Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g98 12/8 uku. 3
  • Yesu Kristo Alikuwa Nani?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Yesu Kristo Alikuwa Nani?
  • Amkeni!—1998
  • Habari Zinazolingana
  • Yesu Alifananaje?
    Amkeni!—1998
  • Mwonekano Halisi wa Yesu Ulikuwaje?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova (Toleo la Watu wote)—2017
  • Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
  • Yesu Alikuwa na Sura ya Aina Gani?
    Maswali ya Biblia Yajibiwa
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1998
g98 12/8 uku. 3

Yesu Kristo Alikuwa Nani?

Wakati huu wa mwaka katika nchi nyingi ulimwenguni pote, kuna miadhimisho ya Krismasi. Mamia ya mamilioni ya watu wanaamini kwamba Yesu Kristo alizaliwa mnamo Desemba 25 miaka ipatayo 2,000 iliyopita. Kwenye picha na sanamu za kuchongwa, Yesu huonyeshwa kwa njia mbalimbali akiwa mtoto ndani ya hori. Lakini, bila shaka, alikua akawa mtu mzima akaishi duniani kwa miaka 33 1/2.

JE, UMEWAHI kujiuliza Yesu alifananaje alipokuwa mtu mzima? Alikuwa na rangi gani? Je, alikuwa mwenye misuli na mwenye sura nzuri, au alikuwa dhaifu na kuonekana mgonjwa-mgonjwa kwa njia fulani, kama ambavyo ameonyeshwa na wachoraji mbalimbali katika karne ambazo zimepita? Je, alinyoa ndevu au alikuwa na ndevu? Je, alikuwa na nywele ndefu?

Je, pia Yesu alikuwa na uzingo wa mtakatifu, kama vile nuru ambayo imezunguka kichwa chake kama achorwavyo na wachoraji fulani? Au alikuwa tofauti—kwamba hakuwa na mambo ya kumtofautisha na umati na angeweza kuchangamana nao?

Wanahistoria na wachoraji wa kilimwengu wametokeza mawazo yenye kuhitilafiana katika karne ambazo zimepita jinsi Yesu alivyofanana. Kwa kuongezea, vidokezi vyenye kutegemeka vimetolewa katika masimulizi ya watu waliomwona ambayo yaliandikwa na waandikaji wa Biblia walioishi katika karne ya kwanza walioandamana naye.

Hata hivyo, yafuatayo ni maswali muhimu kuliko jinsi alivyoonekana: Kwa kweli Yesu Kristo alikuwa nani? Anatimiza fungu gani katika kusudi la Mungu? Je, ametimiza fungu hilo? Yeye ni nani sasa, na yuko wapi? Je, ana wadhifa wa maana sana utakaoathiri wanadamu wote, hata wengi ambao wamekufa?

Kwanza, ebu tuchunguze uthibitisho kuhusu sura ya Yesu. Alifananaje?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki