Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 5/22 kur. 3-4
  • Mazungumzo Kuhusu Halihewa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mazungumzo Kuhusu Halihewa
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Biblia Inasema Nini Kuhusu Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Wakati Wetu Ujao?
    Habari Zaidi
  • Kwa Nini Hali ya Hewa Imebadilika?
    Amkeni!—2003
  • Je, Dunia Inakabili Hatari?
    Amkeni!—2008
  • Ustadi na Utaalamu wa Kutabiri Hali ya Hewa
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 5/22 kur. 3-4

Mazungumzo Kuhusu Halihewa

POPOTE unapoishi hata uwe nani, halihewa huathiri maisha yako. Siku inapoamua kuwa yenye joto na yenye jua, unavalia nguo nyepesi. Inapokuwa baridi, unavalia koti na kofia. Inyeshapo? Unachukua mwavuli wako.

Nyakati fulani, halihewa hutupendeza; nyakati nyingine, hututamausha. Pindi kwa pindi, huwa muuaji kwa njia kama vile vimbunga, chamchela, ukame, dhoruba za theluji, au monsuni. Bila kujali kama waipenda au waichukia, waitukana au waipuuza, halihewa huwapo sikuzote, ikiathiri maisha zetu kuanzia siku tunayozaliwa mpaka siku tunapokufa.

Wakati mmoja mtu fulani alikejeli hivi: “Kila mtu huzungumza kuhusu halihewa, lakini hakuna mtu afanyaye chochote kuihusu.” Kwa kweli, sikuzote imeonekana kuwa halihewa inapita uwezo wetu wa kuibadili kwa njia yoyote. Hata hivyo, kwa kuongezeka, wanasayansi wengi hawaamini hivyo tena. Wanasema kwamba kurushwa kwa kaboni dioksidi na gesi nyingine kwenye angahewa yetu kunaleta badiliko katika vigezo vya halihewa vya muda mrefu—tabia ya nchi yetu.

Kulingana na wataalamu, ni nini asili ya badiliko hili linalokuja? Labda jibu lenye kuaminika zaidi latoka kwa shirika la Intergovernmental Panel on Climate Change (IPCC), ambalo lilirejezea ustadi wa wachunguzi zaidi ya 2,500 wa tabia ya nchi, wataalamu wa uchumi, na wataalamu wa utafiti wa hatari kutoka nchi 80. Katika ripoti yao ya 1995, IPCC lilifikia mkataa kwamba tabia ya nchi ya dunia inazidi kuwa yenye joto. Katika karne itakayofuata, ikiwa mambo yataendelea jinsi yalivyo, yawezekana kwamba halijoto ingeweza kuongezeka kufikia kiwango cha digrii 3.5 Selsiasi.

Ingawa ongezeko la digrii chache huenda lisisikike kuwa jambo lenye kutia wasiwasi, badiliko dogo la halijoto kwenye tabia ya nchi ya ulimwengu lingeweza kusababisha maafa. Yafuatayo ni mambo ambayo wengi hutabiri kuhusu karne ijayo.

Halihewa za kimkoa zipitazo kiasi. Katika maeneo fulani, ukame ungeendelea kwa muda mrefu, huku katika maeneo mengine, mvua ingekuwa nyingi zaidi. Dhoruba na mafuriko zingeweza kuwa kali zaidi; vimbunga, viwe vyenye kusababisha hasara zaidi. Ingawa tayari mamilioni hufa likiwa tokeo la mafuriko na njaa kali, ongezeko la halijoto la tufeni pote lingeweza kuongezea zaidi jumla ya vifo.

Ongezeko la hatari ya afya. Magonjwa yanayohusiana na joto na vifo yangeweza kuongezeka. Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, ongezeko la joto la tufeni pote lingeweza kueneza masafa ya wadudu ambao hubeba maradhi ya kitropiki, kama vile malaria na kidingapopo. Kwa kuongezea, kupungua kwa maji safi ya kutumia kwa sababu ya mabadiliko ya mvua ya kimkoa na theluji kungeweza kusababisha ongezeko katika maradhi fulani yasambazwayo na maji na chakula na vimelea.

Makao ya asili yatishwa. Misitu na kinamasi, ambayo huchuja hewa na maji yetu, ingeweza kuhatarishwa na halijoto zenye joto zaidi na mabadiliko katika mvua. Mioto ya misitu ingeweza kutokea mara nyingi na kuwa mikali zaidi.

Kupanda kwa usawa wa bahari. Wale wanaoishi katika maeneo ya pwani ya chini wangehitaji kuhama isipokuwa miradi yenye kugharimu kiasi kikubwa cha pesa ichukuliwe ili kuzuia bahari. Visiwa fulani vingezama kabisa.

Je, hofu kama hizo ni halali? Je, tabia ya nchi ya dunia inakuwa na joto zaidi? Ikiwa ndivyo, je, wanadamu ni wa kulaumiwa? Kukiwa na hatari hizi zote, haishangazi kwamba wataalamu wanajadili kwa nguvu maswali haya. Makala mbili zifuatazo zachunguza baadhi ya masuala yahusikayo na kushughulikia swali la kama twahitaji kuwa na wasiwasi kuhusu wakati ujao wa sayari yetu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki