Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 3/8 uku. 11
  • Kufurahia Kuwatazama Ndege

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kufurahia Kuwatazama Ndege
  • Amkeni!—2001
  • Habari Zinazolingana
  • Kuwatazama Ndege—Je, Kwavutia Kila Mtu?
    Amkeni!—1998
  • Wakati Ndege Wanapogonga Majengo
    Amkeni!—2009
  • “Waangalieni kwa Makini Ndege”
    Amkeni!—2014
  • Mfungwa Aweza Kujifunza Nini Kutokana na Ndege?
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2001
g01 3/8 uku. 11

Kufurahia Kuwatazama Ndege

ULIMWENGU usio na ndege ungalikuwa tofauti kama nini! Sauti zao, nyimbo zao, rangi zao tofauti-tofauti na jinsi wanavyoruka—yote huchangia unamna-namna wenye kupendeza katika maisha. Lakini ni mara ngapi sisi hutua ili kuwasikiliza na kuwatazama? Ikiwa wewe ni mkazi wa mji wenye hekaheka nyingi na kelele za magari, huenda hata usiwaone ndege hao. Hata kama unaishi mashambani, ni rahisi kuwapuuza ndege kabisa. Hata hivyo, je, ungependa kuwachunguza kwa kindani ndege walioko eneo lako?

Unaweza kufanya hivyo kwa kuweka tu sinia la kuwalisha ndege uani, karibu na dirisha unapoweza kuwaona kwa urahisi. Kisha, unahitaji kuwa na jozi ya darubini na kamera yenye lenzi ya kuvuta—na uwe mvumilivu! Pia hakikisha una filamu yenye mwendo-kasi wa kupigia picha na kitabu chenye picha ili uwatambue ndege unaowatazama. Sasa, ni wakati wako wa kutazama, kusikiliza na kufurahia!

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki