Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 1/8 kur. 26-27
  • Roho Takatifu ya Mungu Ni Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Roho Takatifu ya Mungu Ni Nini?
  • Amkeni!—1999
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Nguvu Ikitenda
  • Utendaji Mbalimbali wa Roho Takatifu
  • Nguvu ya Mungu Inatumika kwa Niaba Yetu
  • Roho Takatifu Ni Nini?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • Kwa Nini Tuongozwe na Roho ya Mungu?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
  • Je, Roho Takatifu Ni Mtu?
    Amkeni!—2006
  • Kuongozwa na Roho ya Mungu Katika Karne ya Kwanza na Leo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 1/8 kur. 26-27

Maoni ya Biblia

Roho Takatifu ya Mungu Ni Nini?

“Basi watu wote walipokuwa wamebatizwa, yesu pia akabatizwa na, alipokuwa akisali, mbingu ilifunguliwa na roho takatifu katika umbo la kiwiliwili kama njiwa ikateremka juu yake, na sauti ikaja kutoka mbinguni: ‘wewe ni mwana wangu, mpendwa; nimekukubali wewe.’”—Luka 3:21, 22.

KATIKA hotuba yake kwa kikundi cha wanafalsafa katika Ugiriki ya kale, mtume Paulo alimwita Mungu “Bwana wa mbingu na dunia.” Paulo alisema kwamba ni Mungu huyu ndiye “aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyo katika huo” na ambaye “huwapa watu wote uhai na pumzi na vitu vyote.” (Matendo 17:24-28) Je, Mungu anatimizaje hayo yote? Ni kupitia roho takatifu yake, au kani ya utendaji.

Biblia inaeleza pia kwamba Mungu ana “wingi wa nishati yenye msukumo, yeye pia akiwa mwenye nguvu nyingi.” (Isaya 40:26, NW) Naam, Mungu aliuumba ulimwengu wote, jambo ambalo linadhihirisha nishati yenye msukumo na nguvu zake.

Nguvu Ikitenda

Isingekuwa sahihi kabisa kusema kwamba roho takatifu ni nguvu ya Mungu. Hii ni kwa sababu nguvu yaweza kufichika, au kukosa kutenda, katika mtu au kitu, kama vile nguvu zilizohifadhiwa katika betri iliyojazwa nguvu za umeme lakini ambayo haitumiki. Lakini Maandiko yanaionyesha roho ya Mungu ikiwa katika mwendo, kwa njia fulani ni kama vile mkondo wa umeme unaotoka katika betri inayotumika. (Mwanzo 1:2) Hivyo basi, roho takatifu ya Mungu ni nishati yake inayotenda, kani yake ya utendaji.

Nyakati nyingine Biblia hutaja roho takatifu ikiwa inatimiza kazi fulani au ikiwa mahali tofauti mbali na alipo Mungu. (Mathayo 28:19, 20; Luka 3:21, 22; Matendo 8:39; 13:4; 15:28, 29) Watu fulani ambao wameyasoma mafungu hayo wanakata kauli kwamba roho takatifu ina utu wake mbali na wa Mungu. Ni kwa nini usemi kama huu hutumiwa katika Maandiko? Je, roho takatifu ni kitu fulani kinachojitegemea mbali na Mungu?

Mungu Mweza Yote ana namna ya uhai iliyo juu zaidi na tofauti kabisa na viumbe vyake vya kimwili. Yeye ni roho, na hatuwezi kumwona kwa macho yetu. (Yohana 4:24) Biblia yatuambia kwamba Yehova Mungu anakaa mbinguni na kwamba yeye huwatazama wanadamu kutoka huko. (Zaburi 33:13, 14) Hili ni jambo linaloeleweka. Muumba lazima awe mkuu kuliko elementi anazofanyiza. Yeye huzitawala, huzifanyiza, na kuzidhibiti.—Mwanzo 1:1.

Kutoka makao yake yasiyoonekana, Mungu aweza kusababisha mambo yatendeke wakati wowote na mahali popote. Hivyo basi, si lazima awe mahali pale ambapo kani yake ya utendaji inatenda kazi. Yeye aweza kuituma roho yake itimize kazi fulani. (Zaburi 104:30) Hili laweza kueleweka kwa urahisi kwa watu wa siku hizi wanaotumia vifaa vya nyumbani kwa kutumia mashine ya mkono ya kuendesha vifaa kutoka mbali. Siku hizi sisi hutambua nguvu ya kani zisizoonekana kama vile umeme au miali ya mawimbi isiyoonekana. Hali kadhalika, Mungu, kwa kutumia kani yake takatifu isiyoonekana, au roho, aweza kutimiza lolote akusudialo kulifanya, pasipo yeye kutoka mahali pamoja hadi pengine.—Isaya 55:11.

Katika nyakati za Biblia wazo hili huenda lilikuwa gumu kueleweka. Kuifafanua roho takatifu kuwa kani tofauti bila shaka kuliwasaidia wasomaji kuelewa jinsi ambavyo Mungu hutumia nguvu zake hata ingawa yeye binafsi hawi mahali palepale inapotenda roho yake. Wakati ambapo Biblia huirejezea roho takatifu kuwa imefanya hivi au hivi, hiyo kwa kweli inamaanisha kwamba Mungu mwenyewe ameitumia au ameiweka nguvu yake juu ya wanadamu au vitu ili kutimiza mapenzi yake.

Utendaji Mbalimbali wa Roho Takatifu

Yehova aliitumia roho takatifu kuumba viumbe na vitu visivyo na uhai. (Zaburi 33:6) Vilevile Mungu aliitumia kukiangamiza kizazi cha wanadamu kisichotubu na chenye jeuri kwa kutumia gharika. (Mwanzo 6:1-22) Ni kani ya utendaji hiihii ambayo Mungu alitumia kuhamisha uhai wenye thamani wa Mwana wake hadi tumbo la uzazi la bikira Myahudi aitwaye Maria.—Luka 1:35.

Nyakati fulani, roho iliwapa wanadamu nguvu ili waseme kweli kwa ushujaa na kwa ujasiri mbele ya maadui, ingawa mara nyingi walihatarisha uhai wao. (Mika 3:8) Na ipo mifano mingi katika Biblia, hasa ile inayohusu unabii, ambapo wanaume na wanawake walipewa ufahamu wenye kina au uelewevu kupitia kani hii. Kwa kuwa hakuna mwanadamu awezaye kutabiri kwa usahihi yatakayotendeka wakati ujao, huu ni utendaji wenye kutokeza wa roho.—2 Petro 1:20, 21.

Pia roho yaweza kuwapa watu mmoja-mmoja nguvu za kufanya miujiza. Kwa kielelezo, kupitia kani hii, Yesu alidhibiti nguvu za asili, akaponya magonjwa, na hata akawafufua wafu. (Luka 4:18-21; 8:22-26, 49-56; 9:11) Roho ilihusika sana katika kuwapanga kitengenezo na kuwapa nguvu Wakristo wa mapema ili watumikie wakiwa mashahidi wa Mungu duniani pote.—Matendo 1:8; 2:1-47; Waroma 15:18, 19; 1 Wakorintho 12:4-11.

Nguvu ya Mungu Inatumika kwa Niaba Yetu

Je, inawezekana siku hizi kwa watumishi wa kibinadamu wa Mungu kufaidika na nishati hii isiyoweza kwisha? Ndiyo! Mungu huwapa watu wake kiasi fulani cha roho takatifu ili iwasaidie kuelewa na kutimiza mapenzi yake. Yeye huwapa roho yake wale wanaomwomba kwa moyo mweupe, walio na nia inayofaa na ambao wanajipatanisha na matakwa yake. (1 Wakorintho 2:10-16) Roho hiyo yaweza kuwaandalia wanadamu wasiokamilika “nguvu ipitayo iliyo ya kawaida,” ikiwawezesha kumtumikia Mungu kwa uaminifu ijapokuwa vizuizi. Kwa hiyo, bila shaka, watu wote wanaomhofu Mungu wana tamaa ya kuipata na kuihifadhi roho ya Mungu.—2 Wakorintho 4:7; Luka 11:13; Matendo 15:8; Waefeso 4:30.

Karibuni Mungu ataitumia kani hii yenye msukumo kukomesha ukosefu wa haki na kuteseka katika ulimwengu huu mwovu, na kwa njia hiyo akilitakasa jina lake kuu na takatifu. Roho takatifu itakuwa na uvutano mzuri katika ulimwengu wote, na matunda yake yatakuwa dhahiri kwa wote, ikimpa Mwanzilishi wake utukufu.—Wagalatia 5:22, 23; Ufunuo 21:3, 4.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki