Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/06 uku. 3
  • Je, Ndiyo Miaka Bora Zaidi?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je, Ndiyo Miaka Bora Zaidi?
  • Amkeni!—2006
  • Habari Zinazolingana
  • Yehova Amenisaidia Kwelikweli
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2014
  • Jinsi Makusanyiko Matatu Yalivyobadili Maisha Yangu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2009
  • “Kutoka Kinywani mwa Watoto Wachanga”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Kweli ya Biblia Iliwaweka Huru
    Amkeni!—2011
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2006
g 2/06 uku. 3

Je, Ndiyo Miaka Bora Zaidi?

NI SAA 12:30 alfajiri wakati wa majira ya baridi kali huko Soweto, Afrika Kusini. Lazima Evelyn aamke.a Kwa kuwa nyumba yake haina mfumo wa kupasha joto, yeye huhisi maumivu mengi anapoamka.

Kwa uchungu anashusha miguu yake iliyoathiriwa na yabisi-kavu kutoka kitandani. Kisha anaketi na kungoja. Polepole maumivu katika miguu yake yanapungua. Evelyn sasa anajikaza na kusimama. Anatoa sauti kwa uchungu. Akiwa amejishika kiunoni, kama vile tu “panzi hujikokota,” Evelyn anajikokota hadi kwenye bafu.—Mhubiri 12:5.b

Evelyn anajiambia, ‘Nimefaulu kweli!’ Ameishi kuona siku nyingine na vilevile ameweza kusogeza mwili wake wenye maumivu.

Hata hivyo, ana wasiwasi mwingine. “Ninahofu kwamba nitavurugika kiakili,” anasema Evelyn. Mara kwa mara yeye husahau mahali alipoacha funguo zake, lakini bado akili yake iko chonjo. Evelyn anasema: “Ninatumaini kwamba akili yangu haitavurugika kama ya wazee fulani.”

Alipokuwa kijana, Evelyn hakufikiria kuhusu matatizo ya uzeeni. Ghafula, miaka imesonga, na sasa mwili wake humkumbusha kila mara kwamba ana umri wa miaka 74.

Wengine wanaoishi katika hali nzuri kuliko Evelyn na wasio na magonjwa mabaya na mfadhaiko wanaweza kuona maisha ya uzeeni kuwa ndiyo miaka bora zaidi. Kama vile mzee wa ukoo Abrahamu, wanaweza kufikia ‘umri mwema wa uzee, wakiwa wazee na wenye kutosheka.’ (Mwanzo 25:8) Wengine huiona kuwa “siku na miaka yenye kuhuzunisha” na wanaweza tu kusema “sifurahii maisha.” (Mhubiri 12:1, Today’s English Version) Katika uchunguzi mmoja, watu wengi sana walikuwa na maoni mabaya kuhusu kustaafu hivi kwamba gazeti Newsweek lilidokeza miaka ya uzeeni iitwe “miaka ya giza.”

Una maoni gani kuhusu uzee? Wazee hukabili magumu gani? Je, inawezekana mtu azeeke bila uwezo wake wa akili kupungua? Ni nini kinachoweza kufanywa ili kuchochea amani ya akili katika miaka hiyo bora ya uzeeni?

[Maelezo ya Chini]

a Majina fulani katika makala hizi yamebadilishwa.

b Simulizi hili katika kitabu cha Biblia cha kale cha Mhubiri limetambuliwa kwa muda mrefu kuwa linafafanua kwa undani na kwa njia ya kishairi matatizo ya uzee.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki