Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 4/09 uku. 3
  • Wanafunzi Waliofadhaika

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Wanafunzi Waliofadhaika
  • Amkeni!—2009
  • Habari Zinazolingana
  • “Asanteni kwa Mfululizo Huo!”
    Amkeni!—2011
  • Yehova Hatasahau Kazi Yenu Enyi Vijana!
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2003
  • Binti Yako Anapokuwa na Mkazo
    Amkeni!—2014
  • Wazazi Wanaweza Kusaidia Jinsi Gani?
    Amkeni!—2009
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2009
g 4/09 uku. 3

Wanafunzi Waliofadhaika

JENNIFER mwenye umri wa miaka 17 alikuwa mmoja kati ya wanafunzi bora kabisa katika darasa lake. Alishiriki katika utendaji mwingi wa baada ya shule na aliheshimiwa na walimu na washauri wa shule. Lakini mwaka mmoja kabla ya kumaliza shule, alianza kuumwa sana na kichwa na kupatwa na kichefuchefu mara nyingi. Anahisi kwamba alikuwa mgonjwa kwa sababu ya saa nyingi alizotumia kukazia sana fikira kazi za shule na kukosa usingizi.

Kuna wanafunzi wengine wengi walio na matatizo kama ya Jennifer. Inaonekana kwamba idadi ya wanafunzi wanaokabili mfadhaiko mwingi shuleni inaongezeka na wengine wanatafuta msaada wa madaktari wa matatizo ya akili. Kwa sababu hiyo, kikundi cha walimu Wamarekani kimeanzisha programu ya kupunguza hali zinazochangia mfadhaiko wa wanafunzi shuleni. Programu hiyo inaitwa Jitahidi Kufanikiwa.

Ikiwa wewe ni mwanafunzi, kama Jennifer huenda unakabili mfadhaiko. Au ikiwa wewe ni mzazi huenda ukaona jinsi mwana au binti yako anavyoshinikizwa sana afaulu shuleni. Wanafunzi na wazazi wanaweza kupata wapi mwongozo unaofaa?

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki