyo.”

Hatari ya Radi

“Mapigo ya radi yenye kufisha,” laripoti gazeti The Australian, “hutokea mara nyingi kuliko watu wafikirivyo.” Radi huua kati ya watu watano na kumi katika Australia kila mwaka na kusababisha majeruhi zaidi ya 100, ripoti hiyo yaeleza. Hakuna onyo kwa pigo linalokaribia, ingawa “watu fulani waliokaribia kupigwa na radi wameripoti kuhisi nywele zao zikisimama wima,” asema Phil Alford wa Ofisi ya Metorolojia la Melbourne. Ili kuboresha hali yako ya kuepuka kupigwa na radi, Alford apendekeza kwamba utafute kinga dhidi ya mvua ya radi katika jengo thabiti au ndani ya gari lililofunikwa lisilo karibu na vitu vilivyojengwa kwa vyuma.

Kushuka Moyo kwa Wazee-Wazee

“Kushuka moyo kwa watu wenye umri huonekana katika njia tofauti na watu wachanga,” laripoti Jornal do Brasil. Badala ya kujitokeza kama maumivu makali au hangaiko, mshuko-moyo kama huo “huashiriwa na kupoteza uwezo wa utambuzi—kumbukumbu, kukazia fikira, na uwezo wa kufikiri.” Zaidi ya hilo, kulingana na Profesa Paulo Mattos wa Chuo Kikuu cha Federal cha Rio de Janeiro, “wazee-wazee walioshuka moyo huonyesha kuhisi hatia kupita kiasi kwa mambo yasiyo na msingi. Wanakosa upendezi katika mambo waliyokuwa wakifanya au mambo yaliyowaletea furaha,” kutia ndani mazungumzo. Dalili kama hizo wakati mwingine huonwa kimakosa kuwa sehemu ya kuzeeka, ripoti hiyo yasema. Ili kutambua mabadiliko kama hayo katika tabia na kutambulisha mshuko-moyo, asema Dakt. Mattos, “ni muhimu kwamba watu washirikiane daima na washiriki wa familia walio wazee-wazee.”

Mchwa Wanaochimba Dhahabu

Katika 1984 mwanakijiji mmoja aligundua dhahabu katika nchi ya Kiafrika ya Niger, na shughuli za kutafuta dhahabu zilizofuata zilileta wachimbaji kutoka nchi nyingi kwenye eneo hilo. Mwanajiolojia Mkanada Chris Gleeson alikumbuka kwamba staarabu za kale za Kiafrika zilitumia vichuguu kupata mahali palipo na dhahabu. Niger ina spishi fulani ya mchwa wanaotengeneza vichuguu vikubwa, vingine vikiwa na urefu wa meta 1.8 na kipenyo cha meta 1.8. Vichuguu hivi huendelea kuwa vikubwa kadiri mchwa waendeleavyo kuchimba—nyakati nyingine kufikia kina cha meta 75—wakitafuta maji, laeleza gazeti National Geographic. Gleeson alichukua sampuli kutoka katika vichuguu vingi akitarajia kuwa zitamwonyesha mahali atakapochimba. Sampuli nyingi hazikuwa na dhahabu, lakini nyingine zilikuwa nayo! Alipata kuwa “kichuguu chochote kilichokuwa na dhahabu kilikuwa na dhahabu kote.” Inaonekana kwamba wakati mchwa wanapochimba ili kupata maji, chochote wanachokutana nacho hukitoa nje, kutia ndani dhahabu.

Adabu za Simu Zenye Kuchukulika

Kufika kwa simu zenye kuchukulika mfukoni kumeongezea uhitaji wa adabu fulani za kikale kulingana na gazeti Far Eastern Economic Review. Mshauri wa biashara wa Hong Kong, Tina Liu anatia moyo kuonyesha staha na ufikirio, kwa mtu unayezungumza naye kwa simu na pia wengine ambao huenda wakawa karibu nawe. Anashauri kuzungumza kwa uwazi lakini si kwa sauti kubwa na kutokula au kunywa unapotumia simu. Liu apendekeza pia kupunguza idadi ya simu zinazopokewa katika mikutano na kuelekeza simu kwingine au kuzibadilisha kwenye ishara za mtetemo katika sehemu kama vile hospitali, maktaba, na majumba ya mikutano. Kukatiza pindi za sherehe kwa kuchukua simu kwaweza kuwafanya marafiki na jamaa wahisi wamepuuzwa. Kuhusu kula katika mikahawa, Liu asema: “Mtu anayezungumza kwa simu akiwa na mwanamke afadhali amalize kuzungumza kwa simu kabla ya matokeo ya maua aliyompa kwisha.”

‘Vioevu Vyenye Akili’

Mradi umeme umepitishwa katika vioevu fulani vyenye vitu vinavyoelea, vitu hivi hutengeneza atomu zilizoungana kama minyororo midogo, vikifanya vioevu hivyo kuwa vizito zaidi. Tukio hili linaitwa tokeo la Winslow, likipewa jina la Dakt. W. M. Winslow, aliyeligundua katika mwaka wa 1940. Tangu wakati huo, kiwanda cha vitu vya mashine pamoja na vingine, kutia ndani Dakt. Winslow mwenyewe, sasa akiwa na umri wa miaka 93, waendelea kutafuta utumizi wenye kutumika wa ‘vioevu vyenye akili kama hivyo.’ Watafiti katika Chuo Kikuu cha Kitaifa cha Michigan katika Marekani walijua kwamba chokoleti ya maziwa yaliyoyeyushwa ina sifa fulani sawa na ‘vioevu vyenye akili.’ Kama ilivyodhaniwa, katika majaribio ya juzijuzi, kipande cha chokoleti kilichoyeyushwa kilibadilika karibu mara hiyo kuwa kizito na kigumu kilipowekewa umeme mkali. ‘Kioevu kingine chenye akili,’ chenye wanga wa mahindi na kuwekwa juu ya mafuta ya taa, hutofautiana kati ya uzito wa maziwa na ule wa siagi kadiri kiasi cha umeme kinavyobadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki