Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 9/8 uku. 26
  • “Upatano Wenye Kulingana Kabisa”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Upatano Wenye Kulingana Kabisa”
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Misuli—Kazi Bora za Ubuni
    Amkeni!—1999
  • Kusema kwa Njia Inayoeleweka Wazi
    Faidika na Elimu ya Shule ya Huduma ya Kitheokrasi
  • Jinsi Ulivyo Kiumbe cha Kipekee!
    Je, Kuna Muumba Anayekujali?
  • Sema Lililo “Jema kwa Ajili ya Kujenga”
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 9/8 uku. 26

“Upatano Wenye Kulingana Kabisa”

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA AFRIKA KUSINI

USEMI wa binadamu hustaajabisha sana. Misuli ipatayo 100 katika kifua, koo, utaya, ulimi, na midomo hufanya kazi pamoja ili kutokeza sauti nyingi sana tofauti-tofauti. Kila musuli ni tita la mamia hadi maelfu ya nyuzi. Chembe nyingi zaidi za ubongo hudhibiti nyuzi hizi za musuli kuliko zinavyohitajika kusukuma misuli ya mguu wa mwanariadha. Chembe moja ya neva inatosha kusukuma nyuzi zote 2,000 za musuli wa shavu la mguu. Kwa kutofautisha, chembe za neva zinazodhibiti zoloto, zaweza kushikanishwa na nyuzi mbili au tatu pekee za musuli.

Kila neno au fungu fupi la maneno ambalo unasema lina kiolezo chake lenyewe cha misogeo ya misuli. Habari zote zinazohitajika ili kurudia fungu la maneno kama “U hali gani?” huwekwa akiba katika eneo la ubongo linaloshughulikia usemi. Je, hiyo yamaanisha kwamba ubongo wako hutumia programu ya kipekee ya musuli ya hatua kwa hatua ambayo hainyambuliki ili urudie kila neno au fungu la maneno? La. Nguvu za usemi ni zenye kutisha sana kuliko hiyo. Kwa kielelezo, huenda ukawa na kidonda kinywani kinachofanya upate ugumu wa kutamka maneno katika njia yako ya kipekee. Bila kufikiria, ubongo hubadilikana ili ufae mwendo wa misuli ya usemi, ukikuwezesha kutamka maneno kwa karibu iwezekanavyo na njia yako ya kawaida ya kusema. Hili laonyesha jambo jingine la kustaajabisha sana.

Salamu sahili kwa sauti kama vile “habari” yaweza kutokeza maana nyingi. Namna ya sauti yaweza kuonyesha kama msemaji ni mwenye furaha, amesisimka, amechoshwa, ana shughuli nyingi, amekasirika, ni mwenye huzuni, au ameogopa na yaweza kuonyesha kadiri tofauti-tofauti za hali hizo za kihisia moyo. Ndiyo, maana ya kila neno yaweza kubadilika kwa kutegemea kadiri ya mwendo na ulingano wa nukta tu za sekunde wa misuli mingi tofauti-tofauti.

“Kwa kadiri,” aeleza Dakt. William H. Perkins katika kitabu chake Stuttering Prevented, “sisi hutamka maneno yapatayo 14 kwa kila sekunde. Hiyo ni mara mbili ya kadiri tuwezavyo kudhibiti ulimi wetu, midomo, utaya au sehemu nyinginezo za utendeshaji wetu wa usemi tunapozijongeza zikiwa tofauti-tofauti. Lakini uziweke zote pamoja kwa ajili ya usemi nazo hufanya kazi kama tu vile vidole vya wachapa-taipu stadi na wapiga-piano wa maonyesho ya muziki vifanyavyo. Misogeo yao hupishana katika upatano wenye kulingana kabisa.”

Kwa kadiri ndogo, ndege fulani waweza kuiga sauti za usemi wa wanadamu. Lakini hakuna mnyama ambaye ana ubongo ambao umeratibiwa kutokeza usemi jinsi ambavyo ubongo wa binadamu hufanya. Haishangazi kwamba wanasayansi hawajafanikiwa katika majaribio yao ya kufundisha sokwe kutamka sauti zilizo wazi za usemi. Kulingana na mwanabiolojia wa nyuroni Ronald Netsell, ustadi ambao unahitajika ili kusema unaweza kulinganishwa na ule wa “mtu asiye wa kawaida ambaye hucheza piano ‘kutokana na kumbukumbu’ tu.” Au kama mtunga-kamusi Ludwig Koehler alivyokata kauli: “Usemi wa binadamu ni siri; ni zawadi ya kimungu, ni muujiza.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki