Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g03 7/22 uku. 3
  • Maoni Yanayotofautiana Kuhusu Ponografia

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Maoni Yanayotofautiana Kuhusu Ponografia
  • Amkeni!—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Madhara Yanayosababishwa na Ponografia
    Amkeni!—2003
  • Kwa Nini Ujiepushe na Ponografia?
    Vijana Huuliza
  • Ninaweza kuepukaje Ponografia?
    Amkeni!—2007
  • Ponografia—Je, Ina Madhara?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2013
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2003
g03 7/22 uku. 3

Maoni Yanayotofautiana Kuhusu Ponografia

“Huamsha hamu zisizofaa, huchochea tamaa ambazo hazipaswi kutoshelezwa.”—Tony Parsons, mwandishi wa habari.

JOHN hakukusudia kamwe kuzoea kutazama ‘ngono kwenye Internet.’a Kama ilivyo na watu wengi ambao kwa kushtukia hupata ponografia na vituo vya maongezi ya ngono, siku moja alipokuwa akitumia Internet alijikuta ghafula katika kituo cha aina hiyo. Muda si muda, akazoea kabisa kutazama ngono kwenye Internet. “Nilikuwa nikingoja mke wangu aende kazini,” akumbuka, “kisha ningetoka mbiombio kitandani na kutumia kompyuta kwa saa nyingi.” Nyakati nyingine alitumia kompyuta kwa vipindi virefu bila kula wala kunywa chochote. Anasema, “sikuwa nikihisi njaa.” Alianza kumdanganya mke wake kuhusu shughuli zake za siri. Zoea hilo likaanza kumfanya akose kuwa makini kazini, na kuwa na wasiwasi mwingi zaidi. Matatizo yakaanza kuipata ndoa yake, na hatimaye alipopanga kukutana ana kwa ana na rafiki yake wa ngono kwenye Internet, mkewe alijua jambo hilo. Leo hii John anatibiwa kwa sababu ya zoea lake.

Watu wanaopinga ponografia hutumia visa kama hivyo kuthibitisha kwamba ponografia ina madhara. Wanadai kwamba inaharibu mahusiano, inawashushia wanawake heshima, inawadhulumu watoto, na kueneza maoni yaliyopotoka na yenye kudhuru kuhusu ngono. Kwa upande mwingine, wale ambao wanaunga mkono ponografia wanasema ni uhuru na wanawaona wale wanaoipinga kuwa watu wanaojiona kuwa wema mno. Mtetezi mmoja anaandika kwamba “watu hawapaswi kuonea aibu mapendezi au tamaa zao za ngono. Ponografia inaweza kutumiwa kuanzisha na kuchochea mazungumzo ya wazi kuhusu ngono.” Baadhi yao hata wanadokeza kwamba kuenea kwa ponografia huonyesha kwamba jamii imekomaa kiakili na ina uhuru. “Jamii iliyokomaa vya kutosha kuona picha za wazi za watu wazima wanaofanya ngono kwa hiari yao yaelekea inaweza kukubali aina mbalimbali za ngono na usawa wa wanawake,” asema mwandishi Brian McNair.

Je, maoni yanayotofautiana katika jamii yanafanya ponografia iwe yenye kukubalika? Kwa nini imeenea sana? Je, kweli ponografia ni hatari? Makala zifuatazo zitajibu maswali hayo.

[Maelezo ya Chini]

a Majina yamebadilishwa.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki