Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 9/8 kur. 24-25
  • Kaba—Mtindo wa Mavazi Wenye Madaha wa Kiafrika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kaba—Mtindo wa Mavazi Wenye Madaha wa Kiafrika
  • Amkeni!—1997
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Kaba Yawa Mtindo
  • Adabu Nzuri ya Kike
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1978
  • Mitindo Inayobadilika
    Amkeni!—2003
  • Fashoni—Mtindo wa Kale wa Kigiriki
    Amkeni!—1995
  • Je, Mtindo Wako wa Mavazi Unamtukuza Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Funzo)—2016
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 9/8 kur. 24-25

Kaba—Mtindo wa Mavazi Wenye Madaha wa Kiafrika

NA MLETA-HABARI WA AMKENI! KATIKA GHANA

KABA—waweza kuiona karibu kila mahali hapa Ghana na nchi jirani za Afrika Magharibi. Huvaliwa kwenye pindi mbalimbali—kutoka maziko hadi vikusanyiko vya Kikristo vyenye furaha. Na kaba ina mitindo na rangi tofauti-tofauti.

Hiyo kaba ni nini hasa? Ni mtindo wa mavazi ya wanawake unaopendwa sana. Jina hilo hurejezea vazi la nje linaloanzia chini ya shingo hadi kwenye kiuno. Hata hivyo, haivaliwi peke yake. Kipande cha kitambaa chenye ukubwa wa meta mbili ambacho huitwa na wengi chapa ya wax au chapa ya java ikitegemea ubora wa kitambaa hicho, huambatana nayo. Likifungwa kiunoni na kuishia kwenye vifundo vya miguu, vazi hili laitwa asetam. Suti hii inakamilika wakati inapofungwa kwa kipande kingine tena cha nguo chenye ukubwa wa meta mbili kiitwacho nguso. Hiyo nguso ina matumizi mengi nayo yaweza kutumiwa pia kama kitambaa cha kichwa chenye kufanana na mavazi au kama njia ya kubebea mtoto mgongoni.

Kaba ni ya kipekee kwa Afrika, lakini yajulikana kwa majina tofauti-tofauti kote katika hii kontinenti. Waliberia huiita suti ya lappa. Katika Benin inaitwa genwu. Watu wa Sierra Leone huiita docket na lappa. Hata hivyo, sio muda mrefu uliopita, kaba haikujulikana katika nchi za Kiafrika. Kwa kielelezo, hapa katika Ghana mtindo wa dansenkran ulipendwa sana na wanawake waliozungumza lugha ya Akan. Huu ulitia ndani vipande viwili vya kitambaa, wakati mwingine vyenye mchoro sawa. Kipande kimoja kilifungwa kiunoni na kushikiliwa kwa mshipi. Kipande cha pili, kikubwa zaidi kwa kawaida, kilivaliwa kwenye bega la kushoto kupitia kifuani na mgongoni. Mtindo maalumu wa nywele ulioitwa pia dansenkran, mara nyingi ulitengenezwa pamoja na vazi hili.

Lakini, kwa kuanzishwa kwa cherahani, wanawake fulani Waafrika walianza kushona nguo zilizofanana na blauzi za Magharibi. Kusudi lilikuwa kufunika mabega kama vile wanawake wa Magharibi walivyofanya. Simulizi moja lasema kwamba watu fulani walikuwa na matatizo ya kutamka msemo “cover the shoulders” (funika mabega). Neno “cover” likawa kaba.

Kaba Yawa Mtindo

Kuanzia wanawake wafanyao kazi ofisini hadi wafanyao kazi shambani, wote waendelea kuvaa kaba. Kwa kweli, hata imekuwa bidhaa ya kuuzwa nchi za nje! Hata hivyo, kupendwa huko ni kwa juzijuzi tu kwa kulinganishwa.

Jambo moja ni kwamba sio wanawake wote waliopenda mitindo ya kaba iliyokuwako miaka kama 40 hivi iliyopita. Mfanyakazi wa huduma za jamii aliyestaafu aitwaye Agnes, mwenye umri wa miaka 62, aliliambia Amkeni! kuwa baadhi ya mitindo ya zamani ilikuwa ya “upuuzi.” Kwa wanawake wengine, kuvaa kaba sawasawa, pamoja na asetam na nguso yake, ilihitaji subira nyingi sana na ustadi. Elizabeth ambaye ana kiwanda cha kushonea nguo, akumbuka: “Ilikuwa vigumu kwetu sisi wanawake wachanga kujifunza ustadi wa kuvaa asetam na nguso. Mimi sikupata ustadi huo,” yeye akiri.

Mgawanyo wa jamii katika tabaka pia ulichangia kupunguza umashuhuri wa mtindo huu wa nguo. Serwah, mwenye umri wa miaka 65, aliliambia Amkeni! kuwa hata kufikia majuzi, wengi wamehisi kwamba nguo za mtindo wa Magharibi ni za wale walioelimika, hali kaba ni ya wale wasioelimika.

Hata hivyo, ufahamu mpya wa kitamaduni umewafanya wanawake Waafrika waifikirie tena kaba. Wafanyiza-mitindo wameuinua sana mvao huu. Jambo moja ni kwamba wametokeza vazi liitwalo slit. Ikiwa na muundo kama wa skati lakini ikifika kwenye vifundo vya miguu, ilisuluhisha tatizo walilokuwa nalo wanawake fulani la kuifunga asetam na nguso sawasawa. Maonyesho pia yamechangia sana kuiinua kaba kuwa mtindo wa hali ya juu.

Bila shaka, kama ilivyo na mitindo katika nchi nyingi, mishono mingine ya karibuni zaidi hukazia sana uvutio wa kingono. Clara, mwenye umri wa miaka 69, hushindania kwamba mavazi kama hayo yenye kufunua mwili yaonekana yapotosha “lengo la awali la kaba,” ambalo lilikuwa “kufunika hata mabega.” Hivyo, wanawake Wakristo huweka maanani shauri la mtume Paulo: “Hivyohivyo natamani wanawake wajirembe wenyewe katika mavazi yenye mpangilio mzuri, pamoja na kiasi na utimamu wa akili.”—1 Timotheo 2:9; 1 Wakorintho 10:29.

Kwa wanawake wanaochagua kwa hekima, kaba yaweza kuthibitika kuwa mtindo wa nguo wenye madaha na wenye kutumika. Na hali mitindo mingi ya kitamaduni ya mavazi ya Kiafrika imekuwa ya kikale, kaba imeweza hadi sasa kuokoka ikiwa mtindo unaoonyesha utamaduni na mazingira ya Kiafrika katika njia yenye kuvutia na yenye madaha.

[Picha katika ukurasa wa 24]

Nguso, ikitumiwa hapa ikiwa kitambaa cha kichwa

[Picha katika ukurasa wa 25]

Nguso, ikitumiwa kumbeba mtoto

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki