Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g 2/11 uku. 29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—2011
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Marafiki Wachache wa Kweli
  • Meli za Kusafirishia Dawa za Kulevya
  • Faida za Familia Kula Pamoja
  • Je, Kula Pamoja Kunaweza Kuimarisha Familia Yako?
    Amkeni!—2010
  • Kuutazama Ulimwengu
    Amkeni!—2012
  • Kisanduku cha Mlo Chatoa Ushahidi
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1995
  • Jinsi Ambavyo Dawa za Kulevya Haramu Huathiri Maisha Yako
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—2011
g 2/11 uku. 29

Kuutazama Ulimwengu

Karibu robo ya Wajerumani walio chini ya umri wa miaka 40 wanaona ni muhimu kusali kila siku pamoja na watoto, na kati ya wale wanaoenda kanisani, ni watu 4 tu kati ya 10 wanaoona jambo hilo kuwa muhimu.—APOTHEKEN UMSCHAU, UJERUMANI.

Mtu fulani aliyetoa shahawa iliyokuwa na mabadiliko fulani katika chembe za urithi yanayohusianishwa na ugonjwa wa moyo aliwapitishia ugonjwa huo watoto 9 kati ya 24 wanaosemekana kuwa wake. Kati ya hao mmoja wao alikufa kutokana na ugonjwa wa moyo akiwa na umri wa miaka miwili.—JAMA, MAREKANI.

“Zaidi ya asilimia 50 ya Warusi wanaamini kwamba ufisadi hauwezi kuepukwa na ni sehemu ya kudumu ya maisha.”—RIA NOVOSTI, URUSI.

Marafiki Wachache wa Kweli

“Mwingereza wa kawaida ana marafiki watatu tu wa kweli ambao anaweza kuwategemea,” linasema gazeti Daily Telegraph la London. Kulingana na uchunguzi mmoja, baadhi ya sababu zinazowafanya watu waache kuwasiliana na “marafiki 36 hivi kadiri miaka inavyopita” ni “maisha yenye shughuli nyingi,” ‘kuacha kuwa na uhusiano wa karibu’ na, asilimia 43 kati ya wale waliochunguzwa walisema kwamba sababu nyingine ilikuwa, “kukosana . . . na kuamua kwamba hawatawahi kuwasiliana tena.” Karibu asilimia 20 huwaeleza wafanyakazi wenzao mambo yao ya siri kwa kuwa “hakuna mtu mwingine wanayeweza kuomba mashauri.” Msemaji wa wale waliofanya uchunguzi huo alisema: “Unahitaji sifa ya pekee ili uaminiwe na kutegemewa.”

Meli za Kusafirishia Dawa za Kulevya

Walanguzi wa dawa za kulevya nchini Kolombia wanaboresha mbinu zao za kuingiza kokeini katika nchi za Amerika ya Kati, Marekani, na Mexico. Tangu mwaka wa 1993, meli 42 hivi za kusafirishia dawa za kulevya zinazokaribia kufanana na nyambizi zimenaswa na wenye mamlaka nchini Kolombia. Karakana kadhaa ambako meli hizo hutengenezewa zimepatikana pia. Ingawa meli hizo zinazotumia dizeli haziwezi kuingia chini kabisa ya maji, ni vigumu sana kuziona kwenye rada. Nyingine zinaweza kwenda umbali wa kilomita 3,200, na zinaweza kubeba zaidi ya tani sita hadi kumi za kokeini, na huenda zikagharimu dola milioni moja hivi (za Marekani) kujenga.

Faida za Familia Kula Pamoja

Idadi isiyozidi nusu ya vijana Wafini wenye umri wa miaka 14 hadi 16 waliohojiwa katika uchunguzi wa hivi karibuni walisema kwamba wao hula pamoja na familia zao. Uchunguzi huo ulionyesha kwamba katika nyumba nyingi hakuna milo inayoandaliwa. Hata hivyo, vijana hutazamia sana pindi hizo za kawaida na zenye kustarehesha za kuwa pamoja na familia zao. Walipoulizwa kile walichotaka kutoka kwa wazazi wao, walisema hivi waziwazi: “Vyakula moto, kula pamoja tukiwa familia, na mtu anayesikiliza na aliye na wakati wa kuwa pamoja nasi,” linaripoti gazeti Helsingin Sanomat. Kula pamoja kama familia kunaathiri afya ya akili ya kijana kwa njia kubwa. Kulingana na gazeti hilo, “vijana ambao hula pamoja na familia zao hufanya vizuri shuleni, hawavuti sigara, hawatumii kileo, au kutumia dawa za kulevya, na hawashuki moyo mara nyingi.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki