Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g01 8/22 uku. 3
  • Unapotishwa

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Unapotishwa
  • Amkeni!—2001
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Mwisho Ulikuwa Mzuri?
  • Mfadhaiko wa Tukio Lenye Kutisha Ni Nini?
    Amkeni!—2001
  • Kuazimia Kumtumikia Yehova!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1994
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—2002
  • Babu na Nyanya Walio “Tofauti”
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2001
g01 8/22 uku. 3

Unapotishwa

“Nina kisu! Nyamaza, au nikuue!”

ILIKUWA alasiri nzuri ya kiangazi. Jane,a mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mmoja wa Mashahidi wa Yehova, alikuwa anacheza kwa kuteleza kwa viatu vya magurudumu katika bustani moja ya umma kule Virginia, Marekani. Ghafula ilionekana kana kwamba yeye pekee ndiye alibaki bustanini, akaamua kuondoka. Alipokuwa ameketi karibu na gari dogo la familia yao na kutoa viatu vya magurudumu, mtu fulani alimkaribia. Kwa maneno yenye kutisha yaliyo juu, huyo mtu alionyesha kwamba alitaka kufanya ngono na Jane, akajaribu kumsukuma ndani ya gari. Jane alipiga mayowe, lakini hakuacha kumshambulia.

‘Nilijisikia mdogo sana, kana kwamba nilikuwa mdudu na yeye alikuwa jitu,’ Jane alisema baadaye. “Lakini niliendelea kupiga mayowe na kupambana naye. Mwishowe nilimlilia Mungu kwa kusema, ‘Yehova, usimruhusu anitende hivyo!’” Inaonekana kwamba maneno hayo yalimshtua mtu huyo, kwa kuwa alimwachilia ghafula na kukimbia.

Mtu huyo aliyejaribu kumbaka Jane aliingia katika gari lake, naye Jane alijifungia katika gari lake akitetemeka. Alijilazimisha kutulia, akachukua simu ya mkononi. Akapigia polisi simu, na mshukiwa akakamatwa baada ya dakika chache tu kwa kuwa Jane aliweza kufafanua vizuri gari lake na namba yake.

Je, Mwisho Ulikuwa Mzuri?

Ndiyo, lakini si mara moja. Mateso ya Jane yalikuwa yameanza tu. Jane alisifiwa na polisi na katika magazeti kwa sababu ya kutenda bila kuchelewa na bila kuvurugika akili. Hata hivyo, baada ya mshtuko kwisha, Jane alihisi kwamba amevurugika akili kwelikweli. Anasema hivi: ‘Baada ya majuma machache nilianza kuwa na mfadhaiko. Nilikuwa na hofu ya daima iliyonizuia nisipate usingizi. Hata baada ya majuma kadhaa nilishindwa kujifunza au kuwa makini. Nilishikwa pia na hofu ya ghafula. Siku moja nilishtuka sana shuleni, mwanafunzi mwenzangu, anayefanana kidogo na yule mtu aliyenishambulia, aliponishika begani ili aniulize ni saa ngapi.’

Anasema hivi: ‘Nilishuka moyo sana. Niliacha kushirikiana na marafiki wangu, na upweke ulifanya nishuke moyo hata zaidi. Nilijilaumu kwa kuruhusu shambulio hilo, na nilihuzunika sana kwa kuwa sikuweza tena kuwa mwenye furaha na tumaini vile nilivyokuwa kabla ya shambulio hilo. Nilihisi kana kwamba nilikuwa mtu tofauti.’

Jane aliathiriwa na dalili za kawaida za mfadhaiko unaosababishwa na tukio lenye kutisha. Mfadhaiko huo ni nini, na wale wanaougua wanaweza kusaidiwaje? Sehemu inayofuata itajibu maswali hayo.

[Maelezo ya Chini]

a Jina limebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki