Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 5/22 uku. 31
  • Je, Umewahi Kuona Samaki Akitembea?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Umewahi Kuona Samaki Akitembea?
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Unapokuwa Mgonjwa kwa Kula Samaki
    Amkeni!—2006
  • Ukuzaji Samaki—Samaki Wakiwa “Mifugo”
    Amkeni!—1995
  • Mbinu za Ndege za Kuvua Samaki
    Amkeni!—2011
  • Uwezo wa Samaki wa Kuogelea Katika Vikundi
    Amkeni!—2012
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 5/22 uku. 31

Je, Umewahi Kuona Samaki Akitembea?

NI JAMBO LA AJABU KAMA NINI! Nilikuwa nimesimama kwenye ukingo wa bwawa la mikoko, nikitazama kile nilichofikiri kuwa upwa wa matope matupu. Kumbe hayakuwa matupu. Kundi la wanasarakasi la kipekee lilikuwa likicheza. Ni la kipekee katika njia gani? Kila mmoja alikuwa na urefu upatao sentimeta 15. Walikuwa samaki.

Ijapokuwa kuwazia samaki wakitembea na kurukaruka laonekana kuwa jambo lisilowezekana kama vile tembo kupuruka, kwa wazi hivi ndivyo nilivyokuwa nikiona. Lakini inawezekanaje samaki atembee, apande, na kuruka—naam, hata apumue—akiwa nje ya maji?

Samaki niliowaona wanaitwa kirukatope au mudskipper. Baadhi ya mambo yasiyo ya kawaida kuwahusu ni macho yao, ambayo huchomoza kwenye kichwa chao kisha hujirudisha ndani. Jambo jingine ni mapezi yao ya kifua, ambayo kirukatope huyatumia kujisukuma—kama vile binadamu hutumia mikongojo kutembea-tembea. Lakini kirukatope huruka namna gani? Samaki huyu asiye wa kawaida anaweza kujirusha mwenyewe kwa kutumia mkia wake, akijivurumisha hewani kwa urefu upatao sentimeta 60. Pia kirukatope ni wahandisi-ujenzi hodari, wakitumia mapezi yao kama sepetu kuchimba vitundu ndani ya matope.

Samaki kirukatope ana tangi lake mwenyewe la oksijeni ndani yake—kinywa na mashavu yake, ambayo hujazwa maji “anapojirusha” juu ya nchi kavu. Oksijeni inapokwisha katika “tangi” lake, yeye hukimbia haraka hadi kwenye dimbwi la matope ili kulijaza upya.

Ikiwa unaweza kutembelea upwa wa matope katika Afrika au Asia na ikiwa waweza kuvumilia mbu na jua kali la kitropiki, mbona usimtafute kirukatope? Ndipo wewe pia utakapoweza kusema kwamba umemwona samaki akitembea!—Imechangwa.

[Hisani ya Picha katika ukurasa wa 31]

Mandharinyuma: Jane Burton/Bruce Coleman Inc.

Picha zilizopigwa chapa: Photographed by Richard Mleczko

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki