Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 11/22 uku. 3
  • Tauni Haikuwa Mwisho wa Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Tauni Haikuwa Mwisho wa Ulimwengu
  • Amkeni!—1997
  • Habari Zinazolingana
  • Tauni ya Karne ya 14 Msiba wa Ulaya ya Enzi za Kati
    Amkeni!—2000
  • Jitihada za Muda Mrefu za Kuboresha Afya
    Amkeni!—2004
  • Mapigo 10
    Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia
  • Magonjwa ya Kuambukiza Katika Karne ya 20
    Amkeni!—1997
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1997
g97 11/22 uku. 3

Tauni Haikuwa Mwisho wa Ulimwengu

KATIKA Oktoba ya 1347, meli za biashara kutoka Mashariki ziliingia bandari ya Messina, katika Sicily. Wapiga-makasia walikuwa wenye maradhi na walikuwa wakifa. Miili yao ilikuwa na vivimbe vyeusi vilivyotoshana na yai na kutoa damu na usaha. Mabaharia hao waliteseka kwa uchungu mwingi na walikufa siku chache baada ya dalili za kwanza kutokea.

Panya kutoka katika meli hizo walikimbia kujiunga na idadi ya wagugunaji wenyeji. Panya hao waliwabeba viroboto waliokuwa wameambukizwa na basila iwezayo kusababisha kifo kwa binadamu. Hivyo ukaenea ugonjwa wa mlipuko uitwao tauni, ugonjwa wa kuambukiza, uliokuwa mbaya zaidi katika historia ya Ulaya kufikia wakati huo.

Tauni hiyo ilikuwa ya aina mbili. Aina moja, iliyopitishwa kwa kuumwa na kiroboto aliyeambukizwa, ilienea katika mfumo wa damu na kusababisha vivimbe na kuvuja damu kwa ndani. Hiyo nyingine, iliyopitishwa kwa wengine kwa kukohoa au kupiga chafya, iliambukiza mapafu. Kwa kuwa namna zote mbili zilikuwako, maradhi hayo yalienea haraka na kwa njia yenye kuogofya na yenye ukatili sana. Katika miaka mitatu tu, ilimaliza robo ya idadi ya watu wa Ulaya; labda watu milioni 25 walikufa.

Wakati huo hakuna aliyejua jinsi maradhi hayo yalivyopitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Wengine waliamini kuwa hewa ilikuwa na sumu, labda kwa sababu ya tetemeko la dunia au mfungamano usio wa kawaida wa sayari. Wengine walifikiri kuwa watu walishikwa na ugonjwa kwa kumtazama tu mtu aliyeambukizwa. Ingawa kauli zilitofautiana, kwa wazi maradhi hayo yalikuwa yenye kuambukiza sana. Tabibu mmoja Mfaransa alionelea kuwa ilionekana ni kama mtu mmoja mgonjwa “angeweza kuambukiza ulimwengu wote.”

Watu hawakujua kinga wala tiba yoyote. Wengi walifikiria unabii mbalimbali wa Biblia kama ule uliorekodiwa kwenye Luka 21:11, ambao hueleza kuhusu magonjwa ya kuambukiza katika wakati wa mwisho. Ingawa pesa nyingi zilimiminwa kanisani, tauni hiyo iliendelea. Mwitalia mmoja aliandika hivi wakati huo: “Kengele za kanisa hazikupigwa kutangaza kifo cha mtu yeyote na hakuna mtu aliyetoa machozi hata awe amepoteza nani kwa sababu karibu kila mmoja alitarajia kifo . . . watu walisema na kuamini, ‘Huu ndio mwisho wa ulimwengu.’”

Hata hivyo, haukuwa mwisho. Kufikia mwisho wa karne ya 14, tauni hiyo ilikuwa imepungua. Ulimwengu uliendelea.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 3]

Picha za Archive

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki