Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 11/22 uku. 31
  • Nawa Mikono na Uipanguse!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nawa Mikono na Uipanguse!
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Njia za Kuboresha Afya Yako
    Amkeni!—2015
  • 2. Dumisha Usafi
    Amkeni!—2012
  • Njia Sita za Kutunza Afya
    Amkeni!—2003
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Afanya Utumishi wa Unyenyekevu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 11/22 uku. 31

Nawa Mikono na Uipanguse!

SISI hushikwaje na mafua na maambukizo mengine? Kulingana na shirika la Marekani la Wataalamu wa Kudhibiti Maambukizo na Magonjwa ya Kuenea, asilimia 80 ya magonjwa hayo huambukiza watu kupitia mikono, si kupitia hewa. Kwa kweli, kwa ujumla kunawa mikono huonwa kuwa njia moja muhimu zaidi ya kuzuia kuenea kwa ugonjwa. Lakini, mara nyingi wengi hawanawi mikono baada ya kwenda msalani au kufuta kamasi au kabla ya kushika chakula. Bila shaka, wengine wengi hunawa mikono sikuzote nyakati kama hizo. Lakini uwezekano wa kuambukizwa hauwezi kwisha baada ya kunawa mikono haraka-haraka na kijuujuu tu.

Kupangusa mikono vizuri kwaweza kuwa jambo la maana vilevile. Watafiti katika Chuo Kikuu cha Westminster nchini Uingereza waligundua kwamba watu wengi hawapangusi mikono vizuri baada ya kunawa, hasa wanapotumia vikausha-mikono yenye kutumia hewa moto. Baada ya kuvitumia wengi hupangusa mikono kwenye nguo zao. Kufanya hivyo kwaweza kueneza vijiumbe hatari vilivyobaki mikononi. Kulingana na watafiti, ni bora kupangusa mikono kabisa, hasa kwa kutumia karatasi za kupangusia au taulo safi ambayo haijatumiwa.

Vitovu vya Kudhibiti na Kuzuia Maradhi vya Marekani vyatoa madokezo yafuatayo ya kunawa mikono:

• Sikuzote tumia maji moto ya mfereji na sabuni. Ikikubidi kutumia beseni badala ya maji ya mfereji, isafishe kwa sabuni kila mara itumiwapo. Karatasi za kusafishia mikono zilizo na umajimaji hazisafishi mikono vizuri.

• Sugua mikono sana hadi povu lionekane, nawe uendelee kusugua kwa sekunde 15 hivi. Sugua juu na viganja vya mikono, na vilevile kati ya vidole, na chini ya kucha.

• Suuza mikono kwa maji moto ya mfereji.

• Ipanguse kwa karatasi ya kupangusia mikono iliyo safi iwezayo kutupwa, au taulo ambayo haijatumiwa, na uepuke kushika mfereji au mahali pa kuanikia taulo kwa mikono safi.

• Funga mfereji kwa kutumia taulo ili usiushike kwa mkono.

• Watoto wapaswa kunawa mikono wakiwa wamesimama kwenye urefu ambao mikono yao itaning’inia bila kizuizi kwenye maji ya mfereji. Saidia mtoto apitie hatua zote ambazo zimetajwa, kisha unawe mikono yako mwenyewe.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki