Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g99 7/8 kur. 12-13
  • Nchi ya Kihekaya ya Vinland Iko Wapi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Nchi ya Kihekaya ya Vinland Iko Wapi?
  • Amkeni!—1999
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Leif Eriksson Alivumbua Amerika?
    Amkeni!—2001
  • Maharamia wa Skandinavia Washindi na Wakoloni
    Amkeni!—2000
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2000
  • Ukurasa wa Pili
    Amkeni!—2001
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1999
g99 7/8 kur. 12-13

Nchi ya Kihekaya ya Vinland Iko Wapi?

Na mleta-habari wa Amkeni! katika Kanada

NCHI hiyo ilikuwa na ngano inayomea yenyewe, vijito vilivyojaa samaki aina ya salmoni, “beri za divai” (cranberries), zinazomea zenyewe, na majira ya baridi kali yasiyokuwa na theluji. Kulingana na hali za Milenia iliyopita, hii ilikuwa paradiso. Simulizi juu ya wanaume 36 wenye ujasiri waliosafiri huko lilikuwa msingi wa uchunguzi wa karne ya 20 wa kutafuta mahali ambapo huenda Wazungu walizuru huko Amerika Kaskazini.

Kati ya mwaka wa 990 na 1000 W.K., Leif Eriksson wa Skandinavia na watu wake walifunga safari ya uvumbuzi ya umbali wa kilometa 2,000. Alipokuwa akiabiri kwa mashua kuelekea upande wa kaskazini kandokando ya pwani ya magharibi ya Greenland na kisha kuelekea upande wa magharibi, Eriksson alifikia mabara mawili, aliyoyaita Helluland na Markland. Leo mabara hayo yanaonwa kuwa Kisiwa cha Baffin na Labrador. Mahali pa tatu walipofika pakawa fumbo—nchi ya kihekaya ya Vinland iko wapi?

Mnamo 1959, mwakiolojia Helge Ingstad na mkewe, Anne Stine Ingstad, wakaanza uchunguzi. Walikuwa na habari chache katika maandishi ya watu wa Norsemen, yanayoitwa Hadithi za Iceland, ambayo ni mchanganyo wa ukweli na hadithi za kubuniwa. Wenzi hao walisafiri kwa maelfu ya kilometa baharini, katika nchi, na angani, huku na huku katika pwani ya mashariki ya Amerika Kaskazini. Hatimaye walifanikiwa walipokutana kwa ghafula na jumuiya ndogo ya L’Anse aux Meadows, katika peninsula ya kaskazini ya kisiwa cha Newfoundland. Wakiwa huko mwenyeji mmoja, George Decker, aliwaongoza hadi eneo lililokuwa na kile kilichoonekana kuwa magofu ya nyumba yaliyokuwa yamefunikwa na vichaka.

Baada ya miaka saba ya kuchimba ilionekana kwamba historia ya mahali hapo ilikuwa imethibitishwa, jambo ambalo lilivutia uangalifu wa ulimwengu. Kwa kutokeza, Ingstad na mkewe walifukua nyumba nane zenye kuta za udongo na majani na pia pini ya shaba iliyotumiwa kufungia vazi. Yote haya yalionyesha dalili ya kwamba zilitoka Skandinavia. Mojawapo ya ugunduzi muhimu sana ulikuwa tanuri ndogo iliyotumiwa kuyeyusha chuma. Mavi ya chuma yaliyosalia yalionekana kuwa ya wakati ambao masimulizi yanaonyesha kwamba Eriksson aliwasili Amerika. Hatimaye uthibitisho uliopatikana ukaonekana kuonyesha kwamba kulikuwapo na watu wa Skandinavia katika Amerika Kaskazini.

Eneo ambalo sasa linaitwa L’Anse aux Meadows halipatani kabisa na maelezo ya hekaya juu ya Vinland. Huenda labda hatutaweza kamwe kupata kwa uhakika mahali penyewe hususa ilipokuwa. Lakini, ingawa huenda ikawa watu wa Skandinavia hawakuwa wa kwanza kuzuru Amerika Kaskazini, yaelekea kwamba waliwasili huko miaka 500 hivi kabla ya Columbus.

Unaweza kuzuru mahali hapo leo na kujionea jinsi walivyoishi watu hao wa Skandinavia. Unaweza kuona nyumba zilizojengwa upya kwa udongo na majani, na pia mfano wa meli ya watu wa Skandinavia ambayo huenda Eriksson alitumia katika safari yake maarufu ya baharini. Wafasiri wa mambo ya kihistoria wakiwa na mavazi ya kikale wanaweza kurudisha fikira zako miaka elfu iliyopita na kukusaidia ujiwazie ukiwa katika nchi ya watu wa Skandinavia.

[Ramani katika ukurasa wa 12]

GREENLAND

KISIWA CHA BAFFIN

LABRADOR

NEWFOUNDLAND

L’ANSE AUX MEADOWS

[Picha katika ukurasa wa 12]

Mashua iitwayo “Snorri,” ambayo ina urefu wa meta 16 ni mfano wa meli ya biashara ya watu wa Skandinavia iitwayo “knarr”

[Hisani]

Nordfoto/Carl D. Walsh

[Picha katika ukurasa wa 12, 13]

Nyumba zilizojengwa upya kwa udongo na majani katika L’Anse aux Meadows

[Hisani]

L’Anse aux Meadows National Historic Site/UNESCO World Heritage Site

[Picha katika ukurasa wa 13]

Leif Eriksson

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki