Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 7/10 uku. 3
  • “Tunakuachisha Kazi”

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Tunakuachisha Kazi”
  • Amkeni!—2010
  • Habari Zinazolingana
  • Kupata Faraja Katika “Bonde la Uvuli wa Mauti”
    Amkeni!—1998
  • “Msiwe na Wasiwasi Juu ya Kesho”
    Amkeni!—2010
  • Pigo la Ukosefu wa Kazi ya Kuajiriwa
    Amkeni!—1996
  • “Kinanisaidia Kugusa Mioyo ya Watu”
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2010
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2010
g 7/10 uku. 3

“Tunakuachisha Kazi”

WASIMAMIZI wa kampuni walimwona Fred kuwa mfanyakazi bora.a Mbinu zake zilikuwa zimesaidia kampuni hiyo kupata faida kubwa katika miaka sita ambayo alikuwa ameajiriwa. Kwa hiyo, alipoitwa kwenye ofisi ya meneja mmoja, Fred alitazamia kwamba angeongezwa mshahara au kupandishwa cheo. Badala yake, meneja huyo alimwambia, “Tunakuachisha kazi.”

Fred hakuamini alichokuwa amesikia. “Nilikuwa nikipata mshahara mnono na nilikuwa nikifurahia kazi yangu, lakini kila kitu kilibadilika ghafula,” akasema. Baadaye, Fred alimwambia mke wake Adele kile kilichokuwa kimetokea, naye pia akashtuka sana. Adele anasema hivi: “Nilijihisi hoi kabisa. Nilijiuliza, ‘Sasa tutafanya nini?’”

Mamilioni ya watu hupatwa na hali iliyompata Fred kama unavyoweza kuona katika tarakimu zilizo hapa chini. Hata hivyo, tarakimu pekee hazionyeshi jinsi watu wanavyoathiriwa kihisia wanapofutwa kazi. Fikiria kisa cha Raúl, mhamiaji kutoka Peru ambaye aliachishwa kazi katika hoteli moja kubwa huko New York City ambako alikuwa ameajiriwa kwa miaka 18. Raúl alijaribu kutafuta kazi, lakini hakufaulu. Anasema hivi: “Nilikuwa nimeiandalia familia yangu mahitaji yake kwa miaka 30 hivi. Sasa nilihisi kuwa nimeshindwa kutimiza wajibu wangu nikiwa kichwa cha familia.”

Kisa cha Raúl kinaonyesha kwamba watu wanaopoteza kazi hupatwa na matatizo mengi zaidi ya yale ya kiuchumi. Mara nyingi, wanapatwa na maumivu makali ya kihisia. “Nilianza kuhisi kuwa sifai kitu,” anasema Renée ambaye mume wake anayeitwa Matthew alikuwa ameachishwa kazi kwa zaidi ya miaka mitatu. “Ikiwa huna pesa, watu huanza kukudharau, na baada ya muda wewe pia unaanza kujidharau.”

Mbali na maumivu ya kihisia, mtu ambaye ameachishwa kazi huanza kukabiliana na ugumu wa kuishi kwa mapato madogo. Fred anasema: “Tulipokuwa na pesa hatukuwahi kufikiria kuhusu kupunguza matumizi. Lakini sasa tulikuwa hatuna kazi, na gharama zilikuwa zilezile, kwa hiyo, tulilazimika kupunguza matumizi yetu.”

Unapotafuta kazi, unahitaji kukabiliana na mahangaiko ya kiakili na kihisia yanayosababishwa na kukosa kazi. Pia unahitaji kupunguza gharama zako. Kwanza, acheni tuchunguze hatua mbili unazoweza kuchukua ili kukabiliana na matatizo ya kihisia.

[Maelezo ya Chini]

a Baadhi ya majina katika mfululizo huu yamebadilishwa.

[Grafu katika ukurasa wa 3]

(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)

Idadi ya Watu Ambao Hawakuwa na Kazi Katika Mwaka wa 2008 Katika Nchi Tatu Tu

Japani 2,650,000

Hispania 2,590,000

Marekani 8,924,000

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki