Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g05 6/8 uku. 14
  • Ondoa Moshi Unaoua

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ondoa Moshi Unaoua
  • Amkeni!—2005
  • Habari Zinazolingana
  • Nahitaji Kujua Nini Kuhusu Uvutaji wa Sigara?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 1
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Kuvuta Sigara?
    Amkeni!—2011
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2004
  • Je! Unaweza Kumpenda Jirani Yako na Bado Uvute Sigara?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1981
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2005
g05 6/8 uku. 14

Ondoa Moshi Unaoua

TAKWIMU zinatia wasiwasi: Watu watatu hufa nyumbani mwao kila dakika, kila siku. Kisababishi ni moshi.

Moshi wa aina gani? Moshi ambao huenda ukatokana na samadi kavu, mbao zilizooza, matawi, nyasi, au mabaki ya mimea. Gazeti The Kathmandu Post la Nepal linaripoti kwamba thuluthi ya watu ulimwenguni, zaidi ya watu bilioni mbili, hutumia vitu hivyo kupika na kupasha nyumba joto. Mara nyingi, vitu hivyo hutumiwa na maskini.

Kwa kusikitisha, vitu hivyo vinapochomwa, hutokeza gesi zenye sumu. Kwa hiyo, ni nini kinachoweza kufanywa? Shirika la Intermediate Technology Development Group (ITDG), linalowasaidia watu katika nchi nyingi kuboresha maisha yao linasema: “Ni rahisi sana kusuluhisha tatizo la uchafuzi wa hewa ndani ya nyumba: ama uzuie moshi usiingie ndani ya nyumba au uuondoe.”

Dokezo la kwanza ni kupikia nje. Hata hivyo, namna gani ikiwa haiwezekani au jambo hilo halipendezi? Shirika la ITDG linapendekeza uboreshe sehemu za kupitishia hewa. Kuna njia mbili za kufanya hivyo—kutoboa mashimo ukutani karibu na paa (wavu wa waya utazuia wanyama wadogo) na kuweka madirisha (madirisha ya mbao yatazuia watu wasitazame ndani). Jambo hilo hufanya hewa izunguke na kutoa moshi nje. Hata hivyo, kutoboa mashimo ukutani hakufai ikiwa moto unawashwa ili kupasha chumba joto, kwa hiyo, njia nyingine rahisi inaweza kutumiwa.

Shirika la ITDG linasema kwamba njia bora na inayopendekezwa ni kutumia mabomba ya kutolea moshi. Mabomba hayo yanaweza kutengenezwa bila gharama kubwa kwa kutumia mabati au hata matofali na udongo. Mabomba hayo makubwa huwekwa juu ya moto nayo hutoa moshi nje kupitia paa. Wataalamu wanasema kwamba sehemu za kuingizia hewa zinapowekwa karibu na paa na mabomba ya kutolea moshi yanapotumiwa, hewa zenye sumu ndani ya nyumba hupunguzwa kwa asilimia 80 hivi. Watu wanaotumia mabomba ya kutolea moshi husema kwamba wamekuwa na afya bora zaidi, wamekuwa safi zaidi, wanaweza kufanya kazi nyingi zaidi, na wanafurahia kuwa nyumbani. Hilo linaonyesha wazi kwamba jambo rahisi sana linaweza kuboresha maisha.

[Picha katika ukurasa wa 14]

Jiko lililo ndani ya nyumba nchini Kenya lenye bomba la kutolea moshi, mianya mikubwa na madirisha

[Hisani]

Dr. Nigel Bruce/www.itdg.org

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki