Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g03 12/8 uku. 31
  • Jina la Mungu Kwenye Jumba la Kifalme

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Jina la Mungu Kwenye Jumba la Kifalme
  • Amkeni!—2003
  • Habari Zinazolingana
  • Hifadhi ya Nyumba za Mbao
    Amkeni!—2004
  • Kwa Nini Watu Hulibusu Jiwe la Blarney?
    Amkeni!—2004
  • Yerusalemu Siku za Mitume
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1977
  • Bratislava Kutoka Kuwa Kivuko cha Kale cha Mto Hadi Kuwa Jiji Kuu la Kisasa
    Amkeni!—2000
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2003
g03 12/8 uku. 31

Jina la Mungu Kwenye Jumba la Kifalme

NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI SLOVAKIA

SLOVAKIA ni nchi ndogo yenye kupendeza sana katikati ya Ulaya. Eneo lake la mashambani lenye kuvutia lina majumba mengi ya kifalme yanayoonyesha utajiri na historia ndefu ya eneo hilo. Mojawapo ya majengo yenye kuvutia ni Jumba la Kifalme la Orava, lililojengwa juu ya majabali ya chokaa yenye urefu wa meta 112 yaliyo karibu na kijiji.

Maandishi ya kwanza kuhusu Jumba la Kifalme la Orava ni ya mwaka wa 1267. Tangu wakati huo limemilikiwa na watu mbalimbali. Mnamo mwaka wa 1556, jumba hilo lilimilikiwa na familia tajiri ya Thurzó. Familia hiyo ilirekebisha na kupanua jengo hilo na pia ilijenga kanisa dogo.

Kila mwaka makumi ya maelfu ya wageni kutoka nchi nyingi huja kuona Jumba la Kifalme la Orava na vivutio vingine. Katika ua, wageni wanaweza kuona jambo la kupendeza kwenye mchongo wa nembo ya familia ya Thurzó uliotengenezwa kwa jiwe-mchanga. Mchongo huo unaonyesha jina la Mungu lililo katika Biblia, Yehova, katika Kilatini.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki